"Pambana na hali yako" Nini chanzo na dhumuni la tungo hii?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
  1. Nani muanzilishi?
  2. Inakusudi gani katika jamii?
  3. kwani kabla ya uwepo wake, watu walikuwa wanapambana na hali za nani?
  4. Je, inauhusiano wowote na siasa?
Kila mtu akipambana na hali yake, hakuna uwezekano kukawa na ubinafsi uliopitiliza maana asili ya jamii ya mwanadamu ni kuishi kama familia kwa kutegemeana na kusaidiana.

Nawaza...
Wataalamu wa tungo na misemo msaada hapa....
 
Ni msemo wenye falsafa na hamaso kubwa.

1. Huwakumbusha watu kuwa wana jukumu na wajibu mkubwa sana katika maisha yao kuliko vile wanavyohangaika na ya wengine.

2. Ni uamsho dhidi ya tabia za udaku na umbeaumbea. (Mind your business)

3. Ni ukumbusho kwamba jinsi ulivyo na unavyotakiwa kuwa ni kutokana na jitihada zako.

[HASHTAG]#Pambana[/HASHTAG] na Hali yako#
 
Ni usemi mzuri angalau ukilinganisha na 'Watapata tabu sana' . Baada ya usemi huu wa watapata tabu sana kuchukuliwa na wanasisa,sasa umeshika sura ya kikatili.
 
Back
Top Bottom