Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesitisha mahusiano yote na Marekani na Israel, yakiwemo yanayohusiana na usalama, baada ya kuupinga mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Abbas alikuwa mjini Cairo kuuhutubia mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ambayo iliwaunga mkono Wapalestina katika upinzani wao kwa mpango huo wa Trump.
Abbas alisema tayari wameifahamisha Israel kuhusu hatua hiyo ya kusitisha mahusiano. Maafisa wa Israel hawajazungumzia kauli hiyo ya Abbas.
Vikosi vya Israel na Mamlaka ya Palestina kwa muda mrefu vimekuwa vikishirikiana katika maeneo ya ulinzi ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel ambayo yako chini ya udhibiti wa Palestina.
Palestina pia ina makubaliano ya ushirikiano wa kijasusi na Shirika la Ujasusi la Marekani - CIA ambayo yaliendelea hata baada ya Wapalestina kuanza kususia juhudi za amani za utawala wa Trump katika mwaka wa 2017.