Uchaguzi 2020 Padre wa Kanisa Katoliki aliyeomba Ubunge huko Kagera kupitia CCM asimamishwa rasmi kuendelea na wito

RC wameonesha mfano.......Gwajima ni jeshi la mtu mmoja hakuna wa kumsema taasisi kaanzisha mwenyewe na anasimamia mwenyewe
 
Hauko sahihi ndugu. Anabaki kuwa kardinali mpaka kifo. Nchi moja inaweza kuwa na makardinali zaidi ya mmoja. Italia inao labda zaidi ya 50. Brazil inao wengi pia nk. pia kuna nchi haxzina kardinali hata mmoja.
 
Mbona barua inasema aliacha kazi kwa hiari yake mwenyewe. Habari ya kufukuzwa inakuja vipi. Mara nyingine muache kujitoa ufahamu nyie nyumbu. Hiyo kimsingi ni barua ya taarifa na kuthibitisha jamaa kuacha kazi. Pia kila mty anao uhuru wa kuishi atakavyo. Hata kadinali anaweza kuamua kubadilisha mwelekeo wa maisha yake.
Hapo barua imeandikwa ili kuweka kumbukumbu sawa,je siku akirudi akiikana barua ya kuacha Upadre huoni Askofu ataonekana alikuwa na lake jambo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee sikujua kama pia wapo mapadre wa catholic, kanisa lenye heshima naye alitaka kwenda bungeni. Shame on you maccm!

Haya amefukuzwa aende vizuri huko CCM
View attachment 1523939

Kumbe principle ni hiyo hiyo hata makanisani.ukiacha kazi uliyoitiwa na kutaka kazi nyingine unahesabika ni mtu asiyetosheka,hivyo unatumbuliwa right away

Sababu padre alitakiwa kubaki kuuombea uchaguzi uende salama ila asigombee ubunge sababu tutakosa waombaji
 
Tanzania haina Kadinali bado. Ruwaichi ni Askofu mkuu. Pia bado Pengo hajaagwa kwa misa takatifu!
Hauko sahihi ndugu. Anabaki kuwa kardinali mpaka kifo. Nchi moja inaweza kuwa na makardinali zaidi ya mmoja. Italia inao labda zaidi ya 50. Brazil inao wengi pia nk. pia kuna nchi haxzina kardinali hata mmoja.
 
Ukiwa askofu mkuu wa jimbo katoliki dar lazima uwe cardinal refer kwa cardinal aliyepita kabla ya pengo
Kitu kama haukijui KAA KIMYA, ukiwa Askofu mkuu Jimbo la Dar es salaam SIO LAZIMA UWE KADINALI, kwani huyo Askofu Mkuu wa sasa ni Cardinal? Mbona Baba mtakatifu amemteua kuwa Askofu mkuu Jimbo la Dar? Sio lazima awe Cardinal ila lazima awe Askofu, japo hao waliopita walikua ma Cardinal
 
Mbona barua inasema aliacha kazi kwa hiari yake mwenyewe. Habari ya kufukuzwa inakuja vipi. Mara nyingine muache kujitoa ufahamu nyie nyumbu. Hiyo kimsingi ni barua ya taarifa na kuthibitisha jamaa kuacha kazi. Pia kila mty anao uhuru wa kuishi atakavyo. Hata kadinali anaweza kuamua kubadilisha mwelekeo wa maisha yake.
Mkuu ukisha kuwa kiongozi au mtumishi wa kidini huwezi tena kuishi vile utakavyo..!!
 
Ukisoma barua vizuri kulichomsimamisha sio kwenda kugombea. Ni kutoka kituoni kwake bila ruhusa. Na hilo ni kosa kubwa kwa maadili ya kipadre.
Kuna mapadri wamewahi kuwa viongozi sehemu mbalimbali hapa.nchini na duniani lakini hawakusimamishwa.
Padri Kiwanga miaka wa 70 alikuwa mbunge Dodoma na akaendelea kuhudumia kanisani. Maelezo ya kwenda kugombea ni ya nyingeza tu
Miaka ya 80 mwishoni kuna padri alikuwa dean wa faculty pale UDSM na alikuwa anasoma misa kama kawaida.
Kuna mapdri walimu wengi tu vyuoni na mashuleni.
Suala ni uombe kwa askofu wako na akukubalie.
Huyu alitoka kwenye kituo chake cha kazi, hilo halikubaliki kabisa.
 
Mbona unaleta mambo ya miaka ambayo wengi humu walikuwa hawajazaliwa? Askofu amenukuu kanisa na canon law inayozuia mtiwa mafuta wa Bwana kushika nafasi ya kisiasa. Ina maana huo msitari kwenye barua hukuuona?
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom