TANZIA Padri Wilfrid Dinho Wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Afariki Dunia

Ameniuma sana, bado naona picha yake inakuja kichwani full, kipe kipindi tunakaa pamoja na kuongea mambo kadha kunifundisha na kunipa moyo na kunijengea moyo wa kujiamini katika uwezo wangu.
Sasa mbona huo Moyo wa kujiaamini aliyokujengea Padri haoneshi kwenye kifo chake!? Unalalamika Kama vile kifo ni uonevu!!
 
Mimi nawashangaa akina Father Kitima, kazi kulaumu serikali tu wakati wao kama kanisa wamechukua hatua gani? wafunge makanisa hadi janga hili lipungue, Italy na Ulaya walifunga.

Hapa nini kinashindikana? Kututajia idadi ya mapadre na ma sister wanaokufa sio suluhisho hata kidogo, kanisa wachukue hatua wao, maana jumuia zinaendelea, mikusanyiko makanisani inaendelea, alafu akifa padre lawama kwa serikali, kwani serikali ndio imewaua? kipi kigumu wasisitishe kanisa kwa miezi kadhaa? Au hawaoni Italy etc
Wakisitisha Kanisa,na Sadaka zitasitishwa pia!!
 
Usiwashangae . Nchi hii tumejiwekea kitanzi sisi wenyewe. Kuna mtu amepewa mamlaka za kimbingu na katiba ya nchi, na jambo lisilompendeza yeye basi inatakiwa wote mlichukie bila kuhoji . Hapo ndipo tulipokwamia
Kwani makanisa si yao kwanini wasiyafunge kwa muda?
 
brazaj umesha hama kwenye Barakoa Sasa uko kwenye kupiga Kampeni ya Chanjo! Usiogope sana kila nafsi lazima itaonja umauti,yote ni Mipango yake Mungu!!

Barakoa na chanjo zote zinapambana na yule yule. Covid 19 na wajukuu zake. Wewe huna habari hiyo?

Kuhusiana na kila nafsi kuonja mauti palikuwa na uzi hapa. Nadhani unakuhusu sana jombi:


Kwa vile utaonja mauti unaona je kama ukayaonja leo hii mkuu?
 
Ni nani aliyezuia chanjo ya korona tanzania? Ni kanisa? Ni nani aliye entertain kutokuvaa barakoa? Ni kanisa? Ni nani aliyetangaza kuwa tanzania haina korona? Aliyedai kuwa corona "imekoronea mbari huko" si mkubwa wa nchi? Au ni askofu?
Nani kakudanganya kuwa waliochanjwa hawaendelei na tahadhari?


Hebu kasome WHO wamesemaje?
 
Kwenye hili ni tofauti mkuu,leo asubuhi waziri ametoa statement ya serikali kwa msisitizo kuwa ni marufuku kutangaza hata vifo vya wapendwa wetu,huko mwanzo hatukuwahi kuzuiwa kufanya hivyo,zamani ikitokea tatizo la mlipuko wa maradhi serikali ilitoa taarifa na kusisitiza kuwa kila atakayepata ujumbe huu amwarifu na mwenzake,kwenye hili tunaambiwa hata kama una taarifa kaa kimya!! Usimwambie yeyote,zamani kipindupindu kiliitwa kipindupindu hivyohivyo,na mtu akifa kwa kipindupindu tuliambiwa wazi ili wengine tuchukue tahadhari,leo huruhusiwi hata kutamka neno corona mbele ya wenye mamlaka,toka kitambo tuliambiwa kuwa chanjo ni haki ya kila mtu,ila chanjo ya corona imekuwa haramu kwa nchi yetu tu! Tafakari,na ujue si kila hatua una haki ya kuchukua,hasa ukiwa mtanzania
Hiyo chanjo bado sio suluhisho bwashee
 
Halafu Jana wamekuja na drama kwenye vyombo vya habari kwamba wagonjwa wa changamoto za kupumua wamepungua muhimbili wakati watu wanaendelea kufa.

Yupo rafiki yangu mjomba wake alikufa wiki iliopota hsptl ya mount meru Arusha wakakosa hifadhi pale mochwari kumejaa,wakahangaika kwingineko pale mjini Arusha ikiwemo na hsptl ya seriani nako kumejaa.

Ukweli ni kwamba serikali haijaleta corona lakini msimamo wake usiofaa umekuwa chanzo cha kusambaa corona na kuuwa watu.

Raisi anasifia padre hadharani kwakutovaa barakoa,daladala watu mrundikano,viwanja vya mpira,kumbi za sinema nk.

Ila nahisi Mungu anakusudi fulani ngoja tusubiri.
Padri alietangaza vifo vya wenzie amevaa barakoa kiroho na yeye!!!
Corona imeleta misuguano hatari
 
Mimi nawashangaa akina Father Kitima, kazi kulaumu serikali tu wakati wao kama kanisa wamechukua hatua gani? wafunge makanisa hadi janga hili lipungue, Italy na Ulaya walifunga.

Hapa nini kinashindikana? Kututajia idadi ya mapadre na ma sister wanaokufa sio suluhisho hata kidogo, kanisa wachukue hatua wao, maana jumuia zinaendelea, mikusanyiko makanisani inaendelea, alafu akifa padre lawama kwa serikali, kwani serikali ndio imewaua? kipi kigumu wasisitishe kanisa kwa miezi kadhaa? Au hawaoni Italy etc
Kwa hili nakuunga mikono na miguu. Naishi karibu na kabisa la Roma shughuli zinaendelea kama kawaida ibada 3, wanaovaa barakoa hata robo hawafiki, idadi ya watu ndio usiseme. Waumini ndio wanawaletea watumishi. Hata hili nalo atalaumiwa Magufuli? .Wachukue hatua.
 
brazaj umesha hama kwenye Barakoa Sasa uko kwenye kupiga Kampeni ya Chanjo! Usiogope sana kila nafsi lazima itaonja umauti,yote ni Mipango yake Mungu!!
Alianzia lockdown, akaja quarantine, akaja barakoa akasahau maji tiririka na Sasa yuko kwenye chanjo, maskini anaishia kusaidia mabwana zake tu hizi kelele lakini serikali yake haina habari na yeye.
 
Padri alietangaza vifo vya wenzie amevaa barakoa kiroho na yeye!!!
Corona imeleta misuguano hatari
Comments zako zinahuzunisha . MnatakaJe, kwakuwa mheshimiwa anataka twende kienyeji ndiyo tutasalimika na Corona ?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom