Pale miujiza pekee inaposubiriwa shahidi muhimu apone ili muuaji apatikane...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pale miujiza pekee inaposubiriwa shahidi muhimu apone ili muuaji apatikane...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 14, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Josie alinusurika.................
  [​IMG]
  Josie alivyo sasa...
  [​IMG]
  Josie akiwa na baba yake
  [​IMG]
  Familia ikiwa pamoja, Lin, Megan, Russell na Josie....
  Megan aliuawa na mama yao Lin naye aliuawa
  [​IMG]
  Josie akiwa na baba yake
  [​IMG]
  Josie akiwa na baba yake

  Ilikuwa ni majira ya saa kumi za jioni mnamo July 1996, katika mji wa Kent kusini mwa Uingereza mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Lin Russell alikuwa ametoka shuleni kuwachukua mabinti zake wawili, Megan aliyekuwa na umri wa miaka 6, na Josie aliyekuwa na miaka 9. Wakiwa wameongozana na mbwa wao aitwae Lucy, walitembea kwa mguu kutoka katika shule hiyo ya Goodneston kuelekea nyumbani kwao. Walikuwa wanaishi katika eneo la Nonington, umbali wa kama kilomita moja kutoka hapo shuleni. Lakini kwa bahati mbaya hawakutokea nyumbani.

  Majira ya saa 1:15 usiku Dk. Shaun Russell 47, mwalimu wa baioloji katika chuo kikuu cha Kent, alirudi nyumbani lakini jambo la kushangaza, hakuikuta familia yake hapo nyumbani. Hali hiyo haikumstua sana, hivyo aliamua kujipumzisha sebuleni kwake akijua kwamba muda wowote mkewe na watoto watarejea kutoka katika matembezi ya jioni. Baada ya saa moja Dk. Russell alishangazwa na familia yake kutotokea na hivyo kuanza kujenga wasiwasi.

  Aliwapigia marafiki zao kadhaa, lakini hakuna hata mmoja aliyedai kuiona familia yake. Ilibidi awajulishe majirani zake na haraka sana kwa kushirikiana na majirani hao walianza kuitafuta familia yake katika maeneo ya hapo karibu na nyumbani kwao wakianzia shuleni, lakini hawakuweza kuwapata. Hatimaye ilipofika majira ya saa 4:45, Dk. Russell aliamua kuwajulisha Polisi kwamba familia yake imetoweka katika mazingira ya kutatanisha. Majira ya saa 7:45 usiku, Polisi hao walifanikiwa kupata miili ya familia ya Dk. Russell ikiwa imelala njiani umbali wa nusu kilomita kutoka hapo nyumbani kwake. Lin na Megan Russell walikuwa wamekufa, akiwemo mbwa wao aitwae Lucy, Josia alikuwa bado hajakufa, lakini alikuwa amepoteza fahamu. Wote walikuwa wamepigwa na nyundo kichwani.

  Mtoto Josie Russell alikimbizwa hospitalini ambapo alifanyiwa upasuaji wa dharura. Ilibidi sehemu ya ubongo wake iondolewe ili kuokoa maisha yake. Hata hivyo hali yake iliendelea kuwa mbaya na kulikuwa na matumaini finyu sana ya mtoto Josie kupona. Dr. Russell alifika pale hospitalini akiwa amechanganyikiwa. Kwa kuwa hali ya mwanaye ilionekana kuwa mbaya na isiyo na chembe ya matumaini ya kupona, madaktari bingwa waliokuwa wakimtibu binti yake walimuomba awaruhusu wazime mashine iliyokuwa ikisaidia mapigo ya moyo na kuridhia binti yake kufa.

  Ditective Chief inspector David Stevens aliyekuwepo pale hospitalini muda wote akifuatilia hali ya binti huyo pia alikuwa na matumaini finyu ya binti huyo kupona na kurudi katika hali yake a kawaida.

