Padri, wengine wawili wafa wakiogelea

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
564
1,000

Geofrey-Kamwela-December5-2014.jpg

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela

Watu watatu wamekufa maji akiwamo Padri wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Same, Amedeus Mangia na wengine tisa kuokolewa baada ya kupigwa na dhoruba kali wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga, alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi na kwamba watu wengine wawili waliopoteza maisha katika tukio hilo bado hawajatambuliwa majina yao.

Alisema walionusurika ni wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Chanjale kinachomilikiwa na Parokia ya Mtakatifu Stephen ya Same, ambao wote waliokolewa wakiwa hoi.

Ndemanga alisema siku ya tukio, wanafunzi hao wakiwa na mwalimu ambaye ni Padri Amedeus, walikwenda katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kufanya hafla fupi ya kujipongeza kwa kuogelea na ghafla wakiwa majini, wimbi kubwa la maji liliwapiga na ndipo baadhi yao wakpoteza maisha.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema Padri Amedeus, kabla ya kufikwa na mauti hayo aliendesha ibada katika kanisa dogo lililopo eneo la bwawani Nyumba ya Mungu.

Baba mzazi wa padri huyo, Saimon Mangi, alisema mwanaye aliopolewa na wavuvi kutoka bwawani akiwa tayari ameshafariki.


MVUA YALETA MAAFA
Katika hatua nyingine, Ndemanga ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya yake, alisema kuwa mtoto ambaye bado hajafahamika jina, mkazi wa kijiji cha Tolowa wilayani hapa, alipoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kuonyesha wilayani humo na maeneo mengine mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alipoulizwa alikiri pia kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa kwa vyombo vya habari.

CHANZO: NIPASHE
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
12,170
2,000
Mimi nilijua watataka kumuiga yule nabii mnaigeria aliyetaka kutembea baharini,kumbe wamepigwa na dhoruba!pole familia za wahanga,walale wanapostahili...
 

kaka km

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,336
2,000
Padri anaendaje kuogelea?anaenda kuwaonyesha waumin pichu yake?anawafunza nini waumini?alafu tunalaumu maadili yameshuka.
 

bmy

Member
Nov 2, 2014
36
95
Hamna maadili as hv kwa mapadri wa Rc. Wanadai kwenda na wakati huku wanaharibu
 

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,014
2,000
Mimi nilijua watataka kumuiga yule nabii mnaigeria aliyetaka kutembea baharini,kumbe wamepigwa na dhoruba!pole familia za wahanga,walale wanapostahili...
Kuogelea ni mazoezi kama mengine, sasa mambo ya imani za kineigeria yametoka wapi tena? Au wewe wa mama mdogo eti ehe? Mkiristo akifa unasema kafiri amekufa..
 

kahtaan

JF-Expert Member
Jul 11, 2009
17,718
2,000
Padri anaendaje kuogelea?anaenda kuwaonyesha waumin pichu yake?anawafunza nini waumini?alafu tunalaumu maadili yameshuka.


Hawa walikuwa wanafanya mzoezi ya kutembea Juu ya maji.

We Huna habari ukiweza kutembea juu ya Maji Ni Mtaji wa kutosha sana huo?

Sasa wazungu wanaofanya hivyo wanakuwa wameweka Vitu chini ambavyo Havionekani kwa Waumini
Tatizo lenu nyie wagakatia wa Afrika Mnaingia Mazima!
Hapo Ndipo balaa inafuata!

Poleni sana aisee!
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,544
2,000
Padri anaendaje kuogelea?anaenda kuwaonyesha waumin pichu yake?anawafunza nini waumini?alafu tunalaumu maadili yameshuka.

Tena wanafunzi wake!! Ama kweli, tumekwisha na wengine wanasapoti hili. Kama huyo Bwana anaona, amewapelekea ujumbe wengine washtuke.
Sifurahii kifo cha yeyote ila hapa mhhhh
 

Mangwelele

Senior Member
Jul 22, 2013
111
195
mcba ni mcba 2 jamani 2we na huruma m2 anavyoandika kua alijuani m2 wamaana kumbe ni padri anamaanixha nn?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom