Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Niliwahi kuweka mada ya micro chips implants lakini kuna baadhi hawakuelewa kabisa..ni kweli kabisa mason wana mpango kabambe wa kuua mlango wa fahamu ya sita ili ile ni rahisi kutawala dunia
63b6ed4254840d649337abc3e6065fea.jpg
2e3a134ba50d2bd65ea492b9c99db901.jpg
9b5321d83a1038b6340eaeff1eb72132.jpg
Hii mada i wapi nimeielewa
 
f6e63668ac1c4a88887ca94b0bd11c01.jpg

Hutaamini utakachogundua hapa kuhusu paji lako la uso...hapa ndio asili ya neno kipaji ilipatikana..hapa napo ni lango hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani jicho lisioonekana.lango kuu la kiroho.

Tutaenda kwa mitazamo yote ya kidini na kiimani, kisayansi, kihisia na hata kwenye nguvu za giza.

1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus
c028b8f6365bdd2fb44aaf6796fdf17f.jpg

Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.

2. Mathematics
22f4856d4325c03356542c3c19a96824.jpg

Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.

3. Tahjud (Meditation)
1a3f1076a0eecca2d21fb8771039a216.gif

Kwenye tahajudi wale waliosoma chakra na habari za milango nane, ukiangalia vizuri huo mchoro chakra ya sita ndio ya kuingilia mlango wa sita wa fahamu.

4. Baptism & Sijda
b23bbe047b4fed53bc8acd968bfbde9f.jpg
7581aaa5dd84dc3d74104360bf95c259.jpg

Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..

Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.

5. A kiss on the Forehead
95e4888b95b1f04ef937618e752fd13d.jpg

Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.

6. FREEMASONRY
2eaa591e515e975051f9640238953750.jpg

Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu

7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)
8654ca9f3d106b3012aa7228ab664632.jpg

Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.

8. Michezoni:
Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.

Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.

Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.

Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.

Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.
Hata SIJDA hutokea kwenye paji la uso

In fact hizi thread huchanganya sana
 
Mtu anasehemu tatu ana mwili..(physical body) and Moyo (hapa sio moyo wa damu rather akili-subconcious mind) na roho(spirit-ambayo ni presence of God)

Roho ipo kutukumbusha kutembea katika njia ya Mungu. Hii inatusukuma kwa kutukumbusha ubaya au wema Wa vitu kabla hatujavifanya au tunapoendelea kufanya au tunapomaliza kuvifanya.. Ubaya haikulazimishi usifanye ila inatoa angalizo tu na hasa ukidevelop tabia ya kuiheshimu sauti hiyo ambayo huja kwa mfumo Wa self doubt..

Subconscious mind ndio sehemu nyingi tunaitumia km moyo. Katika dini tunasema itunze sheria ya Mungu moyoni, Au mtaani unasiki huyu mwana ana moyo wa kipekee au anampenda kwa moyo.. Moyo hauna yote hayo... Kinacho yafanya yote haya ni akili... Subconscious mind sio rahisi kuicontrol ila kwa hakika inacontrol action zetu..

Mfano akili yetu ya kawaida inatufanya tufanye routine things kwa ufasaha .. Ila tunapochukua muda kumeditate juu ya routine things tunaanza kuconcive ideas za incident ambazo hazijatokea bado na kuja solution ,..kwa wakati zinaweza kuwa minor nazikawa suppressed usikumbuke tena... Ila kwenye incident umekubwa na live scenario ya kitu kile unajikuta umereact same way km ulivo conceive..

Hii inaweza kuelezewa na mfano Wa mtu ambaye ni muoga wa kuruka sehemu ndefu ktk purukshani za kujiokoa kutoka sudden threat ..anaruka vizuri sehemu amby anabaki anajiuliza... Au mtu anayewahi na kumuokoa mtt aliyesimama ktk reli wakt train inakuja .. Au mess anayefanya move uwanjani akiulizwa anasema ht yy hajui ilikuwaje.. Wote wanaongozwa na subconscious mind.. Japo ni wachache sana wenye uwezo Wa kuimunipulate,..

Katika mfano wako wa maombi .. Inabidi vyote vitatu mwili..Moyo na roho viwe in harmony. Unaposali kwa Mungu wako na ukawa una mashaka ya kimwili hakuna kitu.. Ikiwa Subconsciously unakubaliana na Roho(yeye ndio hutoa signal za ubaya wote) na ukazifikiria kwa kina katika misingi ya imani yako... (Hapa muda na concentration ni muhimu) naturally subconsciously utakuwa unaepuka ubaya kwa kuutenda au kukutana na watu wabaya bila kutumia nguvu ...(instinct) kwa maana mwili wako sasa kupitia kuona kuhisi kuonja nk utakuwa na uwezo wa kung'amua in secs.

Ktk hali ya kawaida mtu anayetumia muda wake kusoma na kumeditate katika maswala Fulani..mfano biashara ataziona fursa kwa hrk kuliko asiyefanya hivyo..au kuliko aliyeanza muda mfupi tu.. Maana ni kupitia kujifunza katika mwili na kujitoa kwa moyo kufikiria tuliyojifunza tunafungua nguvu iliyoko ndani yetu kufikiria zaidi katika hali isiyokuwa limited(mwili) kuona mambo katika muktadha usiokuwa na mwisho (moyo-subconcious realm)

Nimekuelewa sana mkuu..
 