  "Itakuwa ni vigumu Josie kukumbuka jambo lolote kuhusu tukio zima la kushambuliwa na muuaji hata kama akipona." Alisema askari huyo wa upelelezi akiongea na waandishi wa habari. "Mpaka sasa inabidi tutafute mashahidi wengine watakaoweza kutusaidia kumpata muuaji. Ni lazima kuna mtu anajua ni nani alihusika na mauaji haya ya kutisha, kwani tusipofanya juhudi za kumkamata mapema anaweza kushambulia tena mahali pengine na kuuwa… hivyo ni lazima ufanyike msako mkali ili mtuhumiwa atiwe mbaroni kabla ya kutekeleza mauaji mengine. Nisingependa wananchi waendelee kuwa na hofu juu ya maisha yao." Aliendelea kusema.
  "Hii ni jamii adilifu iliyokuwa ikiishi kwa amani kabla ya mauaji haya, ni pale muuaji atakapopatikana ingawa sijui ni kwa namna gani, ndipo nitakaposema watu sasa wako salama. Kutokana na tukio hili, kuanzia sasa watoto wasiruhusiwe kuwa nje peke yao na si vyema wanawake kutoka nje ya nyumba zao wakiwa peke yao. Ukweli ni kwamba hili ni tukio la kutisha ambalo sijawahi kulishuhudia katika maisha yangu. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kufanya hivyo."
  [​IMG]
  Mchoro wa picha ya muuaji

  Ili kumpata muuaji, ilibidi Detective Chief Inspector Stevens aunde timu ya wapelelezi 30 ambayo aliipa kazi maalum ya kufanya upelelezi makini juu ya mauaji hayo. Kwa kuanzia askari hao wa upelelezi walifankiwa kupata silaha iliyotumika katika mauaji hayo ambayo ilikuwa ni nyundo.

  Askari hao walianza upelelezi wao kwa kuhoji nyumba kwa nyumba, walitengeneza mchoro unaionyesha familia hiyo ikitembea kutoka shuleni kurudi nyumbani, pia walichora picha ya mtu aliyetajwa na mashahidi mbalimbali waliomuona katika eneo hilo muda mfupi kabla ya mauaji kutokana na muonekano wake kuwa ni wa kutiliwa mashaka. Michoro yote hiyo ilionyeshwa katika televisheni ikiwa ni juhudi za askari hao wa upelelezi kumpata muuaji.

  Mpaka kufikia hapo, walichokuwa wakihitaji askari hao wa upelelezi ni maelezo kutoka kwa mtu aliyeshuhudia tukio hilo la mauaji. Na shahidi muhimu na ambaye angeweza kuwategulia kitendawili hicho alikuwa bado amelazwa hospitalini hali yake ikiwa mbaya sana. Binti huyo alionekana dhahiri kupigania maisha yake, kwani baada ya wiki tatu, aliwashangaza madakatari ambao walishakata tamaa, kutokana na afya yake kuonekana kuimarika kwa kasi ya ajabu. Haraka sana alimudu kunyanyuka kitandani na kuanza kutembea pale wodini. Alimudu pia kuongea, ingawa matamshi yake yalikuwa kama ya mtoto wa miaka miwili anayejifunza kuongea. Hata hivyo baba yake hakupoteza matumaini. "Ingawa ni vigumu kwangu kujua itachukua muda gani Josie kumudu kuongea na kuwasiliana kama zamani, lakini anaonyesha dalili zote za kukusanya kumbukumbu ambapo siku moja ataweza kuwasaidia askari wa upelelezi kumkamata muaji aliyewaua mama yake na dada yake." Alisema Dr. Russell.

  Detective Chief Inspector Stevens akizungumzia kuimarika kwa afya ya Mtoto Josie alisema kwamba, amefurahishwa na kuimarika kwa afya ya binti huyo, lakini alieleza wasiwasi wake kuhusiana na uwezekano mdogo wa binti huyo kukumbuka tukio zima. "Kwa akili ya kawaida huwezi kutegemea binti aliyejeruhiwa kwa kiwango kile kupona na kumudu kukumbuka tukio zima kwa usahihi. Tukio hilo litamtesa kwa maisha yake yote."

  Mara baada ya Josie kuruhusiwa, baba yake Dr. Shaun Russell alihama kutoka katika eneo hilo na kuhamia Kaskazini mwa Wales katika eneo ambalo halikutajwa kwa usalama wake na wa mtoto Josie. Kwa muda wa mwaka mmoja Josie alikuwa anahudhuria katika hospitali kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuongea (Speech Therapy) na taratibu alianza kumudu kuongea na pia kurudisha kumbukumbu. Pamoja na kuwahoji watu zaidi ya 9,000, na kuchukua maelezo kutoka kwa watu mbalimbali wapatao 1,000 nchini humo na nje ya nchi hiyo, kama Ufaransa, Ubelgiji na Marekani, lakini Detective Chief Inspector na timu yake walionekana kukwama kumpata muuaji.

  Hata hivyo Ditective Stevens alionekana kuwa mtulivu na aliendelea kuvuta subira huku akifuatilia maendeleo ya binti Josie. Hali ya mtoto Josie iliendelea kuimarika na Detective Stevens aliona kwamba huo ni wakati muafaka kwa Josie kusaidia kumpata muuaji wa mama yake na dada yake. Josie alikubali kuongea na askari huyo wa upelelezi na mnamo July 9, 1997 ikiwa umeshapita mwaka mmoja tangu tukio hilo litokee, Polisi walitangaza rasmi kwamba Josie amekubali kutoa maelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo.

  Katika mkutano wake na vyombo vya habari Ditective Chief Inspector Stevens alisema kwamba, maeleza waliyoyapata kutoka kwa Josie yatasaidia sana kumpata muuaji pasi na shaka yoyote. Katika kipindi chote cha mahojiani yaliyofanywa na Polisi maalum wa upelelezi waliofunzwa kufanya mahojiano na watu wenye hali kama ya Josie waliotajwa kwa majina ya Pauline Smith na Ed Tingley. Josie alionekana kuwa na kumbukumbu sahihi juu ya tukio hilo.

  Detective Stevens alitoa maelezo hayo kutoka kwa Josie kama ifuatavyo:

  "Josie na familia yake walikuwa wanarudi nyumbani kutoka shuleni, ambapo waliona gari likija nyuma yao na kuwapita. Waliendelea kutembea, lakini walipokuwa wanakaribia kukata kona, waliliona lile gari likiwa limesimama mbele yao. Josie alikumbuka rangi ya gari kuwa lilikuwa ni jekundu. Wakati walipolikaribia hilo gari, walimuona mtu aliyekuwa kwenye gari hilo akichukua nyundo kutoka kwenye kishubaka cha kuhifadhia vifurushi ndani ya gari. Aliwafuata na kumuamuru mama yao: "Nipe pesa haraka" mama yao alimjibu: "Nitakwenda nyumbani kukuchukulia, kwani siishi mbali kutoka hapa." Mtu huyo alianza kuwashambulia, na mama yao alianza kupika kelele: "Tafadhali usitudhuru….." Mama yake alimamuru Jose akimbie na Josie alikimbilia katika nyumba moja ambayo kwa bahati mbaya ilikuwa haikaliwi na mtu kwa wakati ule. Yule muuaji alimkimbiza na kumkamata kisha kumrudisha pale alipo mama yake na dada yake. Yule muuaji aliwafunga kwa kipande cha kamba alichokipasua kutoka kwenye taulo. Muuaji huyo alidiriki hata kumuuliza Josie kama ile kamba aliyowafunga imekaza sawasawa. Alianza kupekua mkoba waliobebea vyakula vyao vya shule ambapo kiukweli haukuwa na kitu chochote. Muuaji yule alianza kumshambulia mama yao. Yule muuaji hakuongea tena bali alianza kuwashambulia lakini hakumbuki kuona dada yake akishambuliwa wala mbwa wao, anachokumbuka ni kuona mama yao akishambuliwa kikatili na muuaji huyo. Alimuelezea muuaji kuwa anafanana na picha iliyowahi kuchorwa na Polisi ambayo ilichorwa baada ya mauaji hayo kwa msaada wa mashahidi waliojitokeza na kudai kumuona mtu katika eneo hilo yalipotokea mauaji mwenye muonekanao wa kutia shaka muda mfupi kabla ya mauaji hayo." Alisema Detective Stevens.

  "Alichotueleza Josie, kinatisha na kusikitisha, na maelezo yake ni msaada mkubwa sana kwetu utakaotuwezesha kumpata muuaji.." Alimalizia kusema Detective Stevens.

