Paka anyofoa nyeti za babu; Akimbia na kuzila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paka anyofoa nyeti za babu; Akimbia na kuzila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bangusilo, Feb 24, 2011.

 1. Bangusilo

  Bangusilo Senior Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maajabu
  Wednesday, 23 February 2011 09:29
  *Paka anyofoa nyeti za babu
  *Akimbia na kuzila

  Na Waandishi Wetu, Manyara

  MAJONZI na masikitiko vilisababisha kikao cha wazee kuvunjika ghafla baada ya mzee mmoja kunyofolewa sehemu zake za siri na paka aliyekimbia nazo.
  Tukio hilo limetokea Februari 20, mwaka huu, saa 11 jioni, mwaka huu, Babati, Mkoani Manyara.

  Mzee huyo ambaye hivi sasa hali yake ni mbaya amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara, ambapo madaktari wa hospitali hiyo wamelazimika kuzikata nyeti hizo.

  Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mzee huyo alikuwa na kundi na wazee wenzake wakimjadili binti aliyetoroshwa na kijana mmoja kijijini hapo.

  Amedai kuwa wakati kikao hicho kikiendelea mzee huyo alikuwa amevalia mavazi msuli na ndani akiwa hajavaa nguo za ndani na kusababisha sehemu zake za siri kuwa nje.

  Wakati kikao hicho kikiendelea ilidaiwa kuwa katika kiti ambacho alikuwa amekaa mzee huyo chini kulikuwa na paka ambaye alikuwa akicheza cheza.

  Ilidaiwa kuwa paka huyo alikuwa akizunguka zunguka maeneo hayo na ghafla aliruka na kunyofoa nyeti za mzee huyo na kukimbia nazo juu ya mti.

  Kutokana na tukio hilo, wazee hao walishindwa kumkimbiza na kumkamata paka huyo na badala yake walianza kumsaidia mzee huyo ambaye damu zilikuwa zikivuja kwa wingi na kisha kumkimbiza katika hospitali ya wilaya ya Babati.

  Hata hivyo, kutokana na kitendo hicho, baadhi ya wakazi wamedai kuwa kinaweza kuwa ni cha kishirikina kutokana na paka huyo kunyofoa nyeti hizo na kukimbia nazo juu ya mti na kuanza kuzila.

  Dar Leo liliwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmenas Sumari, ambaye hakuweza kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa hizo kutomfikia ofisini kwake.

  “Inawezekana hili tukio likawepo lakini wakaamua kwenda hospitalini kwa kuwa si la kipolisi zaidi ila ofisini kwangu bado halijanifikia,” amesema kamanda.

  source:
  Maajabu
   
Loading...