Pale tamko la CCM linapopoteza uhalali wake kwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pale tamko la CCM linapopoteza uhalali wake kwetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyimo, Sep 6, 2012.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Katika tamko la CCM juu ya kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kuna kifungu cha maneno kinachoeleza:

  Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.

  Imetolewa na;

  Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.  Maswali tunayojiuliza?
  1. Inamaana wameshindwa kubaini wahusika wa tukio hili zima wakati wao ndiyo wenye SERIKALI ama wanajaribu kupotezea?
  2. Wao kama chama cha siasa, lini wamefata utamaduni wa UTAWALA WA SHERIA ikiwa siku hiyo wao walifanya kikao cha hadhara huku CDM wakitaka kufanya kikao cha ndani ambacho waliruhusiwa?
  3. Kwanini wasiwalaani POLISI ama wao ndiyo waliwatuma wafanye hivyo?
  4. Kwanini wanatoa majibu ambayo serikali yao inadai imeunda TUME ya kuchunguza tukio hili?

  View attachment 64042

  walivyomwuawangosijpg-2204219_p9.jpg

  Bububu_2.jpg

  View attachment 64045

   
 2. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyimbo ni zilezile za kumfumbia jirani huku mmejifunga vibwebwe, ziko wapi zile za mashujaa waliokua wakituamsha na kutukimbiza katikati ya umande ili tuwe mashujaa? Tanzania mbona wajiua na kupiga miruzi ya kujigamba kwa kumuua mbu kwa meli ya kivita tena ya 1979?
   
 3. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Sheria zote wamezipindisha ili zifuate matakwa yao hivo ni lazima zinyooshwe ili vyama vyote na asasi mbalimbali pamoja na majeshi yetu yatumike kwa sheria zenye usawa.
   
 4. j

  jossy chuwa Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu nakushukuru kwa kunifunua akili yangu mapema na kuichukia ccm! Tena nakushukuru kwa namna unavyoiua mdo mdo
   
 5. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna haki za msingi anazozaliwa nazo binadamu, wakati mwingi tabaka tawala wanapotumia madaraka vibaya na kuwanyima hata zile haki za msingi huleta uadui mbaya baina ya serikali na watu wake. Ccm yamefikia mahali wanacreate uadui na Watanzani. I real hate CCM and it's government.
   
 6. M

  Masikrodinga JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyo NAPE ndo hamna ki2 kabisa, kila siku anakurupuka tu kutoa matamko kama vile hana washauri au washauri wenyewe ndo afadhali ya yeye?
   
 7. m

  mamajack JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  3. Kwanini wasiwalaani POLISI ama wao ndiyo waliwatuma wafanye hivyo?
  NDIYO;HAWAWEZI KULAANI POLIS KWA SABABU WALIWATUMA WAKAUE.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Nadhani alikuwa anawalenga BASHE na KIGWANGALA
   
 9. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  serikali legevu siku zote huamua mambo kidhaifu, bado kidogo wataanza kukimbia vivuli vyao....R.I.P DAUDI MWANGOSI
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
   
 11. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tamko hili limejaa upotoshaji mkubwa. Bado halijagusa kiini cha tatizo hasa lililojitokeza huko Iringa. Lakini sijashangaa sana kwa kuwa aliyelitoa namjua. Huwezi kulizungumzia suala la vurugu za Iringa zilizosababisha kifo cha Mwangozi (RIP) bila kuwalaani polisi wale waliomuua. Ushahidi uko wazi kabisa juu ya kuhusika kwa polisi, hivyo longo longo za kuhusu utawala wa sheria hapa ni ubatili mtupu.
   
 12. yakowazi

  yakowazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 1,171
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  je serikali yangu mnasubiri AFE nani ndio mjuekuwa police wetu wanaua RAI VYAMA vyote vilivyoko TANZANIA ni vya WATANZANIA hivyo waote waliofia mikononi mwa POLISI ni WATANZANIA je serikali YAYETU KWA MTINDO HUU ITAKUWA INAPENDWA
   
 13. m

  mwimbule JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 485
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hawa vilaza we acha tu. Wamejisahau sana na pengine wanaota hii ni nchi yao peke yao na eti wana uhuru wa kufanya chochote.
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,534
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumeshasema ccm "HATUITAKI."
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nape anasema utwala wa sheria upi? maana kila kitu kinaonekana kweupe kabisa waliovunja haki ni polisi na ccm yake sasa anaropoka nini hapo
   
Loading...