Padri alishukia Bunge, serikali | Adai nchi inaelekea kubaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri alishukia Bunge, serikali | Adai nchi inaelekea kubaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 23, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]  • [*=1]
   Speaker, Naibu na wenyeviti bungeni wanatabia ya kuwapendelea wabunge wa CCM

   [*=1]
   Speaker, Naibu na wenyeviti wanawakandamiza wabunge wa upinzani

   [*=1]
   Bunge sasa ni Chuo Kikuu cha matusi

   [*=1]
   Ufisadi sasa imegeuzwa taaluma ya ajira serikalini

  Spika Makinda, Ndugai walipuliwa

  Padri Baptiste Mapunda wa Kanisa Katoliki Tanzania amewataka Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu wake, John Ndugai na wenyeviti kuacha tabia ya kuwapendelea wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwakandamiza wa upinzani wakati wa vikao, hali ambayo imesababisha Bunge kuwa chuo kikuu cha matusi na kuhatarisha mustakabari wa usalama wa nchi.

  Aidha, amesema hivi sasa nchi imejaa ufisadi ambao sasa imekuwa kama taaluma ambayo watu wanakweda kuisomea ili wanapoingia madarakani wajichotee fedha huku Watanzania wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa.

  Padri Mapunda alitoa kauli hiyo jana wakati akihubiri katika misa ya Jumapili kwenye Parokia ya Manzese ya Kanisa Katoliki jijini Dar es Salaam.

  "Taifa limefika mahali pabaya sana, hivi sasa chuo kikuu cha matusi kimekuwa ni bungeni na kimsingi hayo yoye yanasababishwa na Spika na wasaidizi wake ambao wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa CCM," alisema Mapunda na Padri Mapunda ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Faidika Afrika Mashariki.

  Huku akishangiliwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo, Padri Mapunda alisema wakati wa uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere nchi ilikuwa na heshima na amani, lakini hivi sasa wameingia madarakani viongozi wasio na maadili mema ambao wamepandikiza virusi na kuifanya nchi isiwe na amani.

  Alisema viongozi wengi wa serikali wamekuwa mstari wa mbele kuhubiria amani, lakini wanasahau kutenda haki kwani nchi isiyokuwa na umoja ni hatari kwa usalama.

  "Nyerere alikuwa nabii na mchungaji mwema aliyeweza kufanikisha kuyaunganisha makabila 120 nchini ambapo nchi kipindi hicho ilikuwa na amani, lakini leo hii wamekuja watu wamepandikiza virusi na sasa nchi haina amani kila siku ni matukio mabaya," alisema Padri Mapunda.

  Alivishutumu vyombo vya usalama kuwa kimsingi vimeshindwa kulinda usalama wa wananchi hali ambayo imesababisha kuwepo kwa maovu mengi na kusababisha watu kuishi kwa hofu.

  Alisema kwa mfano tukio la kutekwa na kuteswa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, vyombo vya dola vimeonyesha udhaifu mkubwa sana kwa kushindwa kuwakamata wahusika wakuu wa tukio hilo na ndiyo maana kumekuwa na uongo mwingi sana unaofanywa viongozi wa Jeshi la Polisi na Serikali kwa lengo la kuficha ukweli.

  "Manyanyaso katika nchi yetu yamekuwa mengi sana kwa mfano Dk. Ulimboka kutekwa na kung'olewa meno na kucha ni hatari, mimi nitaendelea kumuombea Dk. Ulimboka apone arudi hapa nchini ili aje amwage ukweli hapa wa tukio hilo," alisema Mapunda.
  "Serikali ya CCM ihakikishe wananchi wanakuwa salama, lakini kwa sasa Tanzania siyo salama, Jeshi la Polisi linaonyesha upendeleo katika utendaji wake wa kazi, kimsingi tumefika pabaya miaka 50 tangu uhuru, tunahitaji manabii wa kuiongoza nchi," alisema Padre Mapunda.

  KUHUSU AJALI

  Padri Mapunda alisema Tanzania imekuwa kama nchi ya majanga ambayo kila siku ajali za barabarani, majini na angani zimekuwa zikitawala na kuongezeka kuwa hali hiyo ni matokeo ya kushindwa kwa waliopewa madaraka ya kusimamia maeneo hayo.

