Pamoja kuwa ni washindani kuwania roho za watu, mustakabali wa tz ni wetu sote

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
173
Ni ukweli usiofichika kuwa ukiacha madhehebu ya dini, hakuna taasisi au chombo chochote chenye uwezo wa kuimbia CCM we acha unavyofanya si vizuri.
Ulipotoka waraka wa Kanisa la Kikatoliki kuhusu uchaguzi mkuu ujao, nimekuwa mmoja wa watu ambao naamini kama taasisi ya kidini imechukua nafasi yake kuiadharisha jamiii juu ya dalili za wasiwasi wa tunakoelekea. Ulipotoka waraka wa Kiislam wa Shura ya Maimam, nikategemea kuwa nao una lengo hilo hilo kumbe sio!. Jana nilipata bahati ya kuusoma huu waraka wa Shura ya Maimam, nimesikitika. Toka utangulizi ni Kanisa tu, ndani ya waraka wenyewe ni Kanisa tu. Pamoja na tathmini nzuri ya kasoro zinazojitokeza wakati wa uchaguzi na kasoro za kuendesha siasa, kwao kiini cha tatizo ni Kanisa tu. Ukweli nimesikitika.
Kama kuna mambo ambayo nayapenda kuhusu Z'bar, kubwa ni utaifa wao. Z'bar pamoja na marumbano yote wanayoweza kuwa nayo kwenye siasa au jambo lolote. Unapokuja kwenye utaifa wote wanakuwa kitu kimoja, Kuitetea Z'bar kwao ndio #1, mambo mengine yanafuata.
Inashangaza kuona hata wakati huu ambapo inahitajika nguvu na jitihada za dhahiri kwa ajili ya kunusuru mustakabali wa taifa letu, baadhi yetu tunataka kuitumia fursa hiyo katika kuwashambulia wengine. Tunapambana wenyewe kwa wenyewe, hapa si tunawapa nafuu wale wasioutakia mema MUSTAKABALI WA NCHI YETU!
 
Back
Top Bottom