Nimeipitia yote Na kujifunza kitu kikubwa Na kimenibadili mtazamo wangu kwa namna moja ama nyingine., Mungu azidikukutia nguvu katika kuendelea kutujuza mwalimu.,
Hii elimu dunia tunaipatia huku wengine.
Shukrani nyingi kwako Mshana Jr. na wengine wote mliochangia
 
Asante sana am humbled..!!!
 
Mkuu Mshana Jr Asante sana kwa uzi huu ingaweje nimeuona tuu juzi. Nimeusoma mwanzo mwisho na michango yote pamoja na majibu uliyotoa. Hii thread imenifungua katika kifungo kikubwa sana. Nimeanza kusoma kitabu cha The power of your subconscious mind na naendelea kufunguka zaidi. Kusema ukweli shetani amekuwa ananitumia sana maana nimekuwa mtu mwenye hasira sizizo za kawaida, furaha kwangu ilikuwa ni kitendawili kikubwa sana. Kwa kifupi nimepitia mengi sana na watu wamenitenda vibaya sana kiasi kwamba vingine hata siwezi kuelezea ila kwa kifupi nimepitia mengi na mazito sana sana ila hii thread imenifungua sana. Nilianza Tahajudi baada tu ya kusoma hii thread na huwa nafanya usiku kabla ya kulala na Alfajiri na kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya kumi nimejiona ni mwenye furaha. Mwili umekuwa mwepesi sana nimeanza kuwasahau watesi wangu na najiona kama nakuwa mpya kabisa. Nikijiangalia kwenye kioo najiona kama nimeanza kung'aa najiona mpya kabisa..nimeanza kuwaoana watu kama viumbe wa kawaida kwani hapa nyuma nilikuwa nawaona watu kama wanyama na sikuwa mtu wa kukutana na mtu yoyote yule na kumuona kama mwenzangu lazima niwe na tahadhari ya hali ya juu sana..kwa sasa nacheka na watu na nayaona maisha kama yenye furaha kwa sasa.

Sehemu nilipo kwa sasa sio tulivu sana ila najitahidi kuweka akili sehemu moja wakati wa kufanya tahajudi ila disturbance za hapa na pale zipo na siwezi kuzizuia maana nipo naishi Lodge kwa sasa kutokana na shughuli ninyafanya. Nimeanza na tahajudi ya kulala chali na kuvuta pumzi na kuiachia taratibu sana, jana nilifanya tahajudi na kuna wakati kama nilitaka kupaa vile nikawa nimeshtuka nikajikuta nimerudi kitandani ila kusema ukweli imenisaidia sana sana. Asubuhi naamka nikiwa mwepesi kabisa kitu ambacho sio kawaida yangu. Nimeanza kuwa mchangamfu sana hata wahudumu wa lodge waninishangaa mpaka mmoja juzi kaniuliza umekuweje mbona siku mbili tatu hizi umekuwa mwenye furaha sana?? Nikamwambia acha tu dada yangu mambo mengine tumwachie tu Mungu.

Mkuu Mshana Jr kuna jambo ambalo lilikuwa linanisumbua na hata baada ya kuanza tahajudi naona bado linanisumbua. Kwanza kabisa mm huwa napendelea sana kulala chali na mara kwa mara huwa napata ndoto za ajabu ajabu sana ila zinazonisumbuaga sana ni zile ndoto ambazo najikuta napiga story na ndugu zangu ambao ni marahemu. Wakati mwingine story zinakuwa nzuri ila wakati mwingine tunakuwa tunagombana. Hizi ndoto huwa zinaninyima amani kabisa. Baada ya kusoma thread yako na comments za watu kuhusu madhara ya kulala chali nilianza kujizoeza kulala kwa ubavu(sijui ndo unaita mshazari) basi hali kama imebadilika nikiweza kulala kwa ubavu sipati tena hzo ndoto...ila sasa tatizo ni kwamba nakilalala nalala kwa ubavu ila usiku nikishtuka najikuta nimelala chali na hyo mindoto ya ajabu ajabu ninakuwa tayari nimeipata ingawaje kwa sasa imepungua kidogo. Sasa mkuu hapa nifanyeje maana hii mindoto kweli huwa inanikera sana. Kwa mfano jana nilipata ndoto naongea na kaka yangu ambaye ni marehemu ananiomba nimtafutie kazi. sasa mm nikawa ninamuuliza nitakutafutiaje kazi wakati wewe ni marehemu, akawa anang'ang'ani tu nimtafutie kazi....mwisho tukaishia kugombana ndo nikastuka nikajikuta nimelala chali... Mkuu wangu ebu nisaidie kwanza nawezaje kulimaliza hili tatizo la ndoto za ajabuajabu kabla hatujaendelea na mengine maana ninayo mengi ambayo nitahitaji msaada kutoka kwako kama hutojali. Natanguliza asante,
 
Asante na hongera kwa kupata mafunuo mapya... Muda mwingi kinachotutesa na kutuumiza sana hakitoki mbali bali kiko ndani ya ufahamu wetu.. Hivyo tunapofunuliwa na mada kama hizi na kuweza kubadili mitazamo yetu, hujikuta tukitoka kwenye vifungo vilivyotutesa muda mrefu sana huku vikituachia makovu mengi
Kuhusu kuota ni lazima uote.. Ndoto huleta afya ya akili lakini si zote... Sasa endelea kujizoeza kulala ubavu hata kama ukistuka usingizini umelala chali rudi kwenye position ya awali
Mwisho nakushauri sasa pamoja na kuendelea na tahajudi punguza matumizi ya vileo, nyama kahawa na kitunguu maji... Pia jizoeze kuogea maji ya chumvi kila mara
 
Back
Top Bottom