 2. K

  Konya JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  amenena vema,hii nchi inahitaji maombi..GOD BLESS TZ
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Haya,,,,nadhan ni yaleyale tunayoyaaandika hapa kila kukicha........
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Subiri kauli reja reja kutoka kwa Mwigulu camp.wanajipange watoke vipi kama ulivyo agiza waraka wake kwa watu wote!:loco:
   
 5. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Bibi kiroboto haisikii la mtu
   
 6. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  This is the bitter truth, He is a man of GOD I congratulate him to air out the truth.Message sent and as days go,CCM are dragging themselves to HELL..Sleeping Tanzanians are awake,Closed Minds are Opened and really CCM days are decreasing sequentially!!

  Even my dead body wont support MAGAMBA'S Party!!
   
 7. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba hawakawii kusema chama fulani kipo nyuma ya mtumishi huyu mkweli wa mungu
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Fr. Mapunda hana woga, ana sauti ya kinabii.
   
 9. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Na Mwandishi wetu

  [​IMG]

  Padri Baptiste Mapunda wa Kanisa Katoliki Tanzania amewataka Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu wake, John Ndugai na wenyeviti kuacha tabia ya kuwapendelea wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwakandamiza wa upinzani wakati wa vikao, hali ambayo imesababisha Bunge kuwa chuo kikuu cha matusi na kuhatarisha mustakabari wa usalama wa nchi.

  Aidha, amesema hivi sasa nchi imejaa ufisadi ambao sasa imekuwa kama taaluma ambayo watu wanakweda kuisomea ili wanapoingia madarakani wajichotee fedha huku Watanzania wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa.

  Padri Mapunda alitoa kauli hiyo jana wakati akihubiri katika misa ya Jumapili kwenye Parokia ya Manzese ya Kanisa Katoliki jijini Dar es Salaam.

  "Taifa limefika mahali pabaya sana, hivi sasa chuo kikuu cha matusi kimekuwa ni bungeni na kimsingi hayo yoye yanasababishwa na Spika na wasaidizi wake ambao wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa CCM," alisema Mapunda na Padri Mapunda ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Faidika Afrika Mashariki.

  Huku akishangiliwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo, Padri Mapunda alisema wakati wa uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere nchi ilikuwa na heshima na amani, lakini hivi sasa wameingia madarakani viongozi wasio na maadili mema ambao wamepandikiza virusi na kuifanya nchi isiwe na amani.

  Alisema viongozi wengi wa serikali wamekuwa mstari wa mbele kuhubiria amani, lakini wanasahau kutenda haki kwani nchi isiyokuwa na umoja ni hatari kwa usalama.

  "Nyerere alikuwa nabii na mchungaji mwema aliyeweza kufanikisha kuyaunganisha makabila 120 nchini ambapo nchi kipindi hicho ilikuwa na amani, lakini leo hii wamekuja watu wamepandikiza virusi na sasa nchi haina amani kila siku ni matukio mabaya," alisema Padri Mapunda.

  Alivishutumu vyombo vya usalama kuwa kimsingi vimeshindwa kulinda usalama wa wananchi hali ambayo imesababisha kuwepo kwa maovu mengi na kusababisha watu kuishi kwa hofu.

  Alisema kwa mfano tukio la kutekwa na kuteswa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, vyombo vya dola vimeonyesha udhaifu mkubwa sana kwa kushindwa kuwakamata wahusika wakuu wa tukio hilo na ndiyo maana kumekuwa na uongo mwingi sana unaofanywa viongozi wa Jeshi la Polisi na Serikali kwa lengo la kuficha ukweli.

  "Manyanyaso katika nchi yetu yamekuwa mengi sana kwa mfano Dk. Ulimboka kutekwa na kung'olewa meno na kucha ni hatari, mimi nitaendelea kumuombea Dk. Ulimboka apone arudi hapa nchini ili aje amwage ukweli hapa wa tukio hilo," alisema Mapunda.
  "Serikali ya CCM ihakikishe wananchi wanakuwa salama, lakini kwa sasa Tanzania siyo salama, Jeshi la Polisi linaonyesha upendeleo katika utendaji wake wa kazi, kimsingi tumefika pabaya miaka 50 tangu uhuru, tunahitaji manabii wa kuiongoza nchi," alisema Padre Mapunda.

