Our beloved late President Magufuli: Was he a science denier or a threat to the Empire?

Mababeru wanatabu sana... hawajahi kututakia memo...
Uko sahihi kabisa mkuu,kila wanalotufanyia lina agenda ya
kutu-sabotage,kwa hiyo ni lazima kila juhudi ifanywe ili tuweze kujitegemea.Ni hatua,lakini ni lazima tuanze harakati hizi.Rome haikujengwa siku moja.
 
Magufuli alifanya vitu kwa manufaa ya wengi bana,watanzania wachache tu ndio wanataka kutuaminisha alikua mbaya.
Uko sahihi kabisa mkuu,na hao ni agents wa mabeberu.Wanataka tuamini kwamba hatuwezi,ila ni lazima tupaishe sauti zetu tuwaambie wazi,sisi ni matajiri,we have the resources kwa hiyo tunaweza kujitegemea, ni swala la muda tu.
 
Umeuliza vyema, what is the problem with us? Kwa ngazi na potential ya mtu mmoja mmoja there is no problem with us. Sisi pia tuna watu wenye uwezo wa kuinvent na kuinnovate, tuna watu wenye uwezo wa kufikiri mambo makubwa sana.

Tatizo lipo kwenye historia, culture na philosophy, na nitafafanua. Historia ni kitu cha msingi sana, hakuna kitu chochote kinachotokea kwenye vacuum. Maendeleo yote waliyonayo Europe yameanzia kipindi cha Civilization ya Enlightenment miaka ya 1500. Kabla ya hapo Ulaya ilikuwa kama Afrika, tena si ajabu kuna civilizations fulani za kiafrika zilikuwa na maendeleo kulilo Ulaya miaka hiyo. Kipindi cha Enlightenment kilitokana na elimu za theologia, wazungu miaka hiyo walikuwa wamejenga ma seminari ya kufundisha biblia, na kufanya tafiti kuhusu Mungu, Christian morality, vilivyotokana na dini ya Ukristo. Vyuo kama Cambridge na Oxford University vilianza kama seminari.

Kutokana na uhitaji huo biblia ikaanza kunakiliwa sana, baadae watu wakagundua printers ili kurahisisha kazi ya kunakili, baadae watu wakaanza kuchapa na vitabu vya maarifa mengine. Ongezeko hili la maarifa likafanya hadi elimu zingine zisizo za dini zianze kupata nafasi, mfano hesabu, sayansi na literature. Kukua kwa sayansi kukachochea ubunh na ugunduzi. Wakati huo waafrika bado tuko kwenye mambo yetu tunayoyajua wenyewe.

Kukua kwa maarifa Ulaya kukazaa industrial revolution, industria revolution ikazaa ukoloni wa Afrika, ukoloni wa Afrika ukazidi kuiweka Afrika chini kiutawala na kiakili.

Ukoloni ulikuwa na madhara makubwa sana. Ulizaa watu wasiojiamini kabisa, ukatengeneza kizazi kinachofikiri wazungu ni species tofauti na waafrika. Inapotokea akaja kiongozi revolutionary kama Magufuli unaona jinsi anavyopata tabu sana kubadilisha mitazamo ya anaowaongoza. Tamaduni zetu zimechangia pia maana zimekaa kichawichawi sana, refers waganga wa vienyeji wanaowaagulia watu kwenye masuala mbalimbali ukiwemo kupata fursa za uongozi au utajiri.

Yaani ni taab tupu, lakini tutafika tu!
Mkuu ni kweli sisi kama wanadamu hatuna matatizo,we can invent.Shida ni years of indoctrination trough the media,education and even verbal communication that we are inferior to the Whiteman.Hii imetufanya tuamini kwamba we cannot do anything good,and so have to depend on them.Hii wameifanikishwa sana pia through soft power,hasa cinema.Cinema hasa Hollywood ni deadly form of soft power.Look at how we value English and therefore the Whiteman.It is beyond belief that we believed that English just a language.Lakini hii imefanikishwa na soft power.
 
Magufuli alipopendekeza mtaala mpya wa historia ufundishwe mashuleni mbona mlimpinga, au nyie mlifikiri hakuwa na mantiki yoyote?

