Pambanua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pambanua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Amosam, Aug 29, 2009.

 1. Amosam

  Amosam Senior Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani nimejaribu kulizuia lakini fupa limenishinda kukaa mdomoni kwani kuendelea kuwa nalo linaweza kunikwama hivyo nahitaji ufafanuzi juu ya methali maarufu ya kuswahili isemayo 'KAFIRI AKUFAAE SI MUISLAM HASIYEKUFAA'.Kutokana na maudhui ya methali hii yaonyesha wazi kuwa kuna makundi mawili tuu ya kiimani yaani 'Makafiri na Waislam'.Swali langu kama hivyo ni kweli je sisi 'raia wa roma'(roman catholics),angalicans,lutherans,full gospal fellowships,pentecostes,n.k tutakuwa upande gani kati ya hizo imani mbili?
  Naomba wachangie watu wenye upeo wa mambo tuu na si kila asomae kwani kusoma sana si kuelimika!
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dini ya kweli mbele ya Mwenyezi Mungu ISLAM. Hapa tukiangalia dini zote ispokuwa uislamu Tutagundua majina ya dini hizo ama ni jina la muanzilishi wa dini hiyo au ni jina la eneo ilipoanzishwa dini hiyo. Tofautina uislamu, neno Uislamu maana yake ni Amani au kujisalimisha kwa yule aliye kuumba, dini ya uislamu ni dini ya watu wote wenye kutaka amani, sio dini ya watu fulani au taifa fulani ndio mana jina lake halifungamani na taifa lolote au jam¨¬i yoyote. Tofauti na dini nyengine! Kama KRISTO hili ni jina la mtu, jewish hili ni jina la eneo "judeya" israil, BUDA Hili ni jina la mtu, na nyengine zote ziko hivyo ni dini zilizo buniwa na watu ndio maana wakazipa majina yao au maeneo yao. Lau UISLAMU ungulikuwa umebuniwa na MUHAMMAD bila shaka angeliupa jina lake au eneo analotoka. Bilashaka yoyote UISLAMU ni dini inayotoka kwa Mungu wa kweli, na haiwezekani kukawa na Mungu zaidi ya mmoja. Kwa hiyo kuna watu wanawaabudu binadamu wenzao. Njia ni mbili tu! "Kweli na uongo", uislamu na ukafiri. njia ni mbili hakuna ya tatu
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mtumikie Kafiri Upate Mradi Wako!
   
 4. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Huo ni usemi tu kama zilivyo semi nyingine nyingi, kama ' ALL ROADS LEAD TO ROME' je ni kweli hata barabara yetu ya Uru Kishumundu inaelekea Rome!
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Hii ni misemo tu ya watu waliochoka kufikiri inayosababisha watu wasifanye kazi waendelee kukaa vijiweni na kucheza karata na bao mchana kutwa''Pia wanasema Mungu si Athumani'',yaani Mungu si mwislamu maana mwislamu ataamulu kupigwa mawe na kukata vidole...........
   
 6. D

  Damas Member

  #6
  Aug 31, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Maoni yako tu. Dini zipo kama watu walivy0 wengi
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  maneno yako umeapangilia vizuri ila kuna wasemao kuwa uislam ulitokana na mganga wa kienyeji, hii imekaaje?
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Maana yake, dini inaweza kuwa longolongo tu. Kwamba unaweza kukuta kafiri akakufaa zaidi ya muislam mwenzako, sasa hapa nani bora?

  Kwamba, kama uislam unahubiri kutoa zaka, na muislam mwenzako mwenye uwezo hakusaidii, na kafiri ambaye hata haujui uislam ndiye aliyekupa zaka na kukusaidia, yupi afaa thawabu hapa? Huyu muislam asiyetekeleza misingi ya uislamu ingawa ana uwezo na kuijua au huyu "kafiri" ambaye haijui misingi ya uislam na pengine hana hata uwezo kama ule wa muislam?

  The moral of the story is, actions speak louder than words, kuna wengine watajitia uislam lakini matendo yao ya "kikafiri". Na kuna wengine makafiri kwa kutojua uislam rasmi, lakini matendo yao yanaendana na misingi ya uislam.

  Kwa hiyo dini inaweza kutumiwa kwa longolongo, inabidi uwe na macho yanayoweza kupeleleza deeper than labels za dini.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  BinMgen jibu post hiyo namba saba:D
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Uislamu ndiyo dini ya kweli? Siamini! Dini ya kweli utaitambua kwa matunda yake
   
 11. N

  Ngisi Member

  #11
  Sep 2, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HISTORIA YA DINI:
  dini imeanzia wapi?
  Tukiichukulia dini kwa maana ya aina Fulani ya mfumo wa maisha uliochaguliwa na kufuatawa na Jamii Fulani ya wanadamu. Tutagundua kwamba historia ya dini inaenda sambasamba na historia ya kuanza kuwepo kwa mwanadamu katika maisha ya ulimwengu huu. Hili ni dhahiri kwa sababu hakuna mwanadamu aliyepata kuishi, anayeishi au atakayeishi katika ulimwengu huu bila ya kufuata mfumo maalumu wa maisha. Iwe ni mfumo alio na khiyari nao mithili ya hizo mila/desturi, ujamaa, ubepari, ukomunisti na kadhalika. Au ule asio na khiyari nao mithili ya ule utaratibu mzima wa tangu kutungana kwa mimba, kuzaliwa mpaka kufa na yote yahitajikayo ili kuukamilisha utaratibu huu. Kwa mantiki hii basi huu unakuwa ni ushahidi wa kimazingira unaoonyesha kuwa dhana dini imeanza kuishi sambasamba na mwanzo wa kuwepo kwa mwanadamu katika ulimwengu huu.
  UISLAMU NI NINI?
  Uislamu ni mfumo kamili na sahihi wa maisha unaozienea nyanja zote za maisha ya mwanadamu katika hali, mahala na zama zote. Mfumo uliofumwa na Allah Mola Muumba ulimwengu na walimwengu kwa ajili ya waja wake na akawaleta kupitia mitume wake. Tangu Nabii Adamu mwanadamu wa kwanza mpaka Nabii Muhamad Mtume wa mwisho. Ili uwe ni muongozo na katiba ya kukiendesha kila kipengele cha maisha yao katika maisha haya ya mpito ya ulimwengu huu yenye dhima ya kuwaandaa na maisha ya milele ya Akhera.
  – KAULI MBIU YA UISLAMU.
  Uislamu kama dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha unalingana na kuhubiri juu ya kuwepo Mungu aliye Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo humo. Unawataka wanadamu wote waitakidi kuwa YEYE ni MUNGU MMOJA WA PEKEE ASIYE NA MSHIRIKA YEYE tu ndiye anayestahiki kukusudiwa na viumbe wake wote kwa kumuabudu, kumuomba na kumtegemea. YEYE hakuzaa wala hakuzaliwa wala YEYE hana anayefanana naye hata mmoja. Hii ndio kauli mbiu ya Uislamu, dini ya jamii ya wanadamu.
  Na akili isiyo lemavu haiwezi kupinga au kukanusha kuwepo kwa Mola Muumba wa ulimwengu na walimwengu kwani kanuni huru za kiakili zinasema kuwa (kila natija/matokeo yana sababu yake). Kwa kuichukua kanuni hii yenye mantiki kama mizani akili haitasita kukubali kuwa kila kiumbe kina Muumba. Kwa sababu kiumbe ni natija/matokeo yanayohitaji sababu na sababu hiyo ndiyo Muumba Mwenyewe. Maadam akili imetumika kumjua Muumba Mkuu, basi uadilifu wa kiakili unamsukuma mwanadamu kumuamini.
  Kauli mbiu ya Uislamu inawafikia walimwengu kupitia ujumbe wa Allah Mola Muumba unaofikishwa kwao kwa njia ya Mjumbe (Mtume).
  ALLAH (MOLA MUUMBA)
  [​IMG]

  UJUMBE (Vitabu)
  [​IMG]

  MJUMBE (Mtume)
  [​IMG]


  WALENGWA WA UJUMBE (Jamii ya wanadamu). Huu ndio utaratibu kamili wa mawasiliano baiana ya Allah Mola Muumba na mwanadamu kiumbe muumbwa chini ya mfumo Islamu.

