Pale panapotokea wizi mkubwa na mnahisi mmoja wenu kahusika na hamtaki habari ivuje, mtatumia mbinu ipi kumbaini mhalifu huyu?

Niliwahi kusaini kupokea box lenye laptops (Delivery) siku tunafungua kuna box moja halina laptop. Nililipa 800,000/=kama miaka 9 iliyopita. Tokea siku hito, nikipokea mzigo wowote nafungua box moja moja nahakikisha hadi serial number.
Hili halipo huku, viilibiwa ndani baada kuidhinishwa
 
Kwenye store hakuna cctv kamera kama ipo nenda kacheck na kama ni vitu vya msaada si lazima kutakuwa na full details kwamba vimeingia vingapi deal na store manager hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kuhurumiana na kuleana ndio kumejenga hii culture ya wizi wizi na udokozi..... Wizi ni wizi tuu hakuna mambo ya huruma ili iwe fundisho katika taasisi
 
Niliwahi kusaini kupokea box lenye laptops (Delivery) siku tunafungua kuna box moja halina laptop. Nililipa 800,000/=kama miaka 9 iliyopita. Tokea siku hito, nikipokea mzigo wowote nafungua box moja moja nahakikisha hadi serial number.
Ni kweli haya huwa yanatokea bila kutegemea,mwisho wa siku mtu anakuja kuwajibishwa kwa kitu ambacho hajafanya;ndio maana maamuzi mengine huwa yanahitaji busara.
 
Mizigo ilikaguliwa baada ya kufika na siku chache tena watoa msaada walikuja kuikagua na ilikuwepo yote. Baada ya kuondoka sasa...........
Kama ripoti ya ukaguzi inaonyesha vitu vyote vilikuwepo,shughulika na anayehusika kuvitunza kama vilikuwa bado stoo au angalia kwenye vielelezo ni nani alikabiziwa na uanzie hapo kujua upotevu pamoja na muhusika
 
Nakuelewa lakini hao waliopokea walihakikisha vitu vyote vipo kwenye mabox tokea wanavipokea?
Kama hiyo timu ya ukaguzi haikuwa makini kujiridhisha kama vitu vyote viko sawa na wakasaini bila kujiridhisha,hapo mtu wa stoo lazima aumie.Cha kujifunza hapa,katika mifumo usimuamini mtu,jiamini mwenyewe kwa kujiridhisha kila kitu.
 
Millions of Tsh
Inategemea na muda kama ushapita mwingi aliyeiba kashaviuza.

-Mnayemshukia/hisia amejihisi anahisiwa? Kama kashajihisi ameshaweka shield ya kutosha.

Kwanini anahisiwa yeye na sio mwingine?[kama hoja inamashiko muiteni private mumpe muda avirudishe na mtishieni asivijishe taarifa.

Kama hoja sio mzito msijaribu huenda sio yeye itaharibu kila kitu.

Mwisho nilijua vitu ni bei ndogo mvinunie kutuliza hali ila huku mkiendelea kuchunguza aliyeviiba.
 
Tehtehteh....

Kuna masuala ya kutumia busara na mengine ya kufuata sheria inavyosema.

Hili linahitaji busara ya hali ya juu.
Sasa kwanini wasiajiri investigator kwa hyo case mi nimeona watu walifuatilia case including tracing mawasiliano wakamkamata mwizi. Waajiri private investigator wakikaa kimya itakuja leta mazoea. Ila wa Tanzania kwa wizi hatujambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom