afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,983
- 1,574
*TUNAPOMKUMBUKA YUDA ISKARIOTE, TUSIWASAHAU* WABUNGE WA CCM *WALIOKATAA HOJA YA KUTETEA MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA ISIJADILIWE BUNGENI TUNAPOELEKEA UCHAGUZI MKUU 2019-2020.*
Na Mwl, John Pambalu.
Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16).
*Usisahau usaliti* ni matokeo ya mtu aliye miongoni mwa watu wengine kufanya kinyume na kile walichokubaliana.
Makubaliano kati ya wananchi na wagombea wa mwaka 2015 ( wabunge wa sasa ) na vyama vyao vya siasa ni kuwa pindi watakapopewa hatamu basi watapigana kuhakikisha maslahi ya watumishi wa umma yanaimarishwa.
CCM waliahidi na CHADEMA waliahidi pia. Mwaka 2019 Mbunge *Ruth Mollel* anayetokana na CHADEMA bungeni akataka bunge lijadili juu ya maslahi ya watumishi wa umma wabunge wa CCM wakagoma.
Sio katika ukristo pekee unaokemea tatizo la kutokutimiza ahadi. Uislamu una kemea kwa nguvu sana tabia hii.
Kwa mujibu wa Hadith, "Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( *Alama za mnafiki ni tatu*: anapozungumza husema uongo, *anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi)* , na *anapoaminiwa hufanya khiyana* ))".
2019- 2020 ni mwaka wa kusahihisha makosa. Wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu wanaopiga day worker, watumishi wa umma mnaosota na law wages ile point mashuhuri Kwenye essay za *colonial exploitation,* wafanyabiashara walio taabani kufilisika ni *2019-2020 NI WAKATI WA KUREKEBISHA MAKOSA*
Tunapomtafakari Yuda Iskariote Kwenye juma kuu la Pasaka tuyatayatafakari na maiskariote mengine,
Wasalaam.
Mwl, John Pambalu.
Diwani Kata Butimba-Mwanza.
Makamu mkt Bavicha.
jpambalu@gmail.com