Padri Mapunda akerwa viongozi kukumbatia rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri Mapunda akerwa viongozi kukumbatia rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 1, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Viongozi nchini wametakiwa kumuiga Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye aliongoza nchi kwa misingi ya Azimio la Arusha badala ya kukumbatia rushwa na ufisadi unaowanufaisha baadhi ya walioko madarakani.

  Kadhalika, wametakiwa kuiga mfano wa Mwalimu Nyerere ambaye wakati wa uongozi wake, hakunyanyasa watu na alitaifisha hata shule zilizokuwa zinamilikiwa na Kanisa Katoliki ili watu wote wapate elimu sawa na kuwa wamoja bila kujali dini, itikadi, rangi wala kabila.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Farijika, Familia na Jamii Afrika Mashariki, Padre Baptiste Mapunda, wakati akiongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Manzese, jijini Dar es Salaam.
   
Loading...