Uchaguzi 2020 Padre wa Kanisa Katoliki aliyeomba Ubunge huko Kagera kupitia CCM asimamishwa rasmi kuendelea na wito

Kama barua hii ni halali basi nyie katoliki mko smart sana. Hata hivyo baada ya kupitia maandiko ya kikatoliki, huyu padre atakuwa na cheo cha Mlei. Na kazi za walei ni zile zile za kitume nje ya kanisa.

Akifanya kazi zake za kitume vizuri huko makazini hupewa cheo na kuwa Mtakatifu. Hakika katoliki wako smart sana. Nawapongeza.
 
Msigwa akigombea ubunge kupitia CHADEMA hakuna shida lakini kasisi wa katoliki akigombea ubunge hasa kupitia CCM ni tatizo kubwa.
Huyo kasisi kaandika barua ya kuomba kuachana n kutoa huduma kama kasisi kisha kaenda kugombea hii haina tofauti na alivyofanya Dr. Wilbroad Slaa.

Siyo habari ya kushika akili za watu majukwaani.
 
Nimeona mkuu wangu.
Ahsante kwa kunistua.
Mkuu, kwa itifaki za kanisa kile ni cheo chake na atakufa nacho. Papa alipostaafu aliendelea kuwa na hadhi ya upapa isipokuwa tu hafanyi misa takatifu. Kumu address Pengo wala hakuna shida.
 
Msigwa akigombea ubunge kupitia CHADEMA hakuna shida lakini kasisi wa katoliki akigombea ubunge hasa kupitia CCM ni tatizo kubwa.
Huyo kasisi kaandika barua ya kuomba kuachana n kutoa huduma kama kasisi kisha kaenda kugombea hii haina tofauti na alivyofanya Dr. Wilbroad Slaa.

Siyo habari ya kushika akili za watu majukwaani.
Kasisi hata angegombea kupitia Chadema angesimamishwa tu. Hawaruhusiwi kabisa kuwa wanasiasa na hata Magufuli akisimama pale madhabahuni hawezi kamwe kutoa maamuzi ya kiuongozi akiwa pale zaidi ya kuongea tu kama muumini wa kawaida.
 
Mbona barua inasema aliacha kazi kwa hiari yake mwenyewe. Habari ya kufukuzwa inakuja vipi. Mara nyingine muache kujitoa ufahamu nyie nyumbu. Hiyo kimsingi ni barua ya taarifa na kuthibitisha jamaa kuacha kazi. Pia kila mty anao uhuru wa kuishi atakavyo. Hata kadinali anaweza kuamua kubadilisha mwelekeo wa maisha yake.
Hakujibiwa hiyo barua, maana Askofu pengine alihitaji kumsikia vizuri hoja zake katika mazungumzo. Lakini kwa kuwa kugombea nafasi za kisiasa ni jambo la hadharani, hilo ndilo limemfanya Askofu aandike barua ya kumsimamisha huduma, maana lipodhahiri zaidi kuliko barua ya Padre
 
Back
Top Bottom