PALANTIR: jicho la dunia kubwa zaidi ya Google.

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
Kwa wapenzi wa Movie za sci-fi kuna movie moja iitwayo Minority Report (2002) - IMDb iliyoigizwa na muigizaji Tom Cruise watakua wanajua nini namaanisha. Movie hii kwa ufupi imeigizwa ikionyesha maisha ya mwaka 2054 ambapo serikali ya USA walitengeneza programme ambayo inaweza bainisha mtu anayetaka kufanya uhalifu katika kipindi kijacho (predict crime before it happens).
Palantir kwa msaada wa Taasisi ya kiintelijensia ya Marekani (CIA) ni programme inayofanya kile kilichoigizwa kwenye movie hii ya Minority report huku tofauti ikiwa movie ile inawakilisha maisha ya miaka ijayo wakati @Palantir ni kitu kinachoendelea katika ulimwengu wa sasa, huku watu wachache wakiwa wanajua uwepo wa programme hii.
Palantir haina ofisi lakini ina kitu kinachojulikana kama SCIF - Sensitive Compartmentalised Information Facility. Hili ni jengo/chumba ambacho kimetengenezwa maalum kuzuia uingiliwaji wowote kutoka kwa aina yeyote ya uvamizi wa kimtandao(hacking) utakaokuwa umedhamiliwa kupata taarifa zinazohifadhiwa ndani ya programme hii.
Mwaka 2004, billionare Peter Thiel mwanzilishi wa PayPal, akiwa pamoja na Nathan Gettings, Joe Lonsdale, Stephen Cohen and Alex Karp walitengeneza Palantir.
Nia yao ikiwa ni kutengeneza kampuni ya kuhifadhi taarifa (data) sehemu ambapo hakuna mtu atathubutu kwenda chukua, ambapo kampuni hii hawakuiorodhesha kwenye soko la hisa kutokana na kuona itakuwa vigumu kwa kampuni kama hii kuiongoza ikiwa kila mtu ataweza kuwa na uwezo wa kununua hisa zake. Palantir inaangalia kila unachofanya na inauwezo wa kubashiri nini unatarajia fanya na kuwaarifu watu husika waweze kuzuia iwapo ni hatari.
Mpaka kufikia mwaka 2013, wateja wake walikuwa ni CIA, FBI, NSA, Centre for Disease Control, the Marine Corps, the Air Force, Special Operations Command, West Pointna IRS.
Palantir inamfatilia kila mmoja toka washukiwa wa ugaidi, mafisadi wakubwa ndani ya makampuni mbalimbali (Bernie Madoff alikamatwa kwa msaada wa Palantir) mpaka wasafirishaji haramu wa watoto (child traffickers). Haya yote yakifanyika kwa msaada wa kubashiri.
Pentagon wamekuwa wakiitumia programme hii huko Iraq kulinda majeahi yake. Sio kwamba programme hii inatumika vitani tuu, imekuwa ikitumika hata mtaa wa Wall Street ambako imekuwa ikitumika kuangalia watakitashaji wa fedha hadi wabadhirifu wa fedha na makosa mengine yahusuyo uchumi wa Marekani.
Kwenye mitaa ya Chicago na Los Angeles, Palantir inatumika kuangalia uhalifu ambapo jeshi la polisi hutuma taarifa za sehemu husika, muda na tarehe za nyuma za makosa yaliyofanyika ambapo baada ya taarifa kufanyiwa kazi hurudishwa kuonyesha maeneo gani yanahitajika kufanyiwa patrol zaidi. Huku Jamii ikilaumu yawezekana programme hii ndio imekua chanzo cha Polisi kuwa piga na kuwashuku sana watu weusi nchini Marekani. Kama ambavyo afisa mmoja wa jeshi la Polisi Marekani, Sgt Peter Jackson wa LAPD alivonukuliwa akisem “Detectives love the type of information [Palantir] provides. They can now do things that we could not do before”.
Palantir ina usiri sana kuhusu ufanyaji kazi wake, huku ikiwa na nguvu kubwa zaidi ya mitandao mingine kama Google, Facebook, Amazon, Microsoft na Apple. Tofauti ikiwa Palantir inafanya kazi chini ya kapeti (under the radar) kwa kazi maalumu tu.
Palantir: the ‘special ops’ tech giant that wields as much real-world power as Google
 
mada tamu hii! sasa utaona kwasababu haihusiani na yale mambo yetu ya sita kwa sita utaoona wachangiaji wachache sana au bado wapo bize kwenye harusi ya JOTI live
 
wenye Azam mnafaidi kweli
Tunafaidi kweli kuangalia harusi ya JOTI LIVE AZAM TV sasa ukitaka kujua wanasiasa siku hizi hawana soko usiku wa leo watu tungekuwa bado tupo bize na press conference ya ZITO.Hata hatukumbuki kama wanasiasa wameongea kitu leo.matatizo yetu angalau tunapata faraja kwa kicheko toka kwa Joti
 
mada tamu hii! sasa utaona kwasababu haihusiani na yale mambo yetu ya sita kwa sita utaoona wachangiaji wachache sana au bado wapo bize kwenye harusi ya JOTI live
hahhahah!!...isije kuwa promo ya tigo walintumia sms Jaza ujazwe inaisha tarehe 28/10/2017 :D:D
 
Back
Top Bottom