  KUHUSU AJALI

  Padri Mapunda alisema Tanzania imekuwa kama nchi ya majanga ambayo kila siku ajali za barabarani, majini na angani zimekuwa zikitawala na kuongezeka kuwa hali hiyo ni matokeo ya kushindwa kwa waliopewa madaraka ya kusimamia maeneo hayo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 10. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dah!!Nabii kapasua jipu...heko sana viongozi pigeni kelele mpaka kieleweke!!!
   
 11. m

  markj JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kweli huyo jamaa ni nabii?
   
 12. m

  markj JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  nchi sio inakokwenda ni kubaya! hii nchi ilishakwenda kubaya,sema sasa ivi ndo wanakazia tu! wakati wote huo walikuwa wapi hawa viongozi wa dini,nao wamepewa ufunuo wakuona muelekeo fulani, na muelekeo wa nchi kwenda pabaya si sasa tu! miaka ya nyuma na mpaka sasa ndo tuko pabaya na si tunaelekea kubaya, bali tupo pabaya!
   
 13. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi utasikia wanakuja hapa na michango uchwara ya kujadiri mtoa hoja badala ya hoja, kwasasa ngoja ni pumzike kwanza!
   
 14. m

  markj JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hawa hawa viongozi wadini ndo huwa wanawapa chaapuo na walikuwa wakiwapa chapuo hawa viongozi ambao sasa wanasema ni wabovu! Je hawakuliona hilo mapema! Wakalizima haya yote yasingetokea au yasingekuwa ya kiwango ichi! Wao ndo wakwanza kwenda kuuza sura ikulu wakiitwa kidogo tu au hata wasiitwe wantatafuta jinsi!

  By the way mi naona hata hawa viongozi wadini wamechangia hii nchi kufika hapa pabaya na si kwenda pabaya! mana wao ndo walikuwa wamewakumbatia hawa viongozi na kuwabebabeba kwenye makampeni hasa nyumba za ibada!

  Leo wanajifanya nchi inakwenda kubaya! inakwenda kubaya barangapi! wakati tayari iko kubaya tu!
   
 15. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hongera.............. Hata kwa Wakristu, naamini hata waislam ni sehemu ya majukumu yao kuionya serikali pale mambo yanapoharibika. Lakini kutokana na hofu iliyojengwa na dola, ni viongozi wachache sana wenye huu ujasiri.
   
 16. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  ndio maana hakuna padre form six leaver! walikwenda shule, tena shule inayooleweka! wanaweza sasa kutoa hoja za msingi!
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Angalia na hizi:
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/296347-sheikh-khalifa-bunge-limeoza-spika-sio-makini-ni-dhaifu.html

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/282946-padre-aitaka-ccm-ijiandae-kuondoka%3B-adai-yuko-tayari-kupigwa-risasi-akisema-ukweli.html

  Hii nchi inaelekea wapi? Masheikh na Mapdre wanaisakama serikali na upinzani. Hawa ni waokozi wetu roho zetu au waokozi wa nchi yetu?

  Nashauri tu, ili kazi yao iwe na mashiko, watoke kwenye madhebahu na mimbari zao wajiunge na siasa - Rukhsa, sio watupe madongo wakiwa nje wakija wakinyukwa waanze kulalama.
   
 18. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  after form ni 3yrs of philosophy then 4yrs of theology
   
 19. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  “Lazima viongozi wazembe tuwaseme, sisi ni mwanga wa kuwasha watu wanaofanya ufisadi na ukandamizaji haki za binadamu japo utasikia baadhi ya watu na magazeti wakisema Padri Mapunda aliutoa wapi unabii...mimi nimepewa na Mungu kupitia Baba Askofu, sitaacha kusema hata wakinipiga mawe,” alisema
  Nimenukuu hapo kwenye red mkuu....
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
Loading...