Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar leo amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kufuatia kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Uteuzi huo umefanywa na Rais kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, na vilevile baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo.

Uteuzi wa Othman Sharif unaanza leo na ataapishwa kesho Machi 02, 2021 Ikulu Zanzibar.

Pia soma

Othman.jpg

46596D7C-1961-4184-B8BA-42F8745ECE58.jpeg

Safi Sana. Huyu jamaa ni muumini wa mamlaka kamili ya Zanzibar na wazanzibari, hatakagi ujinga huyu.

Aliitupilia mbali nafasi yake ya kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati wa mjadala wa katiba mpya kwa kusimamia anachokiamini.

Bravo ACT!
 
Sure yupo vizuri sn
 
Kama ndio jina ambalo maalim Seif aliacha mezani mwake kabla ya kutwaliwa, basi ni mtu muafaka zaidi,

Kama ni jina lilipendekezwa na kamati ya uongozi wa ACT kwa muda huu mchache, basi kamati ina jicho la mbali.

Yanayobaki ni Othman Masoud mwenyewe kuprove beyond reasonable double kuhusu uwezo wake
 
Back
Top Bottom