Pale CCM wanaposhindwa kutofautisha Harakati na SIASA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pale CCM wanaposhindwa kutofautisha Harakati na SIASA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fredwash, May 26, 2011.

 1. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  katika miaka ya hivi karibuni CCM illiamua kuanza kutumia mbinu mbalimbali ili kuendena na kasi ya upepo wa mabadiliko unaoikumba tanzania na Dunia kwa ujumla. lakini cha kusikitisha hawakufanya reseach za kutosha au kukaa na wadau wao wakitumia rasilimali zao kuanalyses yaliotokea na yanayoendela kutokea hapa tanzania na duani kwa ujumla li wajue wa approach vipi mabadiliko haya kwa faida yao.

  kuna kitu CCM wanashindwa kukitofautisha. nacho ni hiki SIASA na HARAKATI. kwangu mimi sasa hivi tuna vyama vya SIASA na viongozi wa KISIASA pamoja na sehemu ndogo sana ambayo inazidi kushuka kila kukicha ya wanachama/wafuasi wa Kisiasa. ila idadi kubwa iliyobaki ni ya WANAHARAKATI/WANAMAPINDUZI. na ndio wanaoleta mabadiliko duniani na hasa huko nchi za kiarabu na ulaya. ingawa kwa hapa kwetu utaona kama bado wapo chini ya mwamvuli wa SIASA, ila amin amin nawaambi kuwa hao mnaowaona ni wafuasi wa kisiasa na kutokana na aina ya mazingira na desturi waliyokuwa nayo au mazoea. ila ukikaa nao mmoja mmoja na kuongea nao ndio utagundua kuwa dhamira zao na maudhui yao ni ya kiuwanamapinduzi

  kwa tafsiri yangu ya elimu ya Ngumbalo . MWanaharakati ni mtu ambaye huwa anahitaji mabadiliko ya kitu flani moja ni kwa kutoridhishwa na hali ya kilichopo ama ni katika kuboresha kile kilichopo kwa manufaaa ya jamii na kizazi kilichopo na kinachokuja. (ama kwa lugha fupi ni kuwa Mwanaharakati kazi yake ni ku maintain the world and make sure it will always remain the Better place to live hii ni kwa utashi wake yeye wa kile anachokiamini (kumbuka kuna wanaharaki wa weye milengo tofauti ila dhamira kuu ni moja kuwa kuwe na uwiano na haki kwa kile wanachokiamini kwa kila mtu pasipo kujali Dini na Jinsia au Rangi). ndio maana kuna wanaharakati wa haki za mashoga, na mengine yanayofanana na hayo.

  lakini MWANASIASA kwanza ni muwakilishi wa kundi ama aina flani ya watu tofauti na mwanaharakati ambaye anaweza akasimama peke yake hata kama the whole world would be against him/her, ndio maana mwanaharaki anaishia kuwa Mwanamapinduzi. lakini MWANASIASA ni mtu ambaye yupo kwa dhamira ya aina moja, kuhakikisha jamii ama aina ya watu anaowakilisha wanapata kile wanachoamini na kukipigania kwa maslahi yao na ya kizazi chao.

  Wanasisasa wetu na wote ulimwenguni wanapigania maslahi ya watu wa eneo husika. na hapo ndio kutakuwepo na Vyama vya SiASA vitakavyokuwa na nembo rangi au aina yoyote ile ya kitu kitakachowawakilisha wao na aina ya jamii inayowawakilisha.

  Tukirudi kwa CCM. kwa kifupi kinachotokea hapa kama ningepewa dakika sifuri ya kuwashauri CCM juu ya nini cha kufanya. ningewaambia haya. "Your battling with the wrong People. Vyama vya siasa vya hapa nchini sio wapinzani wenu kwa sasa bali Wapinzani wenu CCM sasa hivi ni Wananchi wa Nchi hii, ambao kila kukicha wanageuka kutoka kuwa wafuasi wa SIASA kwa Vyama ama viongozi wa ki SIASA na kuwa WANAHARAKATI. Na ndicho kinachotokea hata huko Ulaya na Mashariki ya Kati.

  utaona Misri hawakumng'oa raisi wao kwa shinikizo la vyama vya Siasa au sababu za kisiasa, na wala Tunisia, Yemen, barhain na nyingine nyingi hawapingani na watalawala wao kwa sababu za kisiasa na watu kutaka mabadiliko pamoja na kuchoshwa na Mifumo iliyodumaaa na iliyodumazwa kwa makusudi na viongozi ambao kwa makusudi na ubabe wamegoma kujirekebisha na kufanya vile inavyostahiki. utadhani walirithishwa nchii hizo na muumba wao. ama wao ndio wenye haki kuliko wengine.

  Kama nilivyosema mimi sio mtu wa mambo ya SIASA, kwa hiyo i just dont care who is ruling, as long i am playing my part to support my country same as he dose whomever is on power, he has to make usre we all have a fair DEAL, and legitimate Obligations, hakuna kuvunja sheria na uonevu. lakini pale inapoanza kuona mambo yanakwenda kombo, na nikiuliza jamani vipi naambiwa si hawa viongozi wako, then hapo ndipo ninapo catch their attention and get down to it to make sure their are doing whats they are suppose to do otherwise we kick them out.

  sasa hawawezi kuniita mimi mfuasi wa KISIASA kwasababu wao ndio chanzo cha mimi kuanza kuwa serious na mambo hayo ya kisiasa, sijali ni mtu wa chama gani atakaa pale madarakani, ali mradi afanye yale tunayoyataka ...

  CCM wamekuwa wakitumia udini, ukabila, stutus ya mtu na mengine yanayofanana na hayo katika kuwin favour ya wananchi na bado wamefeli vibaya sana, niliwahi kusema iliwatumia waislam kama mti wka ajili ya kivuli wakati wa mchana wajua kali ili hali itawatumia kama kuni kuwachoma ili wapate joto wakati wa usiku wa baridi kali.. na vivyo hivyo ndio wamekuwa wakifanya katika jamii zingine kwa kivuli cha ukabila na rangi.

  lakini baada ya kugundua kuwa jinsi mda unavyokwenda na idadi ya hao inaowaita wafuasi wa vyama fulani vya upinzani inazid ikugeuka na kuwa wana aharakati tena ikiongezeka kwa idadi kutoka hata ndani yao. mi nilidhani wangeshtuka na kuamua kukubali kuleta mabadiliko ambayo UMMA unayataka. ila wao wameendela kujiaminisha kuwa ni Vyama PINZANI vya SIASA ndio vyanzo vya haya yote na kwa gharama yoyote watavia dabisha wao na wafuasi wao.

  napenda kuwaambia CCM hata wakiungana na vyama vyote vya SIASA kikawa chama kimoja wakaunda serikali yao ikafanya utumbo bado we will TAKE IT TO THE STREET, and KICK THEM OUT, hatuangalii chama wala nasaba ya MTU tunataka mabadilko watanzania ni WANAHARAKATI ama WAITE WANAMAPINDUZI, ndio maana hizo tacticts zao za udini, ukabila na mengineyo yanayofanana na hayo zinaendelea kufeli , huu ni upepo wa mabadiliko kamwe they will never stand Againts it, its just a matter of time, they will see the true COLOR of SOLIDARITY and WILLNGNESS OF this poor TANZANIA, kama imeshaandikwa wang'oke watang'oka tuu.

  Hivyo nawaomba CCM wajue kujaa kwa watu kwenye mikutano ya Kisiasa ya vyama vya upinzani sio kwasababu wao ni wafuasi wa chama hicho bali wanachotaka ni kumu assess huyo mtu ili wajue kuwa watamuweka mtu pale ambaye atafanye yale wanayoyataka, kwasababu hatuwezi wote kuwa Viongozi na kwa sababu binadamu sio kama wanyama huwa tunaishi ki civilized so some one has to be in command but yet serving us, so we have to interview him/her before we gives him/her a chance, and if (s)he screws up we take him/her out and gives the job to another fellow and we will keep doing the same until we get the Right person for the job. haijalishi kama tutakuwa na ma rais 1000 alimradi we get the right person to do the DEED.

