P.L.O Lumumba na chambuziza kuwatakasa masihi

Free Africans

Member
Feb 9, 2017
7
1
P.L.O. LUMUMBA NA CHAMBUZI ZA KUWATAKASA MASIHI

Na Gikaro Africa.

Katika mhadhara wake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwanazuoni mashuhuri Afrika, Prof. P.L.O Lumumba alizungumzia dhana ya usafi wa kisiasa (political hygiene). Alitaja viongozi wakuu wa Kiafrika, wengine akiwasifia kama wasafi, na wengine akiwakandia kama wachafu. Cha kushangaza ni pale huo “usafi wa kisiasa” unapoonekana ni jambo la mtu mmoja (kiongozi) na hauhusishwi kabisa na suala pana la mfumo wa uzalishaji-mali.

Kwa hiyo, kama tukifuata uchambuzi wake ni kwamba tukimchagua masihi na kutengeneza katiba ya kiliberali basi mambo yote yatakuwa salama. Kwa hiyo “uduni wa maendeleo” uliopo Afrika unaonekana kusababishwa na viongozi wachafu na katiba mbovu.

Hata hivyo, kila kona ya Dunia kilio chetu ni kimoja, tunaweza tukawa tumetofautiana viwango. Rushwa ipo hata Ulaya. Viongozi wabovu wamejaa katika nchi za Ulaya.

Ninatoa hoja kwamba “political hygiene” haiwezi kupatikana chini ya mfumo wa kiubinafsi (ubepari). Taasisi za mfumo wa kibepari huwandaa watu kuilingana na hitaji la mfumo la kudumisha unyonyaji wa wawavujasho.

Mawazo ya Prof Lumumba pia yanatukuza nchi za Magharibi (Eurocentric).Hoja zake zimekaa kimagharibi na kibepari katika kuyaelezea matatizo ya Afrika kama vile Wasomi wao wakina Prof Rostow na Nurkes waliovyatizama "Uduni" Waafrika ni sababu za ndani kama vile uongozi mbovu, Mabadiliko ya kitabia na kuacha kuzungumza kuhusu "Utumwa na ukoloni kama chanzo cha Uduni.

Prof Lumumba anawaminisha watu kuwa sababu za kibeberu hazijachangia kabisa katika uduni wa maendeleo barani Afrika? Je, chumi za kikuadi zilizopo Africa (compradorial economies) sio chanzo cha matatizo na umasikini Waafrika?

Kama chumi za Ulaya zimepiga hatua fulani ni kutokana na mirija waliochomeka Afrika, Amerika ya Kusini na Asia, zinazowafanya wanyonye utajiri wetu. Na mirija hiyo inachagizwa zaidi na makuadi wao waliotengenezwa na mfumo wa ubepari wa kimataifa. Hivi ni vyanzo vikubwa maana vimepora ajira za wavujajasho na wanyonge na rasimali zetu kwa kuchagizwa na sheria zao.

Mwalimu Nyerere alishawahi kusema, kuwa haijawai kutokea watu wenye uzito tofauti wakapangwa ulingo mmoja wangumi katika kupigania ubingwa labda hao ni vichaa wakipanga uzito tofauti. Kweli kabisa! Ukimweka Cheka na David Haye katika uliongo mmoja itakuwa ni janga kwa Cheka! Vivyo hivyo kwa Paquio na Mada Maugo.

Kwa kutumia mfano huo wa Mwl. Nyerere tunaona kuwa ni vigumu kumaliza uduni huo katika ubepari wa kimataifa kwa sababu nchi maskini zinakuwa zinashindana kwenye soko na nchi zilizohodhi uchumi wa dunia katika kila nyanja, toka uzalishaji na usambazaji.

‘Vishilingi’ vya uchumi wetu, japo ni vingi, haviwezi kupambana na ‘dollar’ ya kibeberu yenye nguvu. Na kuanguka kwa shilingi yetu si bahati mbaya bali ni mpango madhubuti wa nchi za kibeberu na washenga wao IMF na World Bank ili ubeberu wa fedha ya kimarekani (dollar imperialism) uendelea kuimarisha uchumi wao na kudumaza uchumi wetu.

Kwa hiyo, ubepari ndio tatizo kuu la Afrika, na ndio chanzo kikuu cha kutokuendelea kwetu. Tuna mifano ya kubadili viongozi kila uchao lakini maisha yetu yapo palepale kwa kuwa bado hatujabadili mfumo huu wa ubeberu wa kimataifa.

Afrika ilishawahi kutoa viongozi waliokuwa wakipinga ubeberu na kujaribu kujenga uchumi unaojitegemea. Hawa ni kama Patrice Lumumba (wa Congo), Muamar Ghaddafi na Thomas Sankara lakini waliuawa kwa hujuma na uvamizi wa nchi za kibeberu. Nkrumah alipinduliwa, na mawazo ya Nyerere yalihujumiwa na kuzikwa.

Haya ni mambo ya msingi ambayo Lumumba anapaswa kuyatambua.

Tusimwache Prof PLO Lumumba aendelee kupotosha kizazi hiki na kukifanya kiache kuwaza mbali. Mawazo ya Prof Lumumba yamejaa sumu inayopaswa yanapaswa kuogopwa. Mawazo hayo hayaonyeshi kiini cha tatizo la Afrika na namna ya kutatua.

Ni mawazo yasiyo na uhai, yasiyojikita katika dhana nzima ya maendeleo. If P.L.O Lumumba were critical towards imperialism, he would never be academically celebrated.

Ahsanteni

Ndugu Gikaro ni mwanachama wa Jukwaa la Wajamaa Tanzania.
 
Ukimsikiliza PLO anapozungumzia rushwa kwa Africa, the guy speaks the truth. But kwenye utawala he is more of the late African leaders than what is wrong with the current regimes.
 
Professional Lumumba yuko right kabisa.
Kwa muda wa miaka 50 kulitakiwa tuwe na mabadiliko makubwa. Hata kama unazungumzia unyonge wetu unaosababishwa na ubeberu lkn ukiangalia kwa undani utagundua ni unyonge wa kujitakia wa viongozi wetu, wameshindwa kuchukua njia sahihi za kuongoza nchi na uthubutu.
Mm namuelewa sana na naungana nae kutupa lawama zote kwa viongozi wa kiafrika kwa kutufikisha hapa.
Viongozi gani wasiweza kuona hatari zinazo wanyemelea dhidi ya mabeberu? Ni viongozi gani ambao wanajisalimisha kwa mabeberu kama mbwa dhidi ya chatu?
Kuwa viongozi ni kujitoa mhanga kwa ajili ya watu wako hivyo walipaswa kuivunja hii milija mapema
 
Professional Lumumba yuko right kabisa.
Kwa muda wa miaka 50 kulitakiwa tuwe na mabadiliko makubwa. Hata kama unazungumzia unyonge wetu unaosababishwa na ubeberu lkn ukiangalia kwa undani utagundua ni unyonge wa kujitakia wa viongozi wetu, wameshindwa kuchukua njia sahihi za kuongoza nchi na uthubutu.
Mm namuelewa sana na naungana nae kutupa lawama zote kwa viongozi wa kiafrika kwa kutufikisha hapa.
Viongozi gani wasiweza kuona hatari zinazo wanyemelea dhidi ya mabeberu? Ni viongozi gani ambao wanajisalimisha kwa mabeberu kama mbwa dhidi ya chatu?
Kuwa viongozi ni kujitoa mhanga kwa ajili ya watu wako hivyo walipaswa kuivunja hii milija mapema
Tumekuwa na viongozi wazuri Afrika ila wakionekana kufanya vizuri wanawauwa. Kwa mfano Leo Magufuli anataka kutaifisha rasimali zetu kutoka kwa Mabeberu atawekewa vikwazo vya kiuchumi , na hata pengine kumuwa ndicho ninachokizungmza kuwa pressure iko kwa Mabeberu tu
 
Back
Top Bottom