Orodha ya wazee wanaoweza kutumiwa kuunda kamati ya kushauri uongozi hii hapa...

Kevin Isaya

JF-Expert Member
May 5, 2012
947
2,000
Bila kujali chama, au itikadi za ukanda,ukabila kama ilivyo kawaida ya watanzania, napendekeza lingekuwepo jopo la wastaafu wa kushauri mambo yafuatayo
 • Mwenendo wa siasa nchini..
 • Nidhamu na mienendo ya vyama vya siasa..
 • Marekebisho mbalimbali kuanzia katiba na kumshauri kiongozi yeyote yule ndan ya nchi kuanzia ngazi ya uwaziri mpaka urais.
 • Kutatua migogoro ya kisiasa nchini kama ule wa Zanzibar na mengineyo.
CCM imekuwa na wazee wa kushauri chama lakini hao hao wazee kuna baadhi ya mambo yanakwama nchini wanakaa kimya.

Hata upande wa upinzani kuna wazee makini wenye busara zao ambao wanaweza kutoa mchango wa mawazo.

NAPENDEKEZA ORODHA HII INGEUNDA KAMATI YA WAZEE WA TAIFA WA USHAURI

 1. Ali Hassan