  NIKITAKA KUWA MUISLAMU NIFANYE NINI?
  Uislamu unaamini kwamba kila mtoto anazaliwa hali ya kuwa tayari ni muislamu tokea tumboni mwa mama yake. Anabakia na Uislamu wake huo wa kuzaliwa mpaka anapofikia umri wa utu uzima (baleghe) hali ya kuwa na akili timamu. Katika umri huu ndipo anapoweza kuitumia akili na khiyari aliyopewa na Mola wake:
  "…………. BASI ANAYETAKA NA AAMINI (awe muislamu) NA ANAYETAKA NA AKUFURU (awe kafiri). HAKIKA TUMEWAANDALIA MADHALIMU (Makafiri) MOTO AMBAO KUTA ZAKE ZITAWAZUNGUKA …………" (18: 29).
  Akaukana na kuuvua Uislamu ndio umbile aliloumbiwa: "BASI UELEKEZE USO WAKO KATIKA DINI ILIYO SAWA SAWA NDILO UMBILE ALLAH ALILOWAUMBIA WATU (yaani dini hii ya kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binadamu). HAKUNA MABADILIKO KATIKA MAUMBILE YA VIUMBE VYA ALLAH. HIYO NDIYO DINI ILIYO YA HAKI, LAKINI WATU WENGI HAWAJUI" (30:30)
  Kwa kufuata mfumo mwingine wa maisha (dini) ulio nje ya Uislamu ambapo atakuwa amejitia khasarani mwenyewe: "NA ANAYETAKA DINI ISIYOKUWA YA KIISLAMU BASI HAITAKUBALIWA KWAKE NAYE AKHERA ATAKUWA KATIKA WENYE KHASARA (kubwa kabisa)" (3:85).
  Sasa muasi huyu anapotaka baada ya kuamua kwa khiyari yake kurudi katika umbile lake la asili (Uislamu) hahitaji kubatizwa. Kitu pekee anachotakwia kufanya ni kutamka hadharani shahada mbili na kuishi kwa mujibu wa shahada mbili hizo.
   
 12. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  1. Nimeshtushwa na neno "Dini ya Kweli" kwa sababu hatuna viashilia vya kuthibitisha ukweli wa dini yo yote hasa kutokana na zote kumtaja Mungu.

  2. Naambatanisha URL za kupambanua maana ya uislam na ukristo kutoka kwenye mtandao ambazo naziona zina mantiki
  http://www.barghouti.com/islam/meaning.html
  http://www.mb-soft.com/believe/txh/chrisdef.htm
  3. 'KAFIRI AKUFAAE SI MUISLAM ASIYEKUFAA' ni usemi binafsi naona una mantiki ukiondoa mnyumbulisho wa Kafiri na Muislamu maana inayojitokeza ni Akufaaye ni bora hata kama ana imani ya dini tofauti na yako.

  4. Usemi kwangu unasisitiza kuwa jamii bila kujali dini zao ina wajibu wa kutendeana mema wakati wote
   
 13. N

  Ngisi Member

  #13
  Sep 2, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee jua tafauti kati ya binaadamu a mnyama ni akili. Mnyama hatahukumiwa kwani hana akili. lkn binaadamu atahukumiwa akitumia vibaya akili yake. kwa hivyo unachotakiwa sasa ni kusoma kiundani Dini mbili hizi sio kwa mtazamo wa jujuu tu. soma viatabu vya diini hizi mbili na utapata jibu sahihi kiudhati kabisa
   
 14. j

  josephkibena Member

  #14
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni msemo kama mingine!,mbona wataalamu wanasema binadamu wa kwanza fuvu lake limepatikana Tanzania Kule Arusha je lilikuwa la mweusi au mweupe?.Lilikuwa la Mkristo au Mwiislamu????? inakaaje hiyo!.
   
Loading...