Mlitaka JPM alete mapinduzi kiasi gani hasa? Yeye alikuja na falsafa ya watanzania tunaweza tujiamini. Kwangu mimi lile lilikuwa ni jambo kubwa sana katika kuleta mapinduzi ya fikra. Wewe kama hauoni kwamba kuna tatizo la watu wetu kujiamini na kufanya mambo yetu kama watu huru, basi ndio nikwambie taifa letu lina hilo tatizo, na limezaa watu wasio na uwezo wa kufanya maamuzi magumu au sahihi. Ufukara unaanzia hapo. Refer, mfano, kwa kiongozi kutowekeza kwenye afya za ndani akitegemea akiugua atakimbizwa nje. Ni utopolo tu yaani

Mkuu kama kweli hujaona mapinduzi aliyoleta Magufuli, basi wewe ni kipofu,kwa kuwa miradi mingi aliyoianzisha Magufuli,ni mapinduzi tosha,achilia mbali kwamba italeta mapinduzi kwenye maisha ya watu moja kwa moja.

Mkuu mapinduzi pia aliyoleta Magufuli kifikra yako wazi.Sasa Watanzania wamejua kwamba kumbe ni matajiri,kwa hiyo wanaweza kujitegemea.Magufuli ame-impart pia ujasiri usio wa kawaida.Ujasiri tunaouona kwa viongozi wetu ni matunda ya Magufuli.Pia Magufuli ame-impart uthubutu kwa Watanzania,na hili tunalishuhudia kwa viongozi wetu,kwa hiyo si kweli kwamba Magufuli hajaleta mapinduzi yeyote.

Nimalizie kwa kusema kwenye shule za "kawaida" za Wazungu hawanafundishwi Historia yetu,infact hata Geografia yetu!Si ajabu Mzungu wa kawaida ukimuuliza Tanzania iko wapi akakuambia iko China!Mkuu ipo special cadre,and mostly familia za watu wa NWO na agents wao,ambao wanafundishwa historia yetu and for a special purpose:kuweza kutu-sabotage ili waweze ku-advance agenda yao ya total enslavement of the human race.
Mkuu miradi ya kimaendeleo kua mingi haimaanishi kwamba tupo vizuri au tumetoka kwenye mental slavery maana hata Ethiopia wanamiradi mikubwa ya maendeleo lakini bado ni tegememezi, bado ni maskini.
So usichukulie miradi kua kipimo cha kiongozi bora (kutoa watu kwenye utumwa wa kifikra)
 
Uko sahihi kabisa mkuu,na hao ni agents wa mabeberu.Wanataka tuamini kwamba hatuwezi,ila ni lazima tupaishe sauti zetu tuwaambie wazi,sisi ni matajiri,we have the resources kwa hiyo tunaweza kujitegemea, ni swala la muda tu.
Mkuu hatuwezi kujitegemea kama hatujawekewa misingi ya kujitegemea.
Kwa mfano ukiwaauliza wasomi wa hapa nchini kazi ya madini aina ya Tanzanite ni ipi 99.99% hawajui.
We have resources but we still don't know yet their value nor uses
 
Mkuu miradi ya kimaendeleo kua mingi haimaanishi kwamba tupo vizuri au tumetoka kwenye mental slavery maana hata Ethiopia wanamiradi mikubwa ya maendeleo lakini bado ni tegememezi, bado ni maskini.
So usichukulie miradi kua kipimo cha kiongozi bora (kutoa watu kwenye utumwa wa kifikra)
Maendeleo ni hatua mkuu,na yanaanza na madiliko ya fikra au vyote pamoja,inategemea jamii yenyewe.
Sisi Tanzania tutakwenda na vyote kwa kuwa tumechelewa.

Naomba usiniambie mambo ya Ethiopia,hizo ni mbinu zile zile za mabeberu za kutukatisha tamaa.Sisi Tanzania ni jamii tofauti na mazingira yetu ni tofauti.Wewe kama unaona huwezi ni wewe,kaa pembeni,sisi tunaweza,acha tusonge mbele.
 
Tunakiwa tuwekeze kwenye elimu zaidi. Watu wengi wakiwa wameelimika ni rahisi maendeleo ya vitu kupatikana.
Kwa hapa Tanzania hayati Magufuli aliwekeza kwenye vitu zaidi kuliko elimu.
Mfano mdogo ni manunuzi ya ndege, alafu kuna shule iliyoko Dar wanafunzi walikua hawana vyumba vya kutosha vya madarasa.
 
Mkuu miradi ya kimaendeleo kua mingi haimaanishi kwamba tupo vizuri au tumetoka kwenye mental slavery maana hata Ethiopia wanamiradi mikubwa ya maendeleo lakini bado ni tegememezi, bado ni maskini.
So usichukulie miradi kua kipimo cha kiongozi bora (kutoa watu kwenye utumwa wa kifikra)
Kwani nani kasema mapinduzi ya msingi tunayoyazungumzia ni miradi tu. Miradi mikubwa ni matunda au matokeo ya mapinduzi ya kifikra tunayoyazungumzia.

Yule bwana hata mi wakati anaanza uongozi wake nilikuwa na mashaka sana. Nilishachoka na system ya CCM iliyozaa viongozi wategemezi na nchi tegemezi balaa, na sikutegemea kama Magufuli angekuwa any different. Lakini alivyoanza kusema sisi tunaweza, nchi hii ni tajiri, hata kabla ya miradi yoyote kuanza nikajua huyu mzee atafanikiwa sana. Na ni kweli kafanikiwa kwa sababu pamoja na hali ngumu kiuchumi kwenye mifuko ya watu lakini alituinspire kukubaliana na hali hiyo kwa sababu tulijua tunajenga nchi yetu kwa mikono yetu sisi wenyewe.

Sasa kuna takataka zingine huko nyuma zilishawahi kuongoza nchi yetu kila kukicha ipo Davos, sijui New York, ukiuliza ilienda kufanya nini kumbe inatumbua kodi zetu na kutembeza bakuli. Mental slavery ni kuamini kwamba solutions za matatizo yetu ziko nje ya uwezo wetu. Mzee alituinspire kuamini kila kitu kiko ndani ya uwezo wetu. Nashangaa hata kwa nini tunajadili hili maana Siasa na Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea ililenga kuleta mapinduzi hayo ya kifkra. Kwanini tulirudi nyuma pengine ni swali lililo complex zaidi ya kufit post hi lakini kiongozi yeyote atakayetusukuma tupige hatua kuelekea lengo la mental independence kwa watanzania kwa kiasi fulani ana nafasi kubwa ya kuteka mioyo ya watanzania. Mwinyi alishindwa kabisa, Mkapa alianza vyema lakini akahemewa baadaye, Kikwete aliturudisha hatua kadhaa nyuma, JPM amegeuza treni lielekee tunakotaka kwenda, bado namsoma mama, lakini la muhimu sana hawa viongozi wetu watahitaji support iwapo nia zao ni njema, ila sisi kama raia wa kawaida tuwapige vita tukiona wanakotaka kwenda au wanakotupeleka hawa viongozi wetu siko. Vinginevyo ni rahisi kupotoka hawa viumbe na kuna pressure kubwa sana kutoka nje ili wapotoke. Tusikubali.
 
Ulishawahi kujiuliza kwa nini washika urais ni Wakatoliki na Waislam(BAKWATA)?
 
Mkuu hatuwezi kujitegemea kama hatujawekewa misingi ya kujitegemea.
Kwa mfano ukiwaauliza wasomi wa hapa nchini kazi ya madini aina ya Tanzanite ni ipi 99.99% hawajui.
We have resources but we still don't know yet their value nor uses
Kuna levels tatu za kujitegemea. Level ya kwanza ni kuamini na kujiaminisha kwa binadamu wote ni sawa na kwa umoja wao kama kikundi cha watu wa sehemu fulani wana potentials au talanta za kufikia mafanikio ya kimwili na kiroho. Bila kuamini hivyo unaweka mwanya wa kunyonywa na kutawaliwa na binadamu wengine, au kudumaa.

Hatua ya pili ya kujitegemea ni kuchukuaa hatua zako wewe mwenyewe, kama mtu binafsi au kama kundi la watu kwa spirit ya kujiamini. Imani ni kitu kikubwa sana, na ndio maana ni vigumu kupigana vita vyenye msingi wa imani. Kwa mfano wazungu wanafanya mambo makubwa sana kwa sababu kuna imani fulani inayowasukuma nyuma. Wamarekani wana imani kwamba nchi yao ipo kwa ajili ya kutawala dunia, Wangereza wanafanya vitu vyao kwa sababu ya pride ya kifalme (ndio maana majeshi yao utasikia royal navy, royal air force, charles darwin alifanya utafiti wake kwenye His Majesty Ship Beagle, n.k), Waisraeli walipigana na waarabu lukuki na kuwashinda maana wana imani kwamba wao ni taifa teule, n.k. Sasa sisi Tanzania Nyerere alinuia kujenga taifa fulani lenye misingi ya imani ya utaifa (Nationalistic Zeal), ila akakumbana na kazi ngumu kwelikweli. Kwanza alijikuta anaongoza watu wapumbavu balaa, kila anachotaka kuwaambukiza wanaona kama anawachelewesha kwenye utajiri. Ni upumbavu huo huo aliokumbana nao Nyerere ndio aliokumbana nao Magufuli. Anyway niishie hapo.

Level ya tatu ya kujitegemea ni kufanya mambo yako mwenyewe, yaani kudictate your own fate, kudetermine your own value na kubuild your own things in your own image. Mfano sisi hatuna sababu ya kufahamu Tanzanite inafanya kazi gani ili tuonekane tumejitegemea. Sisi kazi yetu ni kujua kwamba kwa vile Tanzanite ina soko huko nje, basi tutahakikisha tunajitegemea katika kuichimba, kuiongezea thamani na kupata faida zaidi. Kama uwezo huo hatuna kwa sasa tunajijengea huo uwezo, au tutashirikiana na wenye uwezo kwa win-win situation. Yapo mambo yetu tunayoyaona ya thamani na tutayapa thamani kwa vile ni yetu, si lazima tudese kwa wenzetu kujua kama ni ya thamani. Kwa mfano, watanzania tunapenda kula ugali samaki sato, kwa hiyo kwetu sisi hatuhitaji validation ya kwingineko huko kujua kama ugali sato ni chakula cha thamani au vipi. Huo ndio uhuru wa kifikra, uhuru wa kujiamini na uhuru wa kujithamini.
 
Ulishawahi kujiuliza kwa nini washika urais ni Wakatoliki na Waislam(BAKWATA)?
Sidhani kama kuna ishu yoyote ya kimfumo inayofanya nafasi ya urais iwaangukie wakatoliki na waislamu. Nafikiri ni inshu ya random chance, na kihesabu kwa vile wakatoliki na waislam ni over 80% ya population ya Tanzania kutakuwa na over 80% probability kwamba nafasi yoyote ile katika nchi hii, si urais tu, watashika waislamu na wakatoliki.
 
This is not a conspiracy theory. It's been substantiated with enormous evidence embedded in the referenced article.
 
Sidhani kama kuna ishu yoyote ya kimfumo inayofanya nafasi ya urais iwaangukie wakatoliki na waislamu. Nafikiri ni inshu ya random chance, na kihesabu kwa vile wakatoliki na waislam ni over 80% ya population ya Tanzania kutakuwa na over 80% probability kwamba nafasi yoyote ile katika nchi hii, si urais tu, watashika waislamu na wakatoliki.
Ili kuepusha nchi kuingia kwenye migogoro ya kidini na kikabila, haijulika idadi ya waislam ni % ngapi wala ya wakristo.
Sijui iyo 80% umeipatia wapi.
 
Kuna levels tatu za kujitegemea. Level ya kwanza ni kuamini na kujiaminisha kwa binadamu wote ni sawa na kwa umoja wao kama kikundi cha watu wa sehemu fulani wana potentials au talanta za kufikia mafanikio ya kimwili na kiroho. Bila kuamini hivyo unaweka mwanya wa kunyonywa na kutawaliwa na binadamu wengine, au kudumaa.

Hatua ya pili ya kujitegemea ni kuchukuaa hatua zako wewe mwenyewe, kama mtu binafsi au kama kundi la watu kwa spirit ya kujiamini. Imani ni kitu kikubwa sana, na ndio maana ni vigumu kupigana vita vyenye msingi wa imani. Kwa mfano wazungu wanafanya mambo makubwa sana kwa sababu kuna imani fulani inayowasukuma nyuma. Wamarekani wana imani kwamba nchi yao ipo kwa ajili ya kutawala dunia, Wangereza wanafanya vitu vyao kwa sababu ya pride ya kifalme (ndio maana majeshi yao utasikia royal navy, royal air force, charles darwin alifanya utafiti wake kwenye His Majesty Ship Beagle, n.k), Waisraeli walipigana na waarabu lukuki na kuwashinda maana wana imani kwamba wao ni taifa teule, n.k. Sasa sisi Tanzania Nyerere alinuia kujenga taifa fulani lenye misingi ya imani ya utaifa (Nationalistic Zeal), ila akakumbana na kazi ngumu kwelikweli. Kwanza alijikuta anaongoza watu wapumbavu balaa, kila anachotaka kuwaambukiza wanaona kama anawachelewesha kwenye utajiri. Ni upumbavu huo huo aliokumbana nao Nyerere ndio aliokumbana nao Magufuli. Anyway niishie hapo.

