TANZIA Padri Monsinyori Deogratias Hukumu Mbiku wa Chuo kikuu Dar Es Salaam Afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
PUMZIKA KWA AMANI MONSINYORI DEOGRATIAS HUKUMU MBIKU

Wapendwa Mapadri, Mashemasi, Watawa na taifa lote la Mungu, Kristo.

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Monsinyori Deogratias Hukumu Mbiku wa Jimbo Kuu la DSM, aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Chuo Kikuu.

Monsinyori Mbiku amefariki leo tarehe 04 Aprili 2021 saa 12:45 jioni katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa, DSM, alipokuwa akitibiwa. Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu.
Naomba tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni.

ASANTENI.
+ Jude THADDAEUS Ruwa'ichi,
Askofu Mkuu wa DSM.
 
Mosinyori ni wadhifa anaopewa Padre aliyefanya mambo mazuri Sana ktk Utume wake.Wadhifa huo hutolewa na Papa baada ya kuombwa na Askofu wa Jimbo ambalo Padre husika yumo.

Wadhifa huo hauendani na madaraka yoyote Yale isipokuwa tu heshima ya kiprotokali mbele ya mapadre wenzake (first among equals) mosinyori kwa sheria mpya za kanisa lazima awe na 60+yrs
 
Asante.

Huyu alifanya nini mpaka akapewa?
 
Back
Top Bottom