Pale Katuni inapobeba maudhui mazito

Ngolinda

Senior Member
Apr 12, 2010
125
25
Ndugu wana JF,
Salaam,

Katika pitapita zangu mtandaoni nilikutana na Katuni hii. Ukiingalia kwa makini unaweza ukatokwa na mchozi. Si kwa sababu ya kuchinjwa kwa Demokrasia..bali kwa kile kinachowekwa mbadala wa Demokrasia. Waweza kuona kambi mbili: Kambi ya kwanza ni ya haki, usawa na Uungu yaani Godliness na Kambi ya pili ni ya dhuluma, ukandamizaji na nguvu za kuzimu yaani demonic powers (angalia maumbo ya kishetani). Kinachoniuma ni kwamba cartoonist anatuambia kwamba kwa sasa Tanzania yetu tunayoipenda imeangukia mikononi mwa kambi ya pili.

Ni hisia tu....tutaonana baadaye! 4945701.jpg
 
Yes, kwa watafsiri wa katuni hii inasikitisha sana!....Ndiyo hali ya Tanzania kwa leo.
 
Shame on you Judge mpindisha haki, mwenye records za hukumu zake jamani muweke jamvini hawa ma judge wawili Makame na yule msajili maana kama anachakachua bila soni wala haya hizo hukumu zake zilikuaje? na itabidi tuanze kufanya follow up za vizazi vyao :A S angry:
 
Jaji Makame ni mtu wa heshima kwenye taifa hili ametumia nchi muda mrefu...

Kama kuna mtu hana imani na Jaji makame hamna haja ya kwenda mahakamani kwani huko napo wapo majaji ndio wanaotoa hukumu
 
Jaji Makame ni mtu wa heshima kwenye taifa hili ametumia nchi muda mrefu...

Kama kuna mtu hana imani na Jaji makame hamna haja ya kwenda mahakamani kwani huko napo wapo majaji ndio wanaotoa hukumu

unasema? huyu mzee mwizi kama wezi wengine wowote wale, kaiba, kura, muda mali na furaha ya watanzania!!!!
 
Ya ndo democrasia ya tanzania hio tunayohitaji maana tunashindwa kuchukua hatua yoyote hata pale ambapo tunapokonywa wazi.Uchakachuaji wa kura ni wizi mkubwa kuliko hata wa EPA
 
Jaji Makame ni mtu wa heshima kwenye taifa hili ametumia nchi muda mrefu...

Kama kuna mtu hana imani na Jaji makame hamna haja ya kwenda mahakamani kwani huko napo wapo majaji ndio wanaotoa hukumu

Hivi ndugu, unaishi dunia gani wewe? Badala ya kukasirika wakati mwingine inabidi kuwaonea huruma viumbe kama wewe !!, maana hata masikini hujui kinachoendelea.
 
Mkuu,
does it real potray a true picture of our democracy?

Personally i find it exagrating the whole issue of democracy and particularly 2010 election
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom