Pamoja na Bodi kumpendekeza, Dk Rashid aweka sharti la kurudi TANESCO!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,037
22,728
Dk Rashid awekasharti la kurudi Tanesco !
Na Sadick Mtulya - Mwananchi.

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (Tanesco), Dk Idris Rashid ametoa sharti la kurudi kwenye nafasi hiyo nyeti baada ya kupendekezwa na bodi ya wakurugenzi.

Nafasi ya mkurugenzi mkuu wa Tanesco imekuwa wazi tangu Dk Idris alipostaafu baada ya kumaliza kipindi chake. Kustaafu wake kuliacha msuguano mkubwa baina ya bodi hiyo na menejimenti, na baadaye bodi ilipendekeza gavana huyo wa zamani wa benki arejeshwe kwenye kiti hicho.

Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa Dk Rashid, ambaye mpango wake wa kununua jenereta za kampuni binafsi ya Dowans Tanzania Limited ulipingwa vikali na Bunge, sasa anataka wanasiasa wasimuingie kwenye kazi yake iwapo atarejea kuliongoza shirika hilo.

Kwa mujibu wa habari hizo, bodi ya Tanesco imefikia hatua ya kupendekeza Dk Rashid arudi Tanesco baada kuwepo na mgogoro wa kiutendaji baina yake na menejimenti ya shirika hilo.

"Kutokana na mvutano uliopo wa kiutendaji na matatizo yanayolikabili shirika kwa sasa, bodi inaamini Dk Rashid ndiye anayeweza kumudu hali hiyo," chanzo cha habari kililidokeza gazeti hili.

"Lakini moja ya masharti aliyotoa ni kutaka asiingiliwe kiutendaji na wanasiasa"


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco, Peter Ngumbuli jana hakutaka kuthibitisha suala hilo na kueleza kwa kifupi kuwa, bodi imeshamaliza kazi yake na kuiachia serikali.

"Ninachoweza kukuambia ni kuwa Bodi imeshatoa mapendekezo yake na kuyakabidhi serikalini kupitia Wizara ya Nishati na Madini," alisema Ngumbuli bila ya kufafanua.

Hata hivyo, Ngumbuli alisema kutokana na unyeti wa nafasi hiyo, bodi iliamua kuunda kamati ndogo kutoka nje ya Tanesco iliyoratibu mchakato mzima, ikiwemo kupitia majina ya watu waliojitokeza kuomba nafasi hiyo.

"Bodi ilipotangaza kazi ya nafasi ya mkurugenzi mtendaji mpya, ilikabidhi majukumu yote kwa kamati ndogo iliyoundwa nje ya Tanesco na yenyewe ndiyo iliratibu mchakato mzima ikiwemo kupitia majina ya watu wote waliojitokeza kuomba nafasi hiyo," alisema Ngumbuli.

Awali chanzo cha habari kilieleza kuwa mgogoro ndani ya Tanesco unatokana na kila upande- bodi shirika hilo na menejimenti- kutaka kuwa na nguvu katika uamuzi wa mkurugenzi mtendaji atakayeteuliwa kushika wadhifa huo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Tanesco zinaeleza kuwa watendaji wa ngazi za ukurugenzi waliandika barua za kuomba nafasi hiyo ya Dk Idris.

Mgogoro wa kiutendaji uliopo Tanesco ulibainishwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

Kutokana na hali hiyo, POAC iliwapa onyo watendaji hao kuacha makundi na kuwasisitizia waongeze jitihada katika utendaji ili waliokoe shirika hilo, ambalo limeelezwa kuwa liko hatarini kufilisika.

POAC, iliyo chini ya uenyekiti wa Zitto Kabwe, ilitoa onyo na maagizo hayo Aprili 6 mwaka huu katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa baina ya kamati hiyo na watendaji wakuu Tanesco na kiliitishwa kujadili matumizi ya fedha ya mwaka 2008.

Katika kikao hicho, Ngumbulu alikiri kuwepo kwa matatizo ya kiutendaji ndani ya shirika hilo na kusema ndiyo yanayosabisha kwa kiasi kikubwa shirika hilo kutetereka

Ni mara chache nakosa la kusema lakini leo hakika sina la kusema, niseme nini ? Ni mtu mmoja tu Tanzania anayeweza kuiendesha TANESCO hata kama mtu huyo kachafuka namna gani ! Jamani kuendesha nchi si mchezo, Mungu inusuru Tanzania !
 
Hii nchi inasikitisha sana.Ngoja wamrudishe akaikamilishe 'kazi' aliyoianza...Sasa sijui ilikuwa na maana gani kutangaza nafasi hiyo na watu wakaaply.Au sheria zao za mapendekezo zinaruhusu kumpendekeza hata asiyeshiriki kwenye mchakato?
 
Dont tell me hatuna watu wa kuongoza Tanesco isipokuwa Dr Rashid tu!
 
Kama ni body iliyo jaa vilafi wale wale kweli tunategemea watampendekeza mtu atakae watolea mlo wao. Tazama alafu pendekezo lake asiingilwe kwenye kuwapatia mlo body members, chanzo hicho hicho kilicho watoa imani nae hata hao wazembe huko bungeni. I mean kwenye mchi ambayo utapeli unatendeka kila kukicha hadi wabunge waseme ujue jamaa alizidi. Aendelee tu kula pension labda wa change na body yenyewe yote guarantee tutapata kiongozi mpya.
 
he is the best in pool :gossip:

Hata mimi labda ningesema hivyo. Wakati wa kuchagua kuna vitu vingi vinaangaliwa na mojawapo ni maslahi ya mwenye kuchagua. Kama ndiye pekee anaweza kulinda maslahi yangu then he is the best.

... Kwani tumesahau kuwa katika TZ hakuna tena kitu kinaitwa maslahi ya umma?
 
Haya mambo yameanza
Kuna ile miradi mikubwa ya umeme ya mabilioni iliyotangazwa na serikali hivi karibuni, yaonekana hakuna mwingine bali Dr. Idris Rashidi kuisimamia. Sababu ziko nyingi lakini kubwa ni ile ya historia kujirudia. Kwanza huu ni mwaka wa uchaguzi na pili kuna chama kinatafuta na kimepanga kutumia bilioni 50 katika kampeni zake.

Hosea yuko pale pale, Ndullu kishawekwa mfukoni, Dr. Dau azidi kumwagiwa sifa na timu inamkosa tu mtu moja, Dr. Idris. Shemeji zao EPA na Richmond nao wamekaa mkao wa kula - kweli mwaka wa uchaguzi una mambo !
 
Haya ni matusi makubwa sana kwa wasomi wengine wa kitanzania. Hivi kweli bila Idris Rashid kuwepo Tanesco hilo shirika litakufa??!! Jamani wakati mwingine wawe wanajua kuchagua aina ya matusi, haya si mazuri kabisa. Tuna vichwa kibao vya kuweza kuendesha hata nchi ije kuwa Tanesco.
 
Mbali ya Peter Ngumbulu hivi hii bodi ya Tanesco wajumbe wengine ni akina nani?............mwenye kujua please anisaidie kunipa majina yao hapa bodini JF
 
Haya ni matusi makubwa sana kwa wasomi wengine wa kitanzania. Hivi kweli bila Idris Rashid kuwepo Tanesco hilo shirika litakufa??!!
Ni yeye tu anayeweza kulinda maslahi yao kwa ufanisi wa hali ya juu potelea mbali hata nchi ikiingia gizani. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Mh. Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma, yasemekana anakubaliana nao kwamba Dr. Rashidi is the Best CEO ever - hakuna kama yeye nchini.

Jamani wakati mwingine wawe wanajua kuchagua aina ya matusi, haya si mazuri kabisa. Tuna vichwa kibao vya kuweza kuendesha hata nchi ije kuwa Tanesco.
Hivyo vichwa vingine yasemekana havina nguvu na jeuri ya Dr. Rashidi aliyetaka kulazimisha ununuzi wa mitambo ya Dowans la sivyo nchi ikumbwe na giza totoro. Yasemekana kwa hili nalo aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na sasa katoa sharti lingine la kutoingiliwa katika utendaji wake - mmh, kazi kweli kweli.
 
Tangu wakati ule alipolazimisha zinunuliwe la sivyo tungeingia katika giza, mbona hazijanunuliwa na hatupo kwenye giza? na akirudi zisiponunuliwa tutaingia kwenye giza kweli.
 
natafuta jeshi la uasi la Tanzania nijiunge nalo maana hivi nilivyo CCM wananiua na uchaguzi ni wizi mtupu si bora nijaribu kuwatoa huenda nikafanikiwa
 
Hata kwa kutumia ufahamu wangu mdogo wa taaluma ya nishati, nafikiri TANESCO ni moja ya mashirika magumu sana kuyaendesha Tanzania. sio kwamba kwa sababu ni kubwa, lakini kutokana na kuingiliwa sana na wanasiasa wakiwa na agenda zao za siri. Hakuna ubishi kuwa ni shirika kubwa ambalo kiutendaji linafaa kuvunjwa na kuwa kampuni tatu, uzalishaji, usafirishaji na ugawaji, na mwisho ufungaji kwa wateja. I hope haya ndio mapendekezo yaliyokuwa yamewasilishwa na Net Group.
 
Watu zaidi ya 50 wajitokeza kuwania ukurugenzi Tanesco
WATU zaidi ya 50 wamejitokeza kuomba nafasi ya Mkurugenzi Mkuu Tanesco iliyotangazwa Septemba 18, mwaka huu na Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.


Source Mwananchi 16th October 2009
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom