Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC leo imekataa Ripoti ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Tume ya Uchaguzi nchini, NEC.
Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kuwepo kwa mapungufu na ubadhilifu mkubwa wa Fedha na kuisababishia Serikali hasara ya fedha zilizotolewa kwa Tume hiyo katika Bajeti ya mwaka 2015/2016.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na wajumbe wa kamati hiyo ambao walikutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC kwa lengo lakujadili na kupokea taarifa ya fedha ya Mapato na Matumizi ya NEC kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.
Baada ya wajumbe hao kutoridhishwa na ripoti hiyo ya tume na kugundua bado kuna upotevu mkubwa na ubadhirifu wa fedha za serikali kwenye tume hiyo hadi kufikia kuwapo kwa deni la fedha takribani shilingi bilioni mbili milioni mia nane na ishirini na tatu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC Ramadhani Kailima amekiri mapungufu hayo ndani ya tume.
Akitoa maazimio ya kikao hicho kati ya Tume ya Uchaguzi na Kamati ya Hesabu za Serikali Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati hiyo Mheshimiwa Aeshi Hilaly amekataa kupokea Ripoti hiyo na kuwataka watendaji wa NEC kuifanyia masahihisho Ripoti hiyo na kuipeleka kwa CAG.