  CCM you better start to be resonable with people of this Country, because surealy i a m telling you you wont have time to go in exile, because your excution wont be for political purpose.

  u better keep your eyes and ears wide open gazing and listening to what happen in middle east and western countries, because the clock is ticking........ hao sponsers wenu wa nje mnaokula nao ndio watakuwa wa kwanza kuwa expose.

  yaani aliyejikuta akiwa mtumwa ndani ya nchi yake na kuamua kuwa mwanaharakati.......... anatafsiriwa kuwa mfuasi wa kisiasa ama wa ki dini.


  Mpoto alisema... ukiona paka kalala chali jikoni anza kuomba ruhusa kazini.... na pia alisema chura anapenda maji lakini sio ya moto, watanzania tunapenda AMANI but now ni HELL.
   
 2. g

  gambatoto Senior Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Too much mkuu. Summarize please
   
 3. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  kaka hakika nimejaribu kuangalia sioni hata pa kusummarize... anyway mimi sio mwandishi by professional ...lakini mbona naona ni kama paraghraph chache ukilinganisha na article nyingi tu ambazo zimeshawekwa humu very useful na zilikuwa ndefu kuliko hii....
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  With thanks added to Thanks.
   
 5. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  i appriciate mkuu....
   
 6. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Kuna wakati ni ngumu ku summarize, article ni nzuri mbona?
   
 7. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kuna msemo wanasema ya kuwa Afrika ni dampo au ni jalala lililokusanya mambo mengi sana kutoka kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea. Na wanasema Afrika kama haitafungua macho haitakaa iendelee milele. Hii kauli ninakaa ninaifikiria sana nikiangalia na mambo yanayoletwa na CCM kama ukabila, udini, nk. Sasa kwa mtindo huu wanaoutumia ccm inamaana wanajenga Taifa letu au wanatubomoa. Wanafikiri ni akinanani watalijenga hili taifa la watanzania ili waweze kuwa na maisha mazuri. Mimi nilishukuru mungu ya kuwa tumebarikiwa kuwa na lugha moja kama familia moja. Baba wa taifa kulielimisha taifa lake kwanza hakuwa na maana ya kuwa alishindwa kutumia mali zilizopo au hakuwa na marafiki ambao walikuwa hawazitamani. Nyerere alitambua ya kuwa Tanzania ni tajiri na ndio maana akaamua kuzuia ili tupate elimu na tuzitumie kwa manufaa ya watanzania wote. Na kweli katupa lugha moja ambayo unaweza kupiga yowe hata mtu aliepo wapi akasikia. Sasa wanzetu inakuwaje wanaivuruga nchi yetu kwa ajili ya kutafuta mikabataba ya kinafki, ubabe, sifa, ubinafsi, uongo, ulafi wa madaraka, ushikaji nk? Hii CCM ikikosolewa inaona kama inafundishwa na kuturudisha kwenye mafundisho ya mnara wa babeli. Kama kweli CCM inawadhamini watanzania kwa nini haya mambo makubwa yasiwekwe wazi kama hii mikataba, tenda, polisi wafanye kazi yao kama polisi, mahakama kutenda haki, kuwasikiliza wananchi wanapochukizwa na kitu ambacho hakina masilahi kwao?

  Ninachotaka kusema ni kwamba tusikubali kuwavumilia hawa wanasiasa uchwara wanaokimbilia dini, ukabila kutuwekea uadui kati yetu. Kama siasa zimewashinda basi wapumzike wawapishe wangine na wao waonyesha walicho nacho. Haki ni kitu cha ajabu sana, na hii kiu iliyopo Tanzania ya leo na haki inatafutwa sio kitu kingine. Tusiifanye Tanzania yetu ni dampo au jalala kama shimo la taka. Kwanza sisi wenyewe kwa wenyewe tukemeane kwanza tuweke maendeleao mbele kila mtu na dini yeke atajua mwenyewe. Tena ikiwezekana iwepo sheria kabisa ya kulinda hivi vitu viwili. Taifa letu tusiliingize kwenye mambo ya dini au ukabila.
   
 8. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  nakugongea thanks,mkuu! Nape, MS et al wamo humu naamini watasema 'point taken'
   
 9. g

  gambatoto Senior Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa nimeielewa, Ahsante sana mkuu. Nape upo hapo.
   
Loading...