Level ya tatu ya kujitegemea ni kufanya mambo yako mwenyewe, yaani kudictate your own fate, kudetermine your own value na kubuild your own things in your own image. Mfano sisi hatuna sababu ya kufahamu Tanzanite inafanya kazi gani ili tuonekane tumejitegemea. Sisi kazi yetu ni kujua kwamba kwa vile Tanzanite ina soko huko nje, basi tutahakikisha tunajitegemea katika kuichimba, kuiongezea thamani na kupata faida zaidi. Kama uwezo huo hatuna kwa sasa tunajijengea huo uwezo, au tutashirikiana na wenye uwezo kwa win-win situation. Yapo mambo yetu tunayoyaona ya thamani na tutayapa thamani kwa vile ni yetu, si lazima tudese kwa wenzetu kujua kama ni ya thamani. Kwa mfano, watanzania tunapenda kula ugali samaki sato, kwa hiyo kwetu sisi hatuhitaji validation ya kwingineko huko kujua kama ugali sato ni chakula cha thamani au vipi. Huo ndio uhuru wa kifikra, uhuru wa kujiamini na uhuru wa kujithamini.
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana.
Yani hutaki kujua kazi ya madini ya Tanzanite? Smfh
 
Ili kuepusha nchi kuingia kwenye migogoro ya kidini na kikabila, haijulika idadi ya waislam ni % ngapi wala ya wakristo.
Sijui iyo 80% umeipatia wapi.
Idadi ya waislamu ni almost thirty percent na ya wakristo ni about sixty percent. Refer hapa. Religion in Tanzania - Wikipedia.

Si kila mkristo ni mkatoliki so naestimate kwamba labda robo tatu ya wakristo ni wakatoliki (about 45%) percent maana ndio dhehebu kubwa zaidi nchini. Ndipo nilipopata hiyo estimate ya about 80%.
 
Religion doesnt matter anymore. The modern economic war is very strategic. Its better for people to be spiritual than religious.
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana.
Yani hutaki kujua kazi ya madini ya Tanzanite? Smfh
Kwa muktadha wa uhuru wa kifikra, si lazima ujue. Kwani utajua vitu vyote duniani?

Mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana, nakubaliana nawe. Sababu kuu ya ubovu wetu wa elimu ndio hiyo hiyo tunayoijadili sasa, kwamba hatupo huru kifikra. Mitaala yetu ipo kinadharia sana kuliko kivitendo, na sababu kuu ya unadharia huo ni kwa sababu tunadesa mitaala ya waliotukoloni. Kimsingi elimu yetu inaandaa makarani, na vibaraka wa wazungu, na hasa ndio lilikuwa lengo la elimu ya mkoloni kwa mwafrika. Mitaala haikuwahi kubadlishwa mizizi yake, na hata maofisa wa elimu wanapokaa kutengeneza mitaala mipya, hawafanikiwi kutengeneza mitaala inayoifaa Tanzania ya leo. Huu uwe mjadala wa kitaifa, ni mtaala gani unafaa kwa Tanzania ya sasa na tunayoitaka?
 
We unafikiri ni kwa nn tanzania pamoja na wizara ya elimu wamekosa confidence ya kubadili mitaala hadi leo. Unahisi mawaziri waliopita wote na maraisi ni kwamba wanasahau au hawalifanyi kimakusudi kuwafurahisha walio uweka mfumo toka ukoloni
 
Religion doesnt matter anymore. The modern economic war is very strategic. Its better for people to be spiritual than religious.
Naunga mkono hoja. Religions divide, Spirituality unites. Kwa mfano ninapowatazama watanzania wote kwa ujumla bila lens za dini nawaona watu wenye changamoto zinazofanana na wenye talanta zinazoshabihiana. Wote tunapenda amani, furaha, watoto wetu wapate elimu na maarifa bora, na upendo baina yao. Hizo ni tunu za kiroho (spiritual elements). Dini pia zina nafasi katika kujenga na kukuza tunu za kiroho, zikijitambua nafasi zao. Ila zikianza kutumika kuhubiri chuki, na kuleta utengano katika jamii, hiyo taasisi lazima ifuatiliwe na kushughulikiwa.
 
Tunakiwa tuwekeze kwenye elimu zaidi. Watu wengi wakiwa wameelimika ni rahisi maendeleo ya vitu kupatikana.
Kwa hapa Tanzania hayati Magufuli aliwekeza kwenye vitu zaidi kuliko elimu.
Mfano mdogo ni manunuzi ya ndege, alafu kuna shule iliyoko Dar wanafunzi walikua hawana vyumba vya kutosha vya madarasa.
Mkuu tuna watu wenye elimu wa kutosha,hili sio tatizo.Nasema wewe kaa pembeni,ninyi watu wachache hamwezi kutu-derail,we know we are on the right path.Mbona kwa Mwinyi,Mkapa na Kikwete hatukuwasikia mkipiga kelele,and they were doing badly.Tafadhali kaeni pembeni,we are not interested.
 
Back
Top Bottom