Pambano la Mwakinyo lilikuwa la kitaifa au kimataifa? Kwanini wahusika wote walikuwa watanzania?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,193
25,503
Siandiki hapa kusema kama Bondia wetu wa Tanzania Hassan Mwakinyo alishinda kwa haki au la kama mijadala iliyofuata pambano lake inavyorindima.Nilitazama na kusikia pambano lake pamoja na mapambano yote ya utangulizi.

Nikiri kuwa nilifurahia mapambano yote na kimsingi kuna juhudi kubwa kusogeza masumbwi kwenye ngazi nyingine. Kama taifa, tunapaswa kuwa na michezo lukuki, ngumi zikiwa mojawapo. Nasema tena kuwa sijadili wala kuandika kuhusu kushinda kwa Mwakinyo. Tulioona tumeona na tunaujua ukweli.

Swali langu ni moja tu. Tumezoea kwenye soka kuona kuwa zinapocheza nchi tofauti, waamuzi hutoka nchi nyingine kabisa. Hata waangalizi wa mchezo husika hutoka nchi nyingine kabisa. Hiyo huchagiza ukimataifa wa mchezo husika na kuonyesha kutendeka kwa haki.

Katika mpambano wa ndondi kati ya Mwakinyo na Mfilipino pale Uwanja wa Uhuru, Muamuzi wa pambano lile alikuwa mtanzania. Majaji watatu wa pambano lile walikuwa ni wa Tanzania akiwemo mwanamama Njau. Na mshindi akawa mtanzania!

Je, pambano lile lilikuwa la kitaifa au kimataifa? Je, sheria na taratibu za ndondi zinaruhusu muamuzi na majaji wote watoke nchi moja? Kuna mtu aliwahi kuniambia ukitaka kushinda mapambano wa ngumi ugenini inakupasa kumpiga mpinzani wako kwa KO tu. Naanza kuamini..
 
Ngoja nimuulize Matumla
Screenshot_20191202-221851.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom