Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Tulikuwa na nyumba yetu ya urithi tuliyoachiwa na babu zetu. Tuliishi vizuri kwa muda mrefu mpaka pale tulipoanza kutofautiana umiliki wake.
Baada ya kutofautiana tukaamua kukaa kikao. Kikao kiliamua kuwa kila mwanaukoo aliyelelewa ndani ya ukoo wetu atakuwa mkuu wa ukoo kwa muda maalum.
Maisha yaliendelea vizuri mpaka pale mdogo wetu alipokuwa anamalizia nafasi yake ya ukuu wa ukoo. Tuligawanyika baada ya baadhi ya ndugu zetu kutaka kuharibu utaratibu wetu wa kumsimika mkuu wa ukoo.
Tuliiona hatari iliyokuwa inatunyemelea baada ya nyumba yetu kuonekana kurithiwa na watoto wa ukoo mwingine ambao ulikuwa na uhusiano wa karibu na ukoo wetu kutokana na mwingiliano wa wazee wetu enzi zao.
Tukaamua kumpa ukuu wa ukoo ndugu yetu mmoja ambae alionekana hana upande wowote ingawaje tulifahamu kuwa huenda asitufikishe salama. Tuliona ni heri ya huyu kuliko nyumba yetu kurithiwa na mtoto wa ukoo mwingine.
Baada ya kumkabidhi nyumba, bila hiana, kuonesha kuwa hana upande wowote, akaamua kuitia nyumba kufuli na kutupa ufunguo ili isije kuharibiwa.
Baada ya nyumba kukaa miaka minne bila kutumika kama ilivyozoeleka, sasa imeanza kuchakaa mpaka kufuli lake limeanza kuharibika.
Wale watoto wa ukoo mwingine wanatucheka kwamba ni bora tungewaachia wao wakairithi, wangekuja na mawazo mbadala ya kuiboresha.
Sisi tuliomwachia ukuu wa ukoo ndugu yetu, tumeamua kukaa kikao ili tuone jinsi ya kuirudisha nyumba yetu katika hali yake ya kawaida kama zamani ikiwezekana zaidi ya pale. Tumeamua tumuache kwanza angalau ndani ya mwaka mmoja tuone kama ataikarabati na asipofanya hivyo tunaenda kubomoa kufuli na kumkabidhi kijana mwingine mwenye maadili na aliyelelewa vizuri na ukoo.
Siku zote ukijikwaa usiangalie pale ulipoangukia, angalia pale ulipojikwaa ili kesho usije ukajikwaa tena.