Paka wa nyumbani kafia miguuni mwangu; kuna cha kuhofia katika ulimwengu wa kiroho?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,034
2,000
Nyumbani kwangu hapa naishi na mke na watoto wangu wawili pamoja na binti wa kazi na ndugu wawili.

Sasa kuna kipindi kuna paka mdogo alikutwa maeneo ya karibu na mtoto wangu basi mtoto wangu huyo akamleta.

Ni kipaka cheupe chenye madoa ya brown kwa mbali, kilikuwa kidogo sana, Binafsi nilikataa kufuga paka nyumbani kwangu ila basi nikakubali kishingo upande baada ya wife kuwa upande wa mtoto wangu kwamba wamfuge.

Sikua na muda na huyo paka kabisa japo yeye nlikuwa namuona anavyokazana kufosi nimzoee, mfano alikuwa anapenda kupita pita chini ya miguu na hata napomfukuza alikuwa anarudi, Nlikuwa nashangaa inakuwaje paka hakazani kujenga mazoea na watu waliomzoea kama wife na watoto ila huku ambako hajaliwi yeye ndio anakutaka.

Kuhusu kumlisha wala hapakuwa na shida, Nlikuwa nashangaa sana jinsi anayvyojaliwa na watoto na wife, maziwa anapewa na kuna wakati mwengine ananunuliwa samaki.

Sasa kuanzia juzi sijui alipatwa na nini ila niliskia tu anaumwa, nikapotezea maana hanihusu sana, mtoto alikuja kuniasa nimwite daktari wa mifugo ila nikaona hii ni kuchezea pesa sasa maana huyu paka anakufa kama paka wengine tu, Ila alipoenda kwa mama yake naona daktari aliletwa sijui hata kilichoendelea.

Leo nipo nje hapa napumzika akaja analia lia nyau, nyau, nyau anapita pita kwenye miguu, namtoa anarudi, namtoa anarudi, basi nikamwacha tu, sasa naamka kwene kiti ile namwangalia nakuta katulia tuli, kumtikisa naona hamna response, nikajua tu huyu kashakata roho.

Anyway haikunistua sana ila jambo nalojiuliza hivi viumbe vikikufia karibu je kuna tatizo hasa katika ulimwengu wa kiroho?

Ni salama kuwazika kwenye eneo lako au ni bora kuwazikia mbali kabisa na kwako?
 

kelphin kepph

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
3,814
2,000
Aliwazalo mtu ndio limtokealo mkuu”kiumbe hai yoyote ana mwisho wake...nae kamaliza wakati wake.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,178
2,000
Mbona kawaida tu.
Paka ameumwa na amekufa karibu yako.
Angeweza kuwa kuku, mbuzi, ng'ombe nk.
Hakuna tatizo lolote.
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,034
2,000
Huyo alikuwa mlinzi wako kiroho na kuna shambulio amelidaka yeye na kuchukua uhai wake! Mpe mazishi ya heshima
Mkuu ni nyau tu huyu 😂😂 ila dah kitendo cha kuanza kuumwa tangu juzi alafu aje anifie mimi leo badala ya kwenda kwa waliokuwa wanamjali sana (watoto na wife) na kuja kwangu hiki kitendo kimenifikirisha, maana binafsi nlikuwa sina time nae kabisa japo alikuwa anafosi sana kupata attention yangu tangu zamani
 

AVRAM

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
616
1,000
Huyo alikuwa mlinzi wako kiroho na kuna shambulio amelidaka yeye na kuchukua uhai wake! Mpe mazishi ya heshima
Nilijua tuuu lazima mzee baba utasogea huku. Uko sawa sana kwenye ulimwengu wa kiroho. Maelezo yako huwa hayanipiti kwenye nyuzi kama hizi hutafuta comment zako tuuu.
 

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
3,697
2,000
Mpaka paka anakufa kizembe ipo namna! Paka ndio kiumbe mwenye uwezo wa kuona viumbe wengi tusioweza waona kwa macho. Mfano ni SCP-966
Mwenye huo uwezo mkubwa mkuu ni mbwa na sio paka na ndiyo maana wachawi huwa hawapendi mbwa
 

Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,063
2,000
Achana kabisa na Imani za kishirikina kwa kijifunza Tabia za Paka na viumbe wengine.wewe ndiyo mtuhumiwa wa kwanza wa mauwaji ya paka.huenda umempa sumu au umempiga. Kwa sheria ya ustawi wa wanyama Tanzania inakuhusu kabisa.ngoja niwajulishe wahusika haraka.
 

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,472
2,000
Wife alipewa paka na brother wangu huyu paka alikuwa mzuri kweli nilikubali kumchukuwa ila sikutaka awe anaingia ndani ya nyumba kwasababu ya harufu(mavi na mikojo). Huyu paka nilikuwa namnunulia vile vyakula vyao kwenye packets zao. Anapenda sana kuingia mwilini na kucheza kila wakati nilimpenda akitaka kunya au kukojoa anatoka nje au anakwenda kwenye poti yake ya mchanga chumbani kwake. Kuna siku nilitoka na wife tulimuacha korido wife alitaka tumuweke ndani nikasema mwache nje sisi tunarudi jioni leo na hii asubuhi.

Nikamuwekea maji/maziwa/dagaa na chakula chake cha packets. Tulipo rudi usiku hatumuoni wakati geti la nyumba na korido yote yalifungwa nikaanza kumtafuta kama 30 minutes tukamuona chini ya gari. Ila hana sauti nikamvuta nikaona miguu yake ya nyuma imevunjika na tumboni kuna mikwaruzo.

Wife akasema paka mkubwa atakuwa kampiga usiku mzima analia tu siku ya pili mapema nikamuweka kwenye boksi nimpeleke hospital ya wanyama ile nataka kutoka tu alikuwa anahema kidogo dogo hapohapo alikufa. Dume zima nilianza kulia🥲 nilimuwekea maziwa na chakula pamoja na taulo kwenye boksi na kwenda kumtupa jalalani. Roho iliniuma siku 3 mpaka leo sina paka ila soon nategemea kuweka mmoja na mbwa 2


Lunatic
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom