PAC yashtushwa na mtaji wa 150,000 wa mwekezaji Mlimani City

Kwa hali kama hii Trump ataendelea kutuambia ukweli! Vipi mradi wa airport kule Chato watafika au wanasubiri 2025 akija rais mwingine watasema wamebaini madudu!
 
Unakosea kuita graduate wapuuzi; nafikiri huwezi linganisha nachuo chochote EA.

Aksante
Samahani kwa kutumia neno wapuuzi, linaudhi lakini ni kweli kwamba wanaotuletea shida ni graduate wa UD. Nakuomba nawe usijidanganye kwamba hakilingani na chuo kingine EA, kwa lipi? Vyuo vikuu hupata sifa siyo kwa kufundisha kwa miaka mingi au kufundisha watu wengi, NOO! Je, wamefanya tafiti zozote za maana? Ugunduzi wowote wa maana? Uvumbuzi wowote wa maana? Najua utajibu NOOO! Nini cha kujivunia baada ya miaka 50?
 
UDSM niliwadharau sana walipoingia ule mkataba wa hovyo kabisa ndipo nikajua Elimu bado haijamkoboa Mtanzania kama taasisi kubwa yenye lundo LA wasomi harafu vichwani hamna kitu wanaweka maslahi mbele...
 
Kumbe kusoma nako ni zero tu. Haya masomi yetu ndo yanaongoza kwa wizi na ubabaishaji, sasa uzuri na faida ya kusoma iko wapi?
 
Naona wachangiaji wametoka nje ya mada wote wanalaumu graduates wa udsm. Graduates ndo walisaini mikataba? Tafuteni mkataba muwalaumu waliosaini. Isitoshe mnalalamika tu mitandaoni.
 
Raha ya PAC ni Zitto K kuwa mwenyekiti...imeloose flava saivi... Mnakumbuka Tegeta Escrow kwa mfano weuwee
 
Hivi miaka yooote ile ambayo ZITO alikua mwenyekiti wa kamati hii hakuona huu wizi? Nawaza Tu kwa maandishi
 
Mwekezaji (mzungu) akija hata na elfu 20 atapata pa kuwekeza, wewe mswahili ni mjasiriamali hata uwe na 100mil utazungushwa, utatoa rushwa hadi ziishe.

Mwekezaji is solely reserved for wazungu.
 
Wasomi wetu hawajawahi kuisaidia nchi hii kila anayepewa nafasi anaiba kadiri awezavyo kuanzia raisi hadi vijitaasisi, na mambo makuu kwao ni kujenga nyumba, kununua gari na kuanzisha vijimiradi nakuiacha taasisi nyingi za umma zikifilisika au kurudi nyuma..."wakati mwingine bora bashite"

Nafikiri nimuhimu sana tukiangalia namna bora mitaala yetu itakavyo badilishwa nakutuandalia wasomi wafia nchi. Ila bado kila ninapowaza juu ya elimu namwona mwalimu aliye na maslahi duni kubebeshwa jukumu la kuandaa taifa bora
Mie kibongo bongo mtu akinitajia wasomi najua ni wasoma magazeti tuu..
 
Kwa hivo mlitaka abebe dola nyingi ili akamatiwe Uwanja wa Ndege? A
Watanzania mmejaa njaa na majungu, uwekezaji wa mlimani siyo hela,, ni technology, management, transfer of skills etc. Hela sii unakopa benki, na kwa uchumi Mzuri unakopa hapa hapa kuendeleza mzunguko wa pesa. Hamtaki, wapeni waswahili waendeshe kama mavi hayakujaa hadi mlangoni , punguzeni majungu
 
Wakati hiyo mwekezaji anapewa hiyo tenda kamati ilikuwepo? Haikupewa nafasi kuchunguza hili!? Loh! taabu kwelikweli!
 
Kugundua uozo ni jambo moja kuushughulikia ni jambo jingine. hapo sasa!!!
Mwaka wa pili hakuna mtu aliyefungwa watu wanaozea rumande na kizuizini, utashangaa wote watatoka eti nimewasamehe au ushahidi hakuna. Justice delayed is justice denied
 
Huu ni upumbavu kabisa, Rais Tunakuomba uwadhughulikie wote bila kujali ni kina nani, wamechukua ardhi kubwa mno ingeweza kufanya mambo mengine ya kiacademia..

Isitoshe Udsm ni kitovu cha wasomi nchini, hivyo likifanyika kosa linadhalilisha wasomi wote nchini, tunakuomba Rais uwanyooshe wahusika wote
Na uchunguzi wa boti la bagamoyo to Dar uanze
 
Back
Top Bottom