kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 265
Wednesday, 01 December 2010 21:50
0
digg
Joyce Joliga, Songea
WAUMINI wa Kanisa Katoliki wa Parokia ya Matogoro, Manispaa ya Songea, wamelazimika kuendesha mchango kwa ajili ya Padri Alphonce Mapunda, ili aweze kupata matibabu ya mgongo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ilifikiwa juzi baada ya kuguswa na tatizo linalomkabili kiongozi wao, huku wakiombwa na watu wengine wenye mapenzi mema ya kumsaidia kupata matibabu.
Muumini mmoja, Grace Joram, alisema wananchi wote wenye mapenzi mema wanaombwa kumsaidia mtumishi huyo ili apatiwe matibabu kwani, anakabiliwa na tatizo hilo kwa wiki tatu sasa.
Joram alisema kabla ya kukumbwa na ugonjwa wa uti wa mgongo, Padri Mapunda alikuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za maombezi kwa waumini na wananchi, bila kujali dini wala kabila na kwamba, aliweza kusuluhisha migogoro mbalimbali ya wana ndoa.
"Jamani tumsaidieni Padri wetu kwani, amekuwa mtu mwema sana kwetu, maumivu aliyonayo sasa ni makali na anahitaji msaada wetu ili aweze kupata matibabu kumsaidia kupata matibabu kutamrejeshea tumaini jipya," alisema Grace.
Naye Jane Mbawala alisema ameguswa na tatizo hilo na ana imani wananchi na waumini wa kanisa hilo, watamsaidia kiongozi huyo fedha za matibabu na mahitaji mengine muhimu.
.
Alisema waumini wengi wameguswa na tatizo hilo kwani, licha ya kuonekana kuwa ni dhaifu na kuanguka mara tatu akitoa huduma ya kiroho Kanisa la Mateka, aliweza kuendelea kusaidia waumini hali ambayo iliwafanya kuguswa na jambo hilo.
Kwa upande wake, Padri Nicodems Luambano, aliwaomba waumini na watu wenye mapenzi mema kumsaidia mtumishi huyo ili aweze kupata matibabu.
Watakaoguswa wampigie simu au kutuma fedha kwenye namba 0713 33 17 22 na 0754 66 17 22