OTHMAN OMARI MSEKENI-Fundi Bingwa na kapteni wa jeshi mstaafu aliyesahaulika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OTHMAN OMARI MSEKENI-Fundi Bingwa na kapteni wa jeshi mstaafu aliyesahaulika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Iga, Sep 5, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Sep 5, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NAPENDA muwasiliane na Kapteni Othamni Omari Msekeni ili kumsaidia katika juhudi zake za kuwakomboa Watanzania masikini na hasa wakulima, wavuvi na wafugaji vijijini.

  Bwana huyu ametengeneza mashine ya kuzalisha umeme inayotumiwa upepo lakini inaelekea anapigwa vita na serikali na makampuni makubwa yanayotoa 10 pasenti kwa Watanzania wasio na uchungu na nchi hii ili wamkatishe tamaa bwana huyu katika jitihada zake hizi takatifu na zenye kumhakikishia pepo tofauti na viongozi wachoyo na madhalimu.

  Vinginevyo Kapteni Othamn Omari Msekeni kawaone balozi wa India au China na wataichangamkia tenda yako mara moja tuache sisi tusiotaka maendeleo kwa sababu ya teni pasenti tubaki hapa hapa.

  TUMESHINDWA kujua kuwa uongozi sio KUSHIKA OFISI YENYE VIYOYOZI NA MASHANGINGI bali ni kwenda kwa watu kwa lengo la kubadili maisha yao wakati wa uongozi wako na sio baadaye. Maana baadaye kila mtu atakuwa keshakufa!

  Tafadhali Redio Kheri mpatieni Mwanakijiji nakala ya mahojiano yenu na Mzee Othman Omari Msekeni aiweke mtandaoni dunia nzima ione jinsi tulivyo na matatizo ya kujitakia sisi Watanzania kwa yakini.
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huko huko jeshini kuna kitengo kikubwa tu cha uhandisi kashindwa nini kufanyakazi nao? another Masau in making...
   
Loading...