Out of Touch: Madhara ya kusafiri mara kwa mara?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nyumbani ni shwari. Mnaweza kusikia mengi ya siasa kupitia magazetini, lakini mwaka huu ni mwaka wa siasa. Mtasikia mengi ya kisiasa, lakini msiwe na wasiwasi, nchi yetu ni shwari - Kikwete (akizungumza na wanafunzi wa kiTZ huko Uturuki)
 
Nchi ni shwari kwa sababu yeye anapata pesa ya walipa kodi na kufanya shopping za nguvu huko ughaibuni. Ingekuwa siyo shwari angekuwa magogoni kwa sababu kusingekuwa na fweza ya kutumbua.
 
He he!

Dodoma ni shwari. Vijana wanafanya kazi vizuri.
Chama chenu kiko shwari....
Yeah, yeah

Hivi kwani mtu lazima uwe diplomatic kila saa?
 
Kuta za ndege zimempumbaza. He even dont know what is going on in his own country.
 
Wakuu kuweni fair sometimes yaani nyinyi Rais asicheke asinune.Akisema tabu,akikaa kimya tabu.Duuh!
 
Mwanakijiji hayo siyo madhara ya kuwa out of touch. The guy is very much in touch with reality ndio maana anapiga hiyo propaganda/pr. He is only alienated from real people!
 
Nyumbani ni shwari. Mnaweza kusikia mengi ya siasa kupitia magazetini, lakini mwaka huu ni mwaka wa siasa. Mtasikia mengi ya kisiasa, lakini msiwe na wasiwasi, nchi yetu ni shwari - Kikwete (akizungumza na wanafunzi wa kiTZ huko Uturuki)

Hata kile kikao cha NEC kilichofanyika mpaka usiku wa mamne mambo yalikuwa shwari kabisa na huo muda tuliongeza kwa kamati ya Mwinyi mambo ni shwari tu. Kuhusu mafisadi...wote ni shawri tu wanaendelea kupeta na hata Kiwira ni shwari tu tutamlipa Mkapa bilioni 17 zake na kisha kuirudisha Serikalini. Richmond nayo ni shwari tu yule best wangu RA bado anapeta tu akijiandaa na kampeni za 2010. Kuhusu rasilimali zetu mambo ni shwari tu, "wachukuaji" bado wanachukua 97% ya mapato na kutuachia sisi 3% hii inatutusha kabisa.

Kwa hiyo kama mtakavyoona nchi yote ni shawri kabisa! :confused:

Usanii wa kutisha!
 
Wakuu kuweni fair sometimes yaani nyinyi Rais asicheke asinune.Akisema tabu,akikaa kimya tabu.Duuh!

Si hivyo p53 (by the way which tumour are you preventing? - inside joke)

Ni kwamba Rais ametuangusha wengi tuliokua na matumaini mengi kwake.
Hasa mimi. Mwanzoni alikua ananisisimua kwa ari yake. Sasa hivi, mh!

Mimi ninachosema ni hivi, kwa nini asiwe mkweli aawambie tu wananchi hali ya kisiasa ni hivi na vile, na sio kusema ni shwari wakati sote twajua sio. Hayo mambo ya "kila kitu shwari" ni ya kusema kwa watu wa nje, watoto wa nyumbani unawaambia ukweli bwana
 
Zenji shwari, Kyela shwari, Manzese shwari, Musoma shwari!!

Nadhani alichokuwa anataka kusema ni - "Bongo tambarare" ila akasita tu kidogo!
 
swaga za bongo tambarare anajua zilishapitwa na wakati....almanusura aseme bongo mbarrtata. Hii swaga aliinasa alipohudhuria tamasha la zinduka.
 
Wakuu kuweni fair sometimes yaani nyinyi Rais asicheke asinune.Akisema tabu,akikaa kimya tabu.Duuh!

Unafikiri kwanini kuna nchi zimeendelea mpaka kuweza kutulemaza sisi kwa kutegemea misaada yao? Unafikiri wananchi wao wana simile na viongozi?? Jinsi Waafrika tulivyo na tamaa na kujawa ujinga mwingi, tusipoamka sasa hivi na kuwakomalia hawa wanaochukua fomu na kuomba kutuongoza unafikiri tutafikia hata nusu ya matamanio yetu??

Pamoja na mafanikio yake ya kuhesabika kwenye baadhi ya mambo, ukweli unabakia palepale, Mh. Rais wetu ni bitoo fulani hivi na anapenda kukata mbuga kichizi, jambo ambalo si baya hata kidogo kwa mtu binafsi tu au mfanyabiashara fulani hivi. Ila tatizo na manung'uniko mengi yanatokana na cheo cha huyu ndugu yetu na mzazi; Ni Mh. Rais wa Jamhuri ya Tz! Tunamhitaji nyumbani. Sote tukiamua kukaa kimya, hachelewi kufunga safari za miezi 3 au 6 Thailand bila kugeuza home. oooh hoh!
 
Si hivyo p53 (by the way which tumour are you preventing? - inside joke)

Ni kwamba Rais ametuangusha wengi tuliokua na matumaini mengi kwake.
Hasa mimi. Mwanzoni alikua ananisisimua kwa ari yake. Sasa hivi, mh!

Mimi ninachosema ni hivi, kwa nini asiwe mkweli aawambie tu wananchi hali ya kisiasa ni hivi na vile, na sio kusema ni shwari wakati sote twajua sio. Hayo mambo ya "kila kitu shwari" ni ya kusema kwa watu wa nje, watoto wa nyumbani unawaambia ukweli bwana

Kweli mkuu ameangusha wengi na mimi ni mmojawapo niliyeweka matumaini mengi sana kwake.Lakini sasa mkuu naona kama yamezidi.Nisingependa kumtetea lakini ifike mahali tumpe pumzi kidogo na yeye hasa kwa mambo madogomadogo kama haya.Yaani seriously speaking Rais awaambie hao vijana wa Uturuki tulikuwa na mzozo kwenye CC au NEC,nchi yenu sasa hivi hali si shwari,inayumba,nusura wajumbe wakamatane mashati,tuna makundi CCM nk nk kwa mfano.Hivi kweli ina make sense hii wakuu?
Which tumor mi protecting??hahaha twende jf doctor tukakate madude mkuu!
 
Unafikiri kwanini kuna nchi zimeendelea mpaka kuweza kutulemaza sisi kwa kutegemea misaada yao? Unafikiri wananchi wao wana simile na viongozi?? Jinsi Waafrika tulivyo na tamaa na kujawa ujinga mwingi, tusipoamka sasa hivi na kuwakomalia hawa wanaochukua fomu na kuomba kutuongoza unafikiri tutafikia hata nusu ya matamanio yetu??

Pamoja na mafanikio yake ya kuhesabika kwenye baadhi ya mambo, ukweli unabakia palepale, Mh. Rais wetu ni bitoo fulani hivi na anapenda kukata mbuga kichizi, jambo ambalo si baya hata kidogo kwa mtu binafsi tu au mfanyabiashara fulani hivi. Ila tatizo na manung'uniko mengi yanatokana na cheo cha huyu ndugu yetu na mzazi; Ni Mh. Rais wa Jamhuri ya Tz! Tunamhitaji nyumbani. Sote tukiamua kukaa kimya, hachelewi kufunga safari za miezi 3 au 6 Thailand bila kugeuza home. oooh hoh!

Ndiyo mkuu nakubaliana nawe unaposema Mh.Rais apunguze safari zisizo za lazima ili ashughulikie matatizo ya nyumbani,kumbe siyo kwenda kutoa siri za vikao kwa vijana wa Uturuki!
 
Kweli mkuu ameangusha wengi na mimi ni mmojawapo niliyeweka matumaini mengi sana kwake.Lakini sasa mkuu naona kama yamezidi.Nisingependa kumtetea lakini ifike mahali tumpe pumzi kidogo na yeye hasa kwa mambo madogomadogo kama haya.Yaani seriously speaking Rais awaambie hao vijana wa Uturuki tulikuwa na mzozo kwenye CC au NEC,nchi yenu sasa hivi hali si shwari,inayumba,nusura wajumbe wakamatane mashati,tuna makundi CCM nk nk kwa mfano.Hivi kweli ina make sense hii wakuu?
Which tumor mi protecting??hahaha twende jf doctor tukakate madude mkuu!

Mkuu wewe huchezi michezo ya ushindani nini? Siasa ni mchezo mchafu. Kama tunataka maendeleo kutokana na bidii za viongozi wetu, hatuna budi kushindilia magoli pale wanapolegea. We have to keep them on their toes, all the time that is, else they'll fail us all!!
 
Wakuu kuweni fair sometimes yaani nyinyi Rais asicheke asinune.Akisema tabu,akikaa kimya tabu.Duuh!

well.. akisema aseme mambo yenye mantiki akinunua anuniane na mkewe siyo na taifa, akicheka acheke kwenye vyenye kuchekesha... vinginevyo.. kama wanavyosema ukikaa kimya watu wanaweza kufikiria una hekima!
 
Well...mantiki ni kusema yale tu ungependa uyasikie,mantiki ni yale yenye kupendeza mbele ya macho yako tu,mantiki ni kuwaambia vijana wa uturuki migogoro ya CCM,mantiki....
 
Wakuu kuweni fair sometimes yaani nyinyi Rais asicheke asinune.Akisema tabu,akikaa kimya tabu.Duuh!

Wewe umesahau? Mwenzio hata akimpa dogo peremende watu wanambebea bango.....either way, he's damned if he doesn't, he's damned if he does (whatever that may be)....it just comes/goes with the territory
 
Ndiyo mkuu nakubaliana nawe unaposema Mh.Rais apunguze safari zisizo za lazima ili ashughulikie matatizo ya nyumbani,kumbe siyo kwenda kutoa siri za vikao kwa vijana wa Uturuki![/QUOT

Hivi kazi ya Membe ni ipi exactly! In the last four years, Kikwete has made way more news in the International Scene than Membe...Jamaica and many others Membe could have easily handled...nini kimfukuzacho Raisi wetu??
 
Wewe umesahau? Mwenzio hata akimpa dogo peremende watu wanambebea bango.....either way, he's damned if he doesn't, he's damned if he does (whatever that may be)....it just comes/goes with the territory

Bado unatetea tu u-candyman, na wewe ulipewa pipi nini?
 
Back
Top Bottom