TANZIA Padre Paul Ignas Shewiyo wa Kanisa la Msimbazi afariki Dunia

fisi 2

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
3,273
4,626
Padri Shewiyo alikua kanisa ka Msimbazi. Amefariki mchana huu hapa Bochi Hospitali .

====

1612515587153.png


TANZIA: Mkuu wa Shirika la Ndugu Wafransisko Wakapuchini Tanzania, Padre, Kalist Tesha, anatangaza kifo cha Padre Paul Ignas Shewiyo, kilichotokea Alhamisi ya tarehe 04/02/2021 majira ya saa nane na nusu mchana. Mipango ya Mazishi inaendelea.

Habari ziwafikie:.
1. Ndugu Wafransisko Wakapuchini popote walipo
2. Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwaichi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Maaskofu, Mapadre, Watawa wa kike na Kiume na Waumini wote
3. Ndugu wa Marehemu wa Padre Paul Ignas Shewiyo, Jamaa na Marafiki popote walipo.

Raha ya Milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani Amina.
 
Huu ugonjwa mbona umekuwa balaa sasa. Huyu ni padre wa ngapi kufariki ndani ya miezi hii ya tishio la Corona?
 
Padri Shewiyo alikua kanisa ka Msimbazi. Amefariki mchana huu hapa Bochi Hospitali .
View attachment 1694362

Apumzike kwa amani mtumishi huyu wa bwana.

Ama kwa hakika uzi huu una maana kubwa sana bandugu:


Ni wazi kuwa tunao muda mchache sana uliobakia kuishi kwa sababu tu ya viongozi wetu.

Jamani eeh, Buriani.
 
Stephen Shewiyo amezikwa jana Jumatano 3rd February 2021. Huyu padre ni mdogo wake wa damu na wote ni changamoto ya upumuaji. Huyo anayedanganya watanzania kuwa hakuna Corona bali ni Pneumonia ninaomba hiyo Pneumonia impate yeye na kizazi chake na asibakie hata mmoja. Leo hii kwenye makundi niliyopo ni msiba mingi na yote ni Pneumonia maana wanaogopa kutaja Corona. Mtu kama kwako hujapigwa na Corona bado kaa kimya. Corona ipo kwa Wingi mno. Wanaugua wanapona na wengine wanakufa. Tusimkebehi Mungu kwa maneno ya uongo ya kutunga. Tanzania siyo Makao Mkuu ya Mungu.

Tuwaambie watanzania ukweli na kweli itatuweka huru. Watu wanakufa wengine wanaponea chupuchupu.
 
Nini Corona nimekua nae hospital tangu jana. Ni Ndugu yangu wa damu. Nasema CORONA NARUDIA CORONA.
Najua hata Maaskofu hawatasema nasema tena ni corona imemchukua Ndugu yangu.

Pole sana apumzike kwa Amani
 
AJABU SANA NAOMBA KUJUZWA HIVI MTU YEYOTE ANAYEFARIKI KATIKA NYAKATI HIZI CHANZO CHA KIFO CHAKE HUWA NI KORONA NAOMBA TUJUZANE HILI KWANZA LINANITATIZA SANA
 
Back
Top Bottom