P-Funk Majani umeteleza kumshambulia binti yako kwenye radio, wewe ni sehemu ya tatizo

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
820
1,000
Majani anasema mtoto wake alimkataa, ila hasemi ilikuwaje wakafika hali hiyo.

Majani anasema kwenye radio kuwa mtoto wake kazaliwa na mama asiyestahili.

Majani anaitangazia dunia kwamba binti yake amelaanika.

Kwa mtu mwenye hekma na utulivu wa akili utagundua Baba pia ana tatizo kubwa kuliko mama anaetupiwa lawama zote.

Majani alishindwa kusimama kama baba wakati wa makuzi ya Paula leo unakuja kuutangazia umma kwamba damu yako imeshindikana.

Majani umeteleza ni heri ungeendelea kukaa kimya tunge assume una busara.

Ona sasa unalaumu binti yako na mama yake wanapeleka vitu mitandaoni, na wewe unafanya kile kile unatumia media kutoa hukumu kwa damu yako.

Siku Paula akirudi kwenye media kutolea ufafanuzi kauli zako utasema amekukosea heshima wakati umeendelea kumchafua??

Majani unaumizwa na mtoto wako kuvujisha videos, lakini uhoni tatizo la baba yake wa kufikia kumtongoza na kumtumia dudu analoliona mama yake. Majani uhoni kama ingekuwa fedhea sana kwako kama bwana angefanikiwa kuwala baby mama wako na binti yako?

Majani tumia busara kama baba, linapofika suala la binti yako wewe sio majani wewe ni baba. Kamwe baba huwa hasimami kuishambulia damu yake ni heri ungeendelea kukaa kimya.
 

Mrs Van

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
5,096
2,000
"Usitukane mamba kabla hujavuka mto". Majani kapuyanga halafu bado ana watoto wengine wadogo ambao hajui mbeleni kutakuaje. Mambo ya malezi hayana ujuaji. Wapo waliozaliwa familia za kidini na wamewehuka. Atakuja kukumbuka shuka kumeshakucha
 

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
820
1,000
"Usitukane mamba kabla hujavuka mto". Majani kapuyanga halafu bado ana watoto wengine wadogo ambao hajui mbeleni kutakuaje. Mambo ya malezi hayana ujuaji. Wapo waliozaliwa familia za kidini na wamewehuka. Atakuja kukumbuka shuka kumeshakucha
Majani alikuwa anaenda na vibe la mtandao kasahau Paula ni mwanae no matter what. Mitandao kazi yao ni kushabikia habari.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,133
2,000
Paula ni binti atakayekuja kuwa na maisha mazuri Sana , probably ndo atakuwa nguzo kuu ya P-Funk majani, mwanao ni mwanao tuu, kama Baba lazima usimamie ubaba wako to the end...majani bado ana akili za kitoto...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom