Pale Rais anapodanganywa hadharani na Maofisa wa Bandari mamlaka zimekaa kimya...

mwanaone

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
637
760
Katika ziara yake ya juzi mh RAIS aliambiwa kuwa kuna meli za MIZIGO 30 ule ni uwongo dhahiri. Na sijui kwanini watu wamdanganye RAIS wetu hivi hivi Kwani aliwaambia asiposikia kuna meli Za kutosha atawatumbua?

Kenya wenzetu wana meli 41 ambazo zipo bandarini Na 18 zipo njiani Sisi tuna 16 na 3 Ndio zipo njiani lakini tunadanganywa kuwa zipo 30.

Ushahidi kuwa mh RAIS amedanganywa Huo hapo ktk link.

Mh hatukupangii lakini tunakuomba hawa jamaa ( maofisa wa mandari) usiishie kuwatumbua tu uwapeleke mahakamani Ili wafungwe kabisa . Haiwezekani wakudanganye mbele ya vyombo vya habari.kuwa kuna meli 30 haliyakuwa ukweli kuna meli 16 Na 3 Ndio zipo njiani.kwahiyo jumla zote itakuwa 19 Na sio 30 Kama walivyosema. Na hizo 19 kuna meli mbovu hapo zilizokuja siku nyingi sana.

mh RAIS Tena KATIKA hizo MELI 19 zipo mpaka BOTI Za Bakharesa. Na wanajua fika wewe uliwauliza meli Za MIZIGO lakini wakajifanya wajanja wakajumlisha meli Za MIZIGO Na BOTI Za Bakharesa. Mkuu usiwaache hawa .mkuu nimeambatanisha na ushahidi wangu najua baadae ukiingia humu utauona ikiwa MODs itakuwa hawajaufuta

Mkuu Jana nimewasiliana Na watu marine traffic Na Kwa kweli wamenipa ushirikiano wa kutosha kuthibitisha Madai yangu kuwa maofisa wa bandari wamekudanganya kuhusu meli Za Mizigo.

Na Nasubiri Yule ofisi wa bandari aje kukana Hizi habari Ili nitoe data zote nilizopata kutoka marine traffic mpaka number Za meli Na idadi yake kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita na zinazotarajia kuja Tanzania ndani ya mwezi mmoja. Nashukuru wazungu kwa ushirikiano.na uzuri ushahidi wa Hili suala nimetumiwa kwa email.


Au muheshimiwa kama vile ambavyo haupagiwi wa kuteua Na wewe ndiye mpangaji Na unaeamua Nani awe wapi Na Nani aseme nini Na Nani adanganye Na Nani asidanganye.

Ukiona mpaka kesho wapo kimya Bila mtu kuchukuliwa hatua hii movie itakuwa sawa Na movie ya bashite kuvamia clouds.

http://www.marinetraffic.com/en/ais/details/ports/2730/Tanzania_port:DAR ES SALAAM
 

Attachments

  • Mh RAIS Akidanganywa Na Wafanyakazi Wa Bandarini.m4a
    553.3 KB · Views: 53
  • Mh RAIS Akidanganywa Na Wafanyakazi Wa Bandarini.m4a
    553.3 KB · Views: 42
  • IMG_9732.jpg
    IMG_9732.jpg
    86.9 KB · Views: 71
  • IMG_9733.jpg
    IMG_9733.jpg
    87.3 KB · Views: 65
  • IMG_9734.jpg
    IMG_9734.jpg
    74.2 KB · Views: 65
  • IMG_9736.jpg
    IMG_9736.jpg
    54.8 KB · Views: 51
  • IMG_9735.jpg
    IMG_9735.jpg
    56.5 KB · Views: 59
  • IMG_9737.jpg
    IMG_9737.jpg
    49.3 KB · Views: 57
  • IMG_9738.jpg
    IMG_9738.jpg
    40.7 KB · Views: 66
Tutadhani anadanganywa kumbe anajidanganyisha ambapo, kabla hajaenda usikute anapiga simu kwanza na mazungumzo kuwa hivi:

SIZONJE: Haroo, Sizonje hapa nakuja TPA lakini jifanye hujui manake nataka ionekane nakuja kwa kushitukiza; sawa?

TPA: Nimekuelewa Mheshi.....

SIZONJE:...Wewe, nisikirize vizuri! Sijakuuliza umeerewa; nimekuuliza, sawa?!

TPA: Sa..sa...sawa Mheshimiwa!

SIZONJE: Kuna meri ngapi bandarini?

TPA: Zipo 12 Mheshimiwa!

SIZONJE: Sasa sikiriza, nikija hapo na watu wa kufotoa picha sema kuna meri 46; umenierewa?!

TPA: Sawa Mheshi...

SIZONJE: WEWEEEE... nimekuuliza umenierewa?

TPA: Nimekuelewa Mheshimiwa!!!

SIZONJE: Sasa ore wako!!! Kumbuka mimi sijaribiwi...
 
Mwaka mmoja uliopita, "Nimezuia Bunge live kwa sababu gharama zake za bilioni 4 kwa mwaka ni kubwa mno."

Wiki moja iliyopita akiongea na Wabunge wa MACCM Dodoma, "Nimezuia Bunge live kwa sababu wengi mlikuwa mnasinzia kwenye vikao vya Bunge."

Mimi naona sasa tusishangae huyo bwana mzee kudanganya. Kusema uongo ni jadi yake. Inabidi tumzoee mzee wa uongo.
 
Tutadhani anadanganywa kumbe kabla hajaenda huwa anapiga simu na mazungumzo kuwa hivi:

SIZONJE: Haroo, Sizonje hapa nakuja TPA lakini jifanye hujui manake nataka ionekane nakuja kwa kushitukiza; sawa?
TPA: Sawa Mheshimiwa!
SIZONJE: Kuna meri ngapi hapo hadi hivi sasa?
TPA: Zipo 12 Mheshimiwa!
SIZONJE: Okay, nikija hapo mbele ya waandishi wa habari sema kuna meri 46; umenierewa?!
TPA: Nimekuelewa Mheshimiwa!!!
Kweli kabisa itakuwa inapangwa hivi mapema.
 
Hataki ukweli akiambiwa ukweli unatumbuliwa. Na Ndio maana akasema Hakuna mtu wa kumpangia kwa lugha nyengine ni kuwa hazikilizi ushauri wa wataalamu.
Kama tunaambiwa issue ya kukamata magari ni usanii mtupu. What if ukute pia issue ya kutaja idadi ya meli nako usanii ulikuwa unaendelea kwa yule mzungumzaji kuandalia cha kusema before?
 
Back
Top Bottom