Uchaguzi 2020 Padre wa Kanisa Katoliki aliyeomba Ubunge huko Kagera kupitia CCM asimamishwa rasmi kuendelea na wito

Hii barua ni ya uongo cardinal pengo Alisha staafu kwa Sasa cardinali ni Rwaichi Kama sijakosea
[/QUOTERuwaichi siyo cardinal ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la DaM,cardinal ni pengo amestaafu majukumua ya uaskofu lakini siyo u cardinal
 
Ukisoma barua vizuri kulichomsimamisha sio kwenda kugombea. Ni kutoka kituoni kwake bila ruhusa. Na hilo ni kosa kubwa kwa maadili ya kipadre.
Kuna mapadri wamewahi kuwa viongozi sehemu mbalimbali hapa.nchini na duniani lakini hawakusimamishwa.
Padri Kiwanga miaka wa 70 alikuwa mbunge Dodoma na akaendelea kuhudumia kanisani. Maelezo ya kwenda kugombea ni ya nyingeza tu
Miaka ya 80 mwishoni kuna padri alikuwa dean wa faculty pale UDSM na alikuwa anasoma misa kama kawaida.
Kuna mapdri walimu wengi tu vyuoni na mashuleni.
Suala ni uombe kwa askofu wako na akukubalie.
Huyu alitoka kwenye kituo chake cha kazi, hilo halikubaliki kabisa.
Asante kwa kunikumbusha kuhusu huyo padri wa UDSM, Rev Fr Dr Daniel Mkude, alinifundisha mlimani miaka hiyo. Baadaye alipanda vyeo vya kitaaluma hadi akawa profesa na amefundisha linguistics kwa miaka mingi Mlimani.
 
Aisee sikujua kama pia wapo mapadre wa catholic, kanisa lenye heshima naye alitaka kwenda bungeni. Shame on you maccm!

Haya amefukuzwa aende vizuri huko CCM.

Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu nzuri. Dr Slaa aliacha Upadre Katoliki, akawa Katibu Mkuu CHADEMA na kuoa.

Mnapodai Haki na Uhuru, mwe tayari kuheshimu maamuzi ya watu wengine na si kila jambo mlichukue kisiasa. AIBU
 
Tanzania haina Kadinali bado. Ruwaichi ni Askofu mkuu. Pia bado Pengo hajaagwa kwa misa takatifu!
Kwanza hakuna sheria inayosema kila nchi ni lazima iwe na kadinali. Rugambwa miaka ya mwanzoni alikuwa kadinali pekee kutoka bara la Afrika. Kadinali ni mjumbe wa baraza la Papa, wala hawakilishi nchi. Ndiyo maana makadinali wote ni raia wa Vatican.

Ili kadinali iweze kushiriki kwenye mabaraza ya nchi, mara nyingi Papa humpa pia cheo cha Askofu wa jimbo. Kwa kupitia nafasi ya Askofu wa jimbo, anakuwa mjumbe wa Baraza la Maaskofu kwenye nchi husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma barua vizuri kulichomsimamisha sio kwenda kugombea. Ni kutoka kituoni kwake bila ruhusa. Na hilo ni kosa kubwa kwa maadili ya kipadre.
Kuna mapadri wamewahi kuwa viongozi sehemu mbalimbali hapa.nchini na duniani lakini hawakusimamishwa.
Padri Kiwanga miaka wa 70 alikuwa mbunge Dodoma na akaendelea kuhudumia kanisani. Maelezo ya kwenda kugombea ni ya nyingeza tu
Miaka ya 80 mwishoni kuna padri alikuwa dean wa faculty pale UDSM na alikuwa anasoma misa kama kawaida.
Kuna mapdri walimu wengi tu vyuoni na mashuleni.
Suala ni uombe kwa askofu wako na akukubalie.
Huyu alitoka kwenye kituo chake cha kazi, hilo halikubaliki kabisa.
Inawezekana kuna kitu unakikosa katika uelewa. Ukweli ni kuwa:

1) watu wenye daraja takatifu ndani ya Kanusa Catholic hawaruhusiwi kushika nafasi za kisiasa

2) Watu wenye madaraja matakatifu wanaruhusiwa kufanya shughuli za utumishi wa huduma kama vile kufundisha, kutibu, ufundi, n.k.

3) Kuna watu waliwahi kuwa wabunge ambao mwanzoni walikuwa mapadre. Lakini hakuna aliyewahi kuwa mbunge na akaendelea kutoa huduma ya kipadre ndani ya kanisa

4) Padre au mtawa kuwa daktari, mwalimu, mhandisi, mhasibu, ni ruksa lakini siyo kuwa DC, mbunge, RC, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom