Padre Recardo Maria "Padri pekupeku"

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
Kwetu Tanzania,Walau tunaye Padre Recardo Maria...huyu ni Mtawa wa shirika la Fransiscani la Ndugu Wadogo,Padre Recardo maarufu kama "pekupeku" alianza safari yake ya Utume huko Jimbo la Iringa ktk Kijiji cha Izazi Parokia ya Isimani,baadae akahama na kuweka "Nyumba ya Kitawa" mkoani Morogoro.Ni mtu anayetoka ktk familia ya kitajiri huko kwao Italy,lakini aliamua kuacha maisha ya kwao na kuja kutoa utume barani Afrika/

Padre Recardo Maria anasifika kwa kuishi maisha ya "ufukara" na unyenyekevu,akiwasaidia watu wa dini na rika zote ktk shida mbalimbali,ameanzisha shule ktk mji wa Morogoro na kusomesha vijana wengi wasio na uwezo.Pia amefungua kituo cha Radio Huruma ktk mji wa Morogoro.

Padre Pekupeku kwa "ufukara" wake hulala chini kama ishara ya majitoleo yake,havai viatu wala kutumia usafiri wa gari ktk mizunguko yake zaidi ya baiskeli,katika umbali mdogo Pd.Recardo hutembea,kwa walioishi naye maeneo ya Iringa na Morogoro wameshuhudi kuwa ana uwezo wa kutembea zaidi ya kilomita kumi hadi ishirini kwa mguu

Maisha ya Pd.Recardo yamejaa "ufukara" na "unyenyekevu". Amesomesha vijana wengi sana ktk miji ya Iringa na Morogoro.Amejitolea kwa mambo mengi.Bado kuhusu usafi na uchaji wake kwa Mungu ni Muumba mwenyewe ndio anaejua,lakini kwa macho ya kibinadamu amefanya kazi yake
Hongera Pd.Pekupeku...
ImageUploadedByJamiiForums1464380643.681243.jpg
 
Naona huyu ni tofauti na yule wa Pomern Kule wilayani Kilolo. Naye kafanya kazi kubwa sana pande zile za Kilolo. Anatembea peku maisha yake yote.
Yule ni shemasi wa kudumu,Anaitwa Shemasi Paul,anaishi Pomelini kwa miaka mingi
 
Kwetu Tanzania,Walau tunaye Padre Recardo Maria...huyu ni Mtawa wa shirika la Fransiscani la Ndugu Wadogo,Padre Recardo maarufu kama "pekupeku" alianza safari yake ya Utume huko Jimbo la Iringa ktk Kijiji cha Izazi Parokia ya Isimani,baadae akahama na kuweka "Nyumba ya Kitawa" mkoani Morogoro.Ni mtu anayetoka ktk familia ya kitajiri huko kwao Italy,lakini aliamua kuacha maisha ya kwao na kuja kutoa utume barani Afrika/

Padre Recardo Maria anasifika kwa kuishi maisha ya "ufukara" na unyenyekevu,akiwasaidia watu wa dini na rika zote ktk shida mbalimbali,ameanzisha shule ktk mji wa Morogoro na kusomesha vijana wengi wasio na uwezo.Pia amefungua kituo cha Radio Huruma ktk mji wa Morogoro.

Padre Pekupeku kwa "ufukara" wake hulala chini kama ishara ya majitoleo yake,havai viatu wala kutumia usafiri wa gari ktk mizunguko yake zaidi ya baiskeli,katika umbali mdogo Pd.Recardo hutembea,kwa walioishi naye maeneo ya Iringa na Morogoro wameshuhudi kuwa ana uwezo wa kutembea zaidi ya kilomita kumi hadi ishirini kwa mguu

Maisha ya Pd.Recardo yamejaa "ufukara" na "unyenyekevu". Amesomesha vijana wengi sana ktk miji ya Iringa na Morogoro.Amejitolea kwa mambo mengi.Bado kuhusu usafi na uchaji wake kwa Mungu ni Muumba mwenyewe ndio anaejua,lakini kwa macho ya kibinadamu amefanya kazi yake
Hongera Pd.Pekupeku...
View attachment 351540

Kutana na Padre Pekupeku na Sir mwenye miujiza,ilishaletwa humu JF
 
Anajitahidi kuishi kama karama ya shirika lake ilivyo, maisha ya ufukara kama mt Francisco wa Asiz, Zamani nilitaka kuwa mtawa wa shirika hilo.
 
Watu wa Isimani Idodi na Pawaga hawawezi kumsahau huyu padre amefanya mengi kule walimwekea mizengwe ndia akahamia Morogoro.. Kuna ile shule ya Serikali Nyerere yenye mpaka advance level kule Migori( mtera) aliamua kuiachia.. Huwa hapo morogoro safari zake ni baiskeli
 
Back
Top Bottom