Orodha ya wilaya 10 zinazoongoza Kwa kuwa na watu wenye furaha Tanzania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
Herehoa Wakuu!

Baada ya kusoma orodha ya mataifa ishirini yanayoongoza Kwa furaha Duniani. Nikaona nami nilete orodha ya wilaya za watu wenye furaha hapa TANZANIA.

Ni Kama ifuatavyo;

1. Wilaya ya Morogoro Mjini.
Kama ulikuwa haujui Morogoro ndio sehemu pekee ambapo watu wake wanaishi Kwa furaha, hata Mgeni ukifika Morogoro mjini utajikuta unafurahia maisha.


2. Wilaya ya Kisarawe.
Huku nilipatembelea mwaka 2018 nikabaki kushangaa. Watu wa kisarawe wengi wao wanaishi Kwa furaha. Hapana maendeleo makubwa lakini watu wake watakushangaza. Wanafuraha tuu mpaka unajikuta nawe unafuraha.

3. Wilaya ya Kyela
Huku nilipatembelea miaka ya 2012.
Wanyakyusa bhana! Watu wa eneo hili wanashikilia nafasi ya tatu Kwa furaha hapa Tanzania. Sio kama ni matajiri au wanamaisha mazuri Sana lakini ukiishi nao siku tatu tuu hata Kama ulikuwa unahuzuni utashangaa furaha imekufunika.


4. Wilaya ya Tanga mjini.
Hawa jamaa wanafurahisha Sana. Wao hawana stress za kijinga jinga, maisha hawayachukulii Sirius ati yawapasue kichwa. Tanga mjini Raha Sana. Watu wake hata awe hana Mia mfukoni lakini huwezi msikia akinuna.

5. Wilaya ya Mufindi
Hawa jamaa licha ya baridi kuwa Kali lakini wanaishi maisha ya furaha mno. Sio watu wa kujitukukuza, wakazi wa Mafinga na viunga vyake licha ya kuwa baadhi Yao ni masikini lakini bado wanaishi Kwa Furaha.

6. Wilaya ya Bagamoyo
Hawa watu wa Pwani bhana! Unaweza sema wanapesa au matajiri kutokana na maisha furaha waliyonayo. Wao hupenda mizaha, kucheka na kucheza bao.

7. Wilaya za kigoma karibu zote.
Hawa watu wakigoma licha ya umasikini wa Maeneo Yao lakini sijui furaha wanaitolea wapi.
Kuna wakati naona furaha ya kweli hutoka moyoni mwa mtu.

Ukioa Mkigoma nakuhakikishia lazima uwe na furaha.

8. Wilaya ya Mbeya Mjini.
Watu wa Mbeya Mjini pia ni miongoni mwa watu wanaoishi Kwa furaha. Sio rahisi umkute Mtu wa Mbeya amenuna hata Kama anasura ngumu lakini bado utaiona ikiwa na furaha.

9. Wilaya ya Mafia
Hawa jamaa unaweza ukadhani hawapo nchini. Wanaishi Kwa furaha licha ya kuwa mazingira Yao sio mazuri kivile.

10. Wilaya ya Kibaha

Ajabu ni kuwa zile wilaya zilizotoa watu wanaojitahidi kuhangaika na maisha ya Duniani na zenye maendeleo ndio hizohizo zinaongoza Kwa kutokuwa na Furaha.

Nawasilisha
 
FURAHA YA KWELI?? Haipatikani kwenye mipira movies visingeri taarabu disko ngono kubeti pesa michepuko au utani na mengneyo kamwe watu hawataweza kupata furaha ya kwel mpaka hapo watakapojitoa kamili (TOTAL SURRENDER) Kwa KRISTO YESU.
 
Back
Top Bottom