Padri anayedaiwa kulawiti kortini .................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Padri anayedaiwa kulawiti kortini
Monday, 06 December 2010 21:56

Daniel Mjema, Moshi
HATIMAYE Padri Stanslaus Msafiri Salla (70) wa Parokia ya Kilema ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 16.

Padre Salla ambaye alipelekwa mahakamani jana kwa njia ambayo polisi walisema ni ya “kistaarabu”, aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waliomdhamini kwa Sh10 milioni kila mmoja.
Ingawaje hati ya mashtaka iliwasilishwa kortini na polisi saa 3:00 asubuhi na kufunguliwa na kupewa namba 743/2010, lakini padre huyo alifika mahakamani hapo saa 5:30 kwa mazingira yaliyoibua maswali mengi kuliko majibu.
Mshtakiwa huyo aliingia mwenyewe jengo la mahakama na polisi mwenye cheo cha Koplo namba 5397, alimwelekeza asiingie mahabusu bali aende moja kwa moja kukaa kwenye benchi la hakimu aliyepangiwa kesi hiyo.
Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili wa Serikali, Abdallah Chavulla, alidai mahakamani kuwa, Oktoba 30, mwaka huu majira ya usiku eneo la Kilema Leso, Padre huyo alimuingia kinyume cha maumbile kijana mwenye umri wa miaka 16.

Alidai kuwa, kitendo kilichofanywa na Padre huyo kilikuwa ni kosa chini ya kifungu namba 154 (1) (a) cha sura namba 16 cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marekebisho na Bunge mwaka 2002.

Chini ya kanuni hiyo, anayepatikana na hatia atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela isipokuwa kama mshtakiwa atakuwa amemfanyia kitendo hicho mtoto chini ya miaka 10 basi, adhabu yake ni kifungo cha maisha.
Hakimu Mkazi Mfawadhi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, alisema dhamana ya mshtakiwa huyo ilikuwa wazi na ndugu waliojitokeza mahakamani hapo wakiwamo baadhi ya mapadre, walifanikiwa kutimiza masharti hayo.

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, amekanusha kumlinda kwa namna yoyote mtuhumiwa huyo akisema hapaswi kunyooshewa kidole kwani, yeye ni mtawala sio mpelelezi wa makosa ya jinai.
“Naambiwa natumia ukatoliki wangu kumlinda Padre, kwanza mimi ni mtawala tu sio mpelelezi,” alisema Kamanda Ng’hoboko na kuongeza kuwa, uandaaji mashtaka sasa unafanywa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ng’hoboko alifafanua kuwa, taarifa kwamba fomu ya polisi (PF3) iliyopelekwa kwa mwanasheria wa serikali sio halisi, amezisoma kwenye vyombo vya habari na kuwataka wenye nakala halisi kuiwasilisha kwake ifanyiwe kazi.
 
Padri 'mlawiti' atinga kizimbani
• Akana kosa, adhaminiwa kwa mil.20/-

na Charles Ndagulla, Moshi


amka2.gif
PADRI Stanslaus Salla wa Parokia ya Mtakatifu, Theresa Lego Muro, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za kumlawiti kijana wa miaka 16. Padri huyo alipandishwa kizimbani saa 8 mchana chini ya ulinzi mkali wa polisi ambapo alisomewa tuhuma zake na Wakili wa Serikali Abdallah Chagula, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Simon Kobero.
Katika kesi hiyo CC namba 743/2010 mtuhumiwa huyo alikabiliwa na makosa mawili; ilidaiwa kwamba Oktoba 30 mwaka huu usiku, maeneo ya Kilema Leso wilaya ya Moshi Vijijini, mtuhumiwa huyo alikula njama kwa nia ya kutenda kosa hilo.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa na kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 10 mwakani itakapotajwa tena kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.
Hata hivyo, Mahakama hiyo ilimwachia kwa dhamana mtuhumiwa huyo baada ya kutimiza masharti ambayo ni wadhamini wawili waliosaini dhamana yenye thamani ya sh milioni 10 kila mmoja.
Kwa upande wake, wakili wa serikali alionyesha kutilia shaka uwezo wa wadhamini na kuitaka mahakama hiyo ijiridhishe juu ya uwezo wa kifedha wa wadhamini hao ili kuepusha uwezekano wa mshtakiwa kuruka dhamana aliyopewa.
Licha ya kuachiwa kwa dhamana, askari na ndugu wa padri huyo walishirikiana kumtoa kwa siri nje ya mahakama mtuhumiwa huyo huku maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake waliofurika kwenye viwanja vya mahakama kushindwa kumwona.
Aidha, kabla ya Padri huyo kupandishwa kizimbani, kulitokea vituko kadhaa kikiwemo cha polisi wanaodaiwa kupewa maagizo maalum kugoma kumuweka mshtakiwa kwenye chumba cha mahubusu cha mahakama hiyo kama ilivyo kwa washtakiwa wengine wa makosa ya jinai.
Kitendo hicho kilionekana kuwakera baadhi ya watu waliofika mahakamani hapo waliosema kuwa mtuhumiwa huyo hakupaswa kunyenyekewa na kulindwa kiasi hicho.
 
ana miaka 70? kama ni kweli atakua ameshapitia wangapi tangu ujana wake?
 
From PETER TEMBA in Moshi, 6th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 202

A CATHOLIC priest on Monday appeared before a magistrate’s court here charged with committing unnatural offence (sodomy) on a 16-year-old boy.

The accused Stanslaus Salla (60), pleaded “not guilty” before Resident Magistrate Simon
Kobero and is out on a 10m/- bail.

Prosecuting, State Attorney, Abdallah Chagula, said the accused allegedly committed
the offence on October 30, at Kilema Lasso area.

The court adjourned the case to January 10, next year, for another mention. The accused was, however, accorded special treatment before he appeared in court.

He did not come in a police truck like other suspects and was also not kept in the court’s lock-up facility.
 
basi akina malaria sugu wanazipenda kweli mada za hivi...
 
Nadhani ni vizuri kama sheria itachukua mkondo wake, tuwape muda wapelelezi wafanye kazi yao kwa umakini mkubwa ili hatima iweze patikana. Tuombe Mungu atuonyeshe njia ya kweli, kwani kama mchunga kondoo anakula anaowachunga basi tunakoelekea siko!!??!!
 
ana miaka 70? kama ni kweli atakua ameshapitia wangapi tangu ujana wake?

We acha tu mkuu kuna mambo mengi sana hatujui haya ni yale ya bahati mbaya tu ila kama angewin huyu jamaa mpaka angemaliza umri wake wa kuishi hapa duniani watu wasingejua uovu wake. Kuna taarifa leo nimeiona kuwa Kanisa limewafukuza waumini wake eti baada ya kuwakashifu viongozi wa dini kuwa watoto waliojazana mitaani ni watoto wa mapadre. Ifike wakati sasa Kanisa liruhusu mapadre kuoa ili kukomesha tabia za mapadri kula kiboga.
 

Attachments

  • SeminariansKissing2.jpg
    SeminariansKissing2.jpg
    5.7 KB · Views: 57
Back
Top Bottom