Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Bora iendelee kubaki "Ndigo" kajifunze kwanza kuandika.Kwa taarifa yako Padre mmoja wa RC ni sawa na wachungaji na maaskofu 10 wa madhehebu mengine! Sasa aende huko kufuata nini?
hapo ndipo umethibitisha ninachosema 'IQ yako ndogo sn' ( yaani unaangalia vitu vidogo kwenye chapisho badala ya ku-ng'amua ujumbe mkuu kwenye chapisho) bado haujui kuwa kwenye typing kuna kitu kinaitwa"TYPING ERROR" elewa content chating ya JF sio mtihani wa kiswahili!!
 
Kuna brother wa kitaa Sengerema anaitwa Bosco Mosha (Maneno anaifahamu hii familia), kwasasa yupo Glasgow kule group la home huyu Padre ni classmate wake alisoma naye Uru Seminary, na akiwa Padre kabatiza watoto wa Bosco. Kweli ni Padre wa hilo shirika linalotajwa, sio Padre wa jimbo (kwa wakatoliki wanajua tofauti). Shirika lake lilimtuma South Sudan kutoa huduma ya kiroho na kule aliingizwa SPLA (Jeshi la Ukombozi la Sudani Kusini) na Garang. Then alipata basic training na kuwa Chaplain (mhudumu kiroho) kwenye Jeshi la South Sudan, vyeo hivyo alipandishwa hukohuko South Sudan, hopefully tunafahamu upandishwaji wa vyeo kwa SPLA ulikuwa wa mtindo gani, very politically kwa interest tofauti. Kwa taarifa za brother Bosco hata hizo uniform ni za South Sudan (SPLA). Ila hana uhakika wa cheo cha Meja, sio Komando ila anapenda kucheza Karate na Kung-fu kama part ya mchezo na kujiweka fit.
Elewa kua tumeshamjua Hana tabia za condition white
 
Huyu mkatoliki padri wa shirika mitume wa yesu yaani Apostles of Jesus (AJ) anaitwa Henry Rimisho pia ni lecturer hapo hapo Ardhi university

HONGERA, NI PADRI, COMMANDO, ENGINEER, LECTURER NK

Anaandika Brother Valerian Komu Valerian
____________
Komandoo wa JWTZ, Padre, Architect Henry Rumisho Mmsionary wa Apostles of Jesus; akiwa kwenye graduation pale Ardhi University Leo ambapo atatunukiwa PhD in Architecture.

Baadhi ya Mapadre wa Kanisa katoliki hujifunza na kuwa tayari kufanya kazi za kichungaji kwa askari walioko mstari wa Mbele vitani, wanajulikana kama Military Ordinariate, hufanya mazoezi na kupanda katika vyeo vya kijeshi sawa na wanajeshi wengine

Fr.Rumisho alihudumu uwanja wa vitani huko Dafour Sudan Nk.

Lakini pia Yeye ni Talented Comandoo, ana uwezo wa kufanya mazoezi magumu ya kikomandoo.

Ukiacha masomo yaliyomwezesha kuwa Padre, ana Bachelor degree, Masters, na leo anatunukiwa PhD zote za Architecture.

Pia ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya AQRB.

Lakini ni Lecturer..School of Architecture , Ardhi University.
Ana karama nyingi.

Cc castongo naomba mchango ktk hili nafahamu wewe ni mtaalamu zaidi
View attachment 2033006View attachment 2033007
View attachment 2033020View attachment 2033023
Nina wasiwasi na habari hizi... kwanza alivyovaa kofia Barrett. Utadhani ni mwizi. Hakuna cheo change nyota zaidi ya tatu, hii yake inaonysha kuvaa nyota zaidi nne. Halafu JWTZ awana beji yenye msalaba. Rangi ya kombati, ni tofauti na JWTZ.....
 
Nina wasiwasi na habari hizi... kwanza alivyovaa kofia Barrett. Utadhani ni mwizi. Hakuna cheo change nyota zaidi ya tatu, hii yake inaonysha kuvaa nyota zaidi nne. Halafu JWTZ awana beji yenye msalaba. Rangi ya kombati, ni tofauti na JWTZ.....
Sifa zote anazosifika nako sii zake na sio za kweli, sifa yake ya kweli ni Upadre pekee!!
 