  Jioni hiyo kituo cha televisheni cha BBC, katika kipindi chake cha matukio ya uhalifu maarufu kama Crimewatch walirudia matangazo yanayoonyesha mchoro wa Lin, Josie na Megan wakitembea kurudi nyumbani, na picha ya mchoro ya mtuhumiwa wa mauaji hayo. Kuonyeshwa kwa tukio hilo katika kipindi hicho kuliamsha hisia za watu wengi na haraka sana simu zilianza kumiminika katika kituo hicho cha televisheni. Mpaka usiku wa manane kulipokelewa simu zaidi ya 1,000 za watu waliodai kuwa na taarifa zitakazowasaidia Polisi kumkamata muuaji.
  [​IMG]
  Wiki moja baada ya kipindi kile kurushwa, Polisi walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Michael Stone aliyekuwa na umri wa miaka 37 wakati huo. Walimkamata katika nyumba aliyokuwa akiishi iliyoko katika eneo la Gilligham Kent. Michael Stone alielezewa kama mtu asiye na mke na mpweke asiye hata na rafiki. Alihojiwa na askari wa upelelezi kwa muda wa masaa 96, kabla ya kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa makosa ya mauaji ya watu wawili na jaribio la kutaka kuua.
  [​IMG]
  Siku mbili baadae Michael Stone alitakiwa kusimama katika gwaride la utambulisho lilioitishwa na askari wa upelelezi na wale watu wote waliotoa maelezo kwa askari wa upelelzi kwamba siku hiyo ya mauaji walimuona mtu mwenye sura ya kutiliwa mashaka katika eneo hilo, waliitwa ili kumtambua muuaji huyo. Ingawa shahidi muhimu katika kesi hiyo alikuwa ni Josie, lakini askari wa upelelezi walisita kumuita kwa sababu hawakuwa na uhakika kama angeweza kukabiliana uso kwa uso na muuaji huyo.

  Hata hivyo Detective Chief Inspector Stevens aliandaa gwaride la utambulisho katika kituo cha polisi cha Rainham ambacho kina eneo maalum kwa kazi hiyo ya utambulisho. Josie aliweza kumuona muuaji wa mama yake na dada yake kwa njia ya video. Baada ya gwaride hilo, la utambulisho Detective Stevens alikataa kusema iwapo Josie au mashahidi walioletwa waliweza kumtambua muuaji Michael Stone, lakini alizungumzia jinsi upelelezi ulivyofanyika kwa ujumla. Akiongea na waandishi wa habari alionyesha kuwa na imani zaidi na ushahidi wa vipimo vya DNA ambayo vimeonekana kuleta mafanikio makubwa katika miaka ya karibuni.

  Wataalamu walichukua mabaki ya nywele yaliyokutwa kwenye vipande vya taulo iliyotumika kuwafunga wahanga hao kabla ya kuuwawa ambavyo vilikutwa katika eneo la tukio. "Tunaamini yeye ndiye muhusika wa tukio hilo." Alisema Ditective Stevens. "Tunazo sampuli za nywele tulizozitoa katika vipande hivyo vya taulo ambapo tutachukua vipimo kutoka kwa mtuhumiwa, kwani zaidi ya watuhumiwa 100 wameshatoa sampuli zao za DNA kwa ajili ya vipimo na walishaondolewa tuhumua hizo. Sasa ni muda muafaka kuchukua sampuli za Michael Stone kwa vipimo hivyo vya DNA, na majibu yatapatikana baada ya wiki tatu.

  Kuanzia siku hiyo Ditective Stevens alikuwa kama anacheza karata zake huku akiwa amezificha mkabala na kifua chake. Alikataa kuzungumzia maendeleo ya vipimo hivyo na jinsi upelelezi unavyoendelea. Lakini ilitosha tu kuamini kwamba vipimo havikumtoa Michael Stone katika tuhuma hizo, kwani aliendelea kusota rumande huku akisubiri kufikishwa mahakamani. Baada ya Michael Stone kukamatwa, Josie na baba yake walirudi katika nyumba yao iliyoko Wales na kuanza maisha mapya. Josie alimudu kurudi shuleni na kuendelea na masomo, na taratibu maisha yake na baba yake yalainza kurudi na kuwa ya kawaida.

  Mnamo April, 1998, Mamlaka inayohusika na kulipa fidia kwa watu waliaoathiriwa na uhalifu (Criminal Injuries Compensation Authority) ilimtunukia Josie kiasi cha dola 30,000 kwa kumpoteza mama yake, dola 8,000 kwa majonzi aliyoyapata na dola 3,500 kwa mwaka kwa kukosa malezi ya mzazi wake. Hata hivyo kulikuwa na kelele nyingi kutoka kwa wananchi, bunge la nchi hiyo pamoja na vyombo vya habari kuhusiana na fidia hiyo. Waziri mmoja wa wakati huo Jack Straw alikiri kuhusu udhaifu huo wa sheria, na alisikitika kwamba hana mamlaka ya kuingilia juu ya maamuzi hayo. Lakini alimtaka baba wa mtoto Josie, Dr. Shaun Russell kukata rufaa kwa niaba ya binti yake.

  Wakili wa Josie, Sarah Harman alisema watakata rufaa.

  [​IMG]
  Damien Daley

  Mnamo mwaka 1998 Michael Stone alikutwa na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa na mfungwa mwenzie aliyekuwa naye gerezani aitwae Damien Daley wakati akiwa anasubiri kufikishwa mahakani ambapo mfungwa huyo alidai kwamba Michael Stone aliwahi kukiri mbale yake kwamba ni yeye aliyehusika ka mauaji hayo. Alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

  Baada ya majaribio kadhaa ya kukata rufaa, mnamo Decemba 21, 2006 mahakama ya rufaa ilitoa uamuzi kwamba Michael Stone atumikie angalau kifungo cha miaka 25 jela ndipo anaweza kufikiriwa kutolewa kwa msamaha wa Parole. Hiyo inaonyesha kwamba ibabidi akae gerezani hadi mwaka 2023 ambapo kama atatolewa, basi atakuwa amefikisha umri wa miaka 63.

  Josie anafanya nini kwa sasa...?


  Josie alifanikiwa kumaliza elimu ya juu katika chuo cha Coleg Menai kilichopo Bangor na kufanikiwa kupata shahada yake ya graphic design hapo mnamo mwaka 2009. Alianzisha mradi wake mwenyewe wa kutengeneza na kuuza kadi za salaam alizokuwa akizitengeneza kiusanii kabla na kupanua wigo wa biashara zake kwa kuanzisha mradi mwingine wa sanaa ya uchoraji ambapo kazi zake zimefikia thamani ya paundi 500 kwa kila kazi moja.
  [​IMG]

  Amefanikiwa kuanzisha website yake inayoonyesha kazi zake, unaweza kubofya hapa kuona kazi zake: www.josierussell.com.

  [​IMG]
  Josie na mpenzi wake Iwan Griffith

  Kwa sasa anaishi na mpenzi wake aitwae Iwan Griffith na wana matarajio ya kufunga ndoa.

  Hii hapa chini ni Documentary inayosimulia tukio zima lililoikumba familia hiyo:   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,098
  Likes Received: 6,562
  Trophy Points: 280
  inasikitisha sana.
  pole sana kwa Josie na baba yake.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi inasikitisha sana
  Pole sana kwa huyo mtoto Josie maana hiyo haitakaa imuondoke maishani mwake kushuhudia mama yake na ndugu yake wakiuwawa kikatili
  Ni kweli inauma sana
  Na pamoja na kuwauwa inaonekana muuaji hakupata lolote la maana zaidi ya kuishia kuiangamiza familia isiyo na hatia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Imany John

  Imany John Verified User

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Jah save us
   
 5. majany

  majany JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Safi Mtambuzi........!!!
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nafurahushwa sana na jinsi askari wapelelezi wa nchi za wenzetu wanavyofanya kazi kwa ueledi na uadilifu mkubwa ktk kupambana na matukio ya uhalifu wa namna hii. Ingekuwa kwetu Tanzania, na hasa ukizingatia baadhi ya askari wetu ndo pombe tupu huku wakitanguliza rushwa na kutimiza haja za viongozi wa kisiasa, kijana huyo asingekamatwa hata kidogo. Tunapaswa kujifunza toka kwao.
  Asante Mtambuzi kwa kutuletea kisa hiki ...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ninachofurahi ni kwamba wenzetu wapo makini na kazi hicho ndo kinachonifanya nifikirie kuish ulaya.usalama kwanza.lakini kwetu maslahi mbele.thanks mkuu mimi huwa ni Fan mkubwa wa posts zako.
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Duh
  Thank God that, this time baba hakuhusika; nilivyoanza kusoma nilipata wasiwasi kuwa huenda muhusika ni baba mtu, au hata mama kuwa aliuwa watoto wake na yeye kajiua.

  Salute kwa Josie, for fighting for her life na kufanikisha mtuhumiwa kutiwa hatiani; l hope she keeps living as she seems to be doing so.

  Kudos kwa police wa Uingereza, maana wa kwetu ndio wahalifu no moja, licha ya kwamba sidhani kama wana capacity ya kutengua vitendawili kama hivyo; sana wangepokea rushwa kutoka kwa mtuhumiwa na kesi ingeishia juu kwa juu. So sad indeed.

  Thanks Mtambuzi kwa another end of the week story!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ninachofurahi ni kwamba wenzetu wapo makini na kazi hicho ndo kinachonifanya nifikirie kuish ulaya.usalama kwanza.lakini kwetu maslahi mbele.thanks mkuu mimi huwa ni Fan mkubwa wa posts zako.
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwanza hongera sana Mtambuzi kwa kutuwekea visa kama hivi, ambapo pamoja na kuwa vinavutia na kusikitisha, pia vinatuonesha kwa kiasi gani nchi yetu ilivyonyuma, kwa makusudi au kupuuza, katika kushughulikia mambo mazito kama haya.

  Kama tukio hili lingetokea petu siku hizi, kwanza lingekuwa mgongo wa kupandia wanasiasa, pili baada ya wiki tu ingeundwa tume, kamati, jopo...na kesi kutangazwa kuwa iko mahakamani kwa hivyo hakuna ruhusa ya kuzungumzwa na kuwataka wadau waiache sheria kufuata mkondo wake.

  Ili kuonesha umakini wa wenzetu, kuna kisa kinaendelea hivi sasa Spain, ambapo baba, José Breton, anadaiwa kuwaua kwa kuwachoma moto watoto wake wawili Ruth na José wa miaka sita na miwili:

  [​IMG]
  Tukio hili lilitokea tarehe 8/10/2011 katika mji wa Cordoba, kusini ya Spain, ambapo baba alikwenda kuwachukua watoto wake toka kwa mkewe ambaye wametengana, na siku hiyo hiyo watoto kupotea. Katika muda wotw huu wa miezi kumi na moja, juhudi zinazofanywa kila siku na vitengo kadhaa vya askari polisi pamoja na hospitali zote kuu nchi nzima, hatimae zimepata ushahidi kidogo kutoka kwa mabaki ya mifupa na meno amabyo iliunguzwa kwenye joto la zaidi nyuzi joto 200, lakini wamehakikisha jinsia na umri wa watoto hao. Hivi sasa wataalamu wanajaribu kuona kama itawezekana kuona DNA kwenye mabaki hayo. Nikipata wasaa nitaweka muhutasari wa mkasa huo hadi ulipofikia.
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Thanks Mtambuzi,
  Yaani inasikitisha sana,
  Sisi wanadam kuuna kama wanyama mh.
  Pole sana kwa binti na baba yake maana pigo ni kubwa sana.

  Mungu akazidi kumpa faraja huyu binti.
  Ingekuwa bongo angekufa siku hiyo hiyo..
  Nawapa hongera sana madcs walioweza kuokoa maisha yake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Only BIG hearts can come to a normal life.....
   
 13. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  baba wafikra tena ndani ya nyumba duh inataka kufanana kwa mbaali na ya ulimboka sema wa kwetu amesusa kusema kwa sababu za kiusalama sababu huku kwetu waliohusika ni akina detective wenyewe thanks mtambuzi.
   
 14. Githeri

  Githeri JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 820
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mtambuzi kwa moyo wako wa kutupatia visa na masimulizi mbali mbali ya watu duniani. Hasa kwa muda wako pia waku tafsiri. Hongera sana.
   
 15. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kabisaa.
  Mtambuzi safi sana!
   
 16. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Km hilo tukio lingetokea tz zinekuwa zimeshaundwa tume na uchunguz wao usingewekwa hadharan. Sijui kwanini mwema hajifunzi toka kwa wenzetu badala yake amefanya jeshi la polisi kuwa tawi la ccm. Tubadilike na tujifunze toka kwa wenzetu
   
 17. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Inabidi polisi wetu wakajifunze job descrption zao ni zipi, maana wanaweza tu kuwadhibiti CHADEMA na kuwaacha wale walotoroka na mamilion pale CBA
   
 18. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Such a touching story!! kuna watu wakatili kweli duniani...Thanks for sharing Gustavo!!
   
 19. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mammamia yaani hii stori nayo inasikitisha, nilihadithiwa na mspanish mmoja colleague wangu hadi nilisisimka kwa uchungu. yaani huyo baba atakuwa katili sana kuwaangamiza malaika hao wawili tena watoto wake damu..
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kweli inatia uchungu. Huwa ninajiuliza mipaka ya haki za binadamu inaanzia wapi na kuishia wapi. Mtu kama huyu angenyongwa wangeibuka watetezi wa haki za binadamu na kupiga kelele.

  .
   
Loading...