Pagasus Spy - Zero Click softaware ya Waisrael inayotumiwa na mataifa makubwa kuhack simu yoyote

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,027
Kampuni ya Israel inayoitwa NSO Group, iliunda program inayojulikana kama Pegasus (Zero Click). Hii software kwa madai ya kampuni hiyo hawauzi kwa watu binafsi ila ni kwa ajili ya serikali za nchi mbalimbali na ni kwa pesa ndefu na inakuwa na limitation ya muda lets say miezi sita ukitaka kuendelea kuitumia unalipia tena.

Software hii inajulikana kama zero click, yani simu yako inakuwa hacked pasipo wao kuigusa wala wewe kufanya chochote. Kinachofanyika itapigwa simu kwenye simu yako wether utapokea au hutopokea ili mradi simu imepigwa kwenye simu yako basi ishakuwa hacked, hii ndiyo sababu ya kuiita zero click.

Waandishi wa habari wa Aljazeera arabic walikuwa hacked simu zao na simu ikiwa hacked wanaweza monitor chocote, iwe mic, ya simu kutumia kusikiliza mazungumzo ya watu waliyo eneo hilo, kutumia blutooth kuwasha vifaa vingine, kumonitor message, na calls, kutumia camera kutazama kinachoendelea maeneo hayo. Kampuni ya Canada ya mambo ya ulinzi wa kimtandao, uligundua simu zao zilikuwa monitored kutoka Saudi Arabia.

Swali linalowatia watu hofu, je hii kampuni hii software inauzwa kwa serikali tu au hata watu wengine wenye uwezo wa kununua, na je serikali ina monitor watu gani. Na hii software inafanya kwenye iOS na Android. Uwezo wa software hii unawaacha midomo wazi watu wengi maana ni technology ya hali ya juu sana.

Ni tofauti na hacking nyingine ambazo unatumia link unahitaji kuclick link ili uwe hacked, jambo ambalo ni rahisi kulishtukia.
 
Mimi hua nablock incoming call zote, labda nikupigie sasa hapo hao hackers kazi wanayo.
Unablock kwa njia gani mkuu ile ya kwenda kwenye block calls au ya kudivert? Kama ni kwenye settings basi hujasolve kitu ila ni kwamba call uwa inaingia simu inawahi kuikata, na pagasus kitendo cha call kuconnect na simu yako basi inatosha.

Hata hivyo hawana shida na watu kama sisi wao wanadeal na watu wanaowahitaji kwa mtu kama mimi wataambuliwa kusoma matatizo ya familia, sms za michepuko, madeni ya voda kunikumbusha nilipe deni la songesha
 
Unablock kwa njia gani mkuu ile ya kwenda kwenye block calls au ya kudivert? Kama ni kwenye settings basi hujasolve kitu ila ni kwamba call uwa inaingia simu inawahi kuikata, na pagasus kitendo cha call kuconnect na simu yako basi inatosha. Hata hivyo hawana shida na watu kama sisi wao wanadeal na watu wanaowahitaji kwa mtu kama mimi wataambuliwa kusoma matatizo ya familia, sms za michepuko, madeni ya voda kunikumbusha nilipe deni ya songesha
Natumia kitochi, bado kazi wanayo
 
Pia wanahack kwa kutumia "Third parties" yaani wanatumia namba yako lakini ipo kwa mtu mwingine ambaye mnawasiliana naye mara kwa mara. Pia kuwa na uwezo kuwa " dormant " mpaka iwe activated " either on site or remotely".
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom