Pale CHADEMA wanaponajisi Tunu ya kwenye Katiba

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Wimbo wa Taifa ni moja ya "tunu" zilizoainishwa kwenye Katiba. Kitu kikiitwa 'tunu" sifa kuu ni kuheshimiwa. Heshima kwa wimbo wa Taifa ni pamoja na kutouimba sehemu isiyostahili, kutobadili maneno, tune au mpangilio. Kwa mfano huwezi kuimba wimbo wa Taifa kwenye mazishi ya mbwa wako au kilabuni. Huwezi kuongeza maneno yako mfano useme "mungu ibariki Tanzania na ukoo wetu". Huwezi kuondoa neno "ibariki" uweke "iangamize"!

Sasa Jana nimesikia Ndugu Makene akiimbisha wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu CHADEMA. Aliuimba vyema hadi mwisho ila akaongeza alichokiita "fungu la chadema"!!!! Katika "fungu" hilo akaondoa "tanzania" akaweka hivi "mungu ibariki chadema, wabariki viongozi wa chadema na wanachama wake"!!

Hii haikubaliki! Ni kununua shida! Ni matumaini yangu wahusika na tunu hii ya Taifa watafuatilia suala hili ili ndugu Makene na wale wote walioshiriki kuinajisi tunu hii wawajibike. Hivi kama chadema hawawezi kuheshimu katiba kiasi hiki wakipewa nchi tutakuwa salama?

Nadhani pia wahusika watizame je ni sahihi kwa chama chochote cha siasa au taasisi isiyo ya kiserikali kuimba wimbo wa Taifa kwenye shughuli yake? Mfano je NGO ikiwa na kikao nayo inaruhusiwa kuimba wimbo wa Taifa na labda kuongeza "fungu' lake?

Tusiache hili lipite! Tutajuta! Iko siku watu watazika mbwa na wataimba wimbo wa Taifa na kuongeza "fungu" la mbwa!

 
Back
Top Bottom