Njowepo
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 9,710
- 2,232
KIKOSI cha wachezaji 16 wa soka walio chini ya umri wa miaka 17, Copa Coca-Cola Dream Team, waliopatikana kupitia fainali za taifa katika michuano ya Copa Coca-Cola, juzi walifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano maalumu yaitwayo Coca-Cola Inter-Tournament yaliyofikia tamati juzi, nchini Brazil.
Mashindano hayo yaliyokwenda sambamba na mafunzo, yalifanyika katika kituo cha michezo cha Brazil cha BSA, kinachomilikiwa na kocha maarufu, Alberto Pereirra, yalifanyika katika Uwanja wa Maracana yakishirikisha vijana wa umri huo kutoka nchi mbalimbali.
Timu hiyo iliyo chini ya makocha - Mbrazili Marcio Maximo na Marsh Sylvestre - katika mechi ya kwanza iliifunga Peru mabao 5-0, hivyo kutinga hatua ya robo fainali.
Katika hatua hiyo, vijana hao walitoka sare ya bila kufungana na Chile kabla ya kuitungua Argentina 2-0 katika mechi ya nusu fainali, hivyo kufanikiwa kufika fainali ya mashindano hayo.
Juhudi za vijana hao hazikuishia hapo, kwani walizidi kujituma hata katika mechi ya fainali dhidi ya Chile na kufanikiwa kuwafunga bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kimataifa.
Keep it up!