P-Funk Majani umeteleza kumshambulia binti yako kwenye radio, wewe ni sehemu ya tatizo

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Kushindwana ni given kama wewe sio Majani
Kikubwa mazungumzo yawe na TIJA,mi ni optimistic na ni mbadilishaji wa matokeo muda wowote ule pasipo matarajio.
Anyway,mi siyo Majani,na najua reaction yako kwa mtu kama mimi ambaye siyo Majani,hivyo nipokee CONDITIONALLY,offer muachie Majani,nadhani umeelewa.
 

nzaghamba

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
606
500
Paula ni binti atakayekuja kuwa na maisha mazuri Sana , probably ndo atakuwa nguzo kuu ya P-Funk majani, mwanao ni mwanao tuu, kama Baba lazima usimamie ubaba wako to the end...majani bado ana akili za kitoto...
asee!
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
88,879
2,000
Hakukuwa kabisa na haja ya yeye kuyaongelea hayo kwenye chombo cha habari.

Ni masuala binafsi. Hakuna haja wala sababu ya kuufaidisha umma, tena ambao hauna msaada wowote zaidi ya kufurahia, kuchekelea, na kuombea drama ziendelee, utadhani ni tamthilia.

Kama mama na mwana wameamua kuyaanika maisha yao kwenye mtandao, ni vyema yeye akajitofautisha nao na kutoyazungumzia kabisa mambo yao hadharani.

Ila anatia huruma.

Kama sijakosea ni juzi juzi tu hapa alitoka kuchimba biti kwamba atamdhuru sijui ndo Reivani yule...kwa kujirekodi video akiwa na hako kabinti [kake].

Leo kanukuliwa akisema kumbe kabinti kenyewe kameshamwambia kuwa yeye si baba yake.

Angekuwa ni majinuni endapo angekapigania hako kabinti, ikiwa ni pamoja na kujiweka au kujiingiza kwenye hali ya hatari, halafu kumbe kabinti kenyewe kanamkana kuwa si baba yake.

Just bad. All bad.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom