OSHA imefanya nini kwa waajiri wakati huu wa korona?

Right3

Senior Member
Aug 16, 2015
193
233
Kwa ninavyofahamu OSHA ilipaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba waajiri wanapata maelekezo kuhusu namna mbalimbali ya kukabiliana na COVID 19 mahala pa kazi.

Pamoja na pesa kubwa wanazotoza wakati wa ukaguzi hawakufanya inavyofaa kuwaelekeza waajiri namna gani ya kufanya ili kufanya pahala pa kazi kuwa mahali bora kwa zile ofisi ambazo hazikua kwenye ''work from home''
Hata ukiangalia utakuta kuna page moja tu ambayo inasisitiza wataendelea kukagua ili wapate pesa na si kuhakikisha wanatoa maelekezo muhimu ili kuwasaidia waajiri na waajiriwa.

Kwa mtazamo wangu OSHA haina la maana imewasaidia waajiri na waajiriwaa wakati huu wa korona inawezekana hawatambui role yao sehemu za kazi wakati wa pandemic km hizi au ni kukosa tu ubunifu wa mkurugenzi na wafanyakazi wa hii taasisi.

Hawa walikua wadau muhimu wa kusaidia kutoa miongozo ya working from home, kutoa guidelines za kiusalama wakati huu wa COVID 19 kwa setor mbalimbali.

Nafikiri OSHA mnatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia wakati, pamoja na waajiri kulipa pesa nyingi za inspection muone pia umuhimu wa kusaidia wakati km huu.

Ingieni kwenye hii web ya OSHA US mjilinganishe na sio lazima mfike huko kwani sisi tunajuana tunastunted working model
 
  • Thanks
Reactions: 911
Back
Top Bottom