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi niambia! Baadhi ya Ma Padre ni majasusi! Nimeanza kuamini hili suala! Ndiyo maana unakuta padre mzungu yuko vijijini ndani ndani kabisa huko,anaishi nyumba haina hata umeme,maji shida,usafiri shida, Mawasiliano ya simu shida! Lakini yuko na anaishi huko hata miaka 10

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kazi ya Padre ni kutangaza Injili. Yesu aliwaambia nendeni kila kona ya ulimwengu mkatangaze neno langu mkijua nipo nanyi mpaka ukamilisho wa dahari. Ndiyo maana kabla ya uhuru waliweza kwenda vijijini kusikokuwa na barabara wala umeme; hawajui lugha ya wananchi; na bado wakaishi miaka nenda rudi. Na hii si kwa Tanzania peke yake. Wengine walienda Bara la Asia na wengine Marekani ya kusini, n.k. Sasa ujasusi huko kijijini ni kwa manufaa yapi? Wengi wanaandika nikifa nizikwe hapa hapa. Na ndivyo inavyokuwa. Kijijini kwangu tu kuna wawili waliozikwa huko; Mholanzi na mwingine kuto Canada. Pia nawafahamu Wajeremani wawili waliozikwa kwenye kijiji kingine. Wote walifariki wakiwa na zaidi ya miaka 80 baada ya kuishi huko zaidi ya miaka 20. Tuwabambikie ujasusi eti tu kwa kuwa walikubali kuishi maisha ya taabu wakati walikuwa na fursa ya kuishi vinginevyo?
 
Nina wasiwasi na habari hizi... kwanza alivyovaa kofia Barrett. Utadhani ni mwizi. Hakuna cheo change nyota zaidi ya tatu, hii yake inaonysha kuvaa nyota zaidi nne. Halafu JWTZ awana beji yenye msalaba. Rangi ya kombati, ni tofauti na JWTZ.....
Hiyo jezi ni ya sudani kusini..
Kuhusu msalaba kazi vitani ya huduma za kiroho hivyo msalaba ni utambulisho wa ukristo wake
 
Nilitaka kumfananisha kidogo na Professor Mkude ambaye kipindi fulani aliwahi kuwepo UDSM. Huyu yeye alikuwa ni Padre halafu Profesa pia. Huyu jamaa hapa sasa naona amempiku hata Profesa Mkude

Mimi vile vile kwa upande wangu, nawa-admire sana watu ambao wana PhD za udaktari wa binadamu, halafu unakuta mtu huyo huyo tena ni Profesa. Mfano ni kama Profesa Mseru Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili. Hawa watu bongo zao Mungu aliziwekea kitu kingine cha ziada ambacho binadamu tulio wengi hatuna
 
Wana Jamii From!

Bila yakupoteza muda naomba kufahamu jambo moja zito ambalo kwa uelewa wangu nimeshindwa lipatia majibu!

Hivi inawezekana vipi Mtumishi wa Mungu Padre awe mwanajeshi tena komandoo??

Picha hapo chini ni Padre Henry,ambaye ni mwanajeshi komandoo,ambaye katunukiwa PhD yake ya Architecture!

😂😂😂 People like to get things twisted so much... Anyways huyo Padre sio commando Wala mwanajeshi... Ila alipata kuhudumu sehemu zenye machafuko ya kivita huko Sudani na alikua akitoa huduma za kiroho kwa wananchi na Wana jeshi wa eneo hilo kwa kifupi alikua chaplain. Sio commando Wala mwanajeshi na kama uliangalia interview yake vizuri utaona story yake yote ya Elimu na U padre lakini sio jeshini.... Na hata wakati wa mahafali yake alilazimika kuomba kibali jeshi limruhusu kuvaa hizo sare iwe ukumbusho kwake. 😂😂😂 Ila wa bongo sasa tunavyo twist vitu
 
😂😂😂 People like to get things twisted so much... Anyways huyo Padre sio commando Wala mwanajeshi... Ila alipata kuhudumu sehemu zenye machafuko ya kivita huko Sudani na alikua akitoa huduma za kiroho kwa wananchi na Wana jeshi wa eneo hilo kwa kifupi alikua chaplain. Sio commando Wala mwanajeshi na kama uliangalia interview yake vizuri utaona story yake yote ya Elimu na U padre lakini sio jeshini.... Na hata wakati wa mahafali yake alilazimika kuomba kibali jeshi limruhusu kuvaa hizo sare iwe ukumbusho kwake. 😂😂😂 Ila wa bongo sasa tunavyo twist vitu
Mkuu mbona kuna clip inamwonyesha akicheza na cheni mithili ya bruce lee.
 
People like to get things twisted so much... Anyways huyo Padre sio commando Wala mwanajeshi... Ila alipata kuhudumu sehemu zenye machafuko ya kivita huko Sudani na alikua akitoa huduma za kiroho kwa wananchi na Wana jeshi wa eneo hilo kwa kifupi alikua chaplain. Sio commando Wala mwanajeshi na kama uliangalia interview yake vizuri utaona story yake yote ya Elimu na U padre lakini sio jeshini.... Na hata wakati wa mahafali yake alilazimika kuomba kibali jeshi limruhusu kuvaa hizo sare iwe ukumbusho kwake. Ila wa bongo sasa tunavyo twist vitu
Hii imekaaje?
Screenshot_20220330-034249.jpg
 
Back
Top Bottom