Paka awa mrithi wa utajiri wa bilioni 465

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Paka aliyekuwa akimilikiwa na mkongwe wa mitindo Duniani marehemu Karl Lagerfeld ndie atakayerithi utajiri wote wa mkongwe huyo.


Marehemu Karl Lagerfeld akiwa na Paka wake.

Paka huyo anayefahamika kwa jina la Choupette atamiliki utajiri wake ambao unatajwa kufikia zaidi ya shilingi Bilioni 456 za Kitanzania na inaripotiwa kuwa paka huyo alikuwa akilelewa kifahari na mmiliki wake tokea mwaka 2011.

Karl Lagerfeld alifariki Jumanne ya Februari 19,2019 jijini Paris akiwa na umri wa miaka 85 akiwa miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya pazia ya mafanikio ya nembo kama Tommy Hilfiger, Chanel na Fendi mwaka 1980.

Umaarufu wa paka huyo umekuwa mkubwa hata katika mitandao ya kijamii, ambapo katika ukurasa wake wa Instagram unaoendeshwa na mtaalam wa masoko mitandaoni, Ashley Tschudin, umefikisha jumla ya wafuasi 120,000

Eatv
 
Na paka akifa ? Maisha haya

Sent using Jamii Forums mobile app
Atarithi mdogo wa paka au mtoto wa paka anae husika na ukoo huo wa huyo paka.

Saizi nafanya mpango nimchukue huyu paka shume wangu wa humu ndani nimpeleke huko azini na huyo bilionea halaf akijifungua tu nasubiri bilionea afe halafu utajiri utakua unamilikiwa na paka wangu ambae mimi ndio nitakua msimamizi wake, kwaiyo hapo mimi nitakua kijakazi wa mtoto wa paka wangu aliyezaa na paka bilionea

Sent using unknown device
 
Kuna:
paka shume.
Paka chongo
Paka mabaka
Paka jizi

Ila huyu ni Papaa Paka, mtoto ya Parii paka ya mupesa kedekede...

Yaani anaweza akakuparua na akaulipa.

Anaweza akakupeleka mahakamani.

Nb
Huyu paka awe makini sana ktk nyendo zake vinginevyo atawapa watu pesa ovyovyo. Kwa mfano mimi nikiwa napaka wangu kisha huyu paka akazaa au azalishwa na huyo Papaa Paka mutoto ya Parii naenda kudai Cat support mahakamani.


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Back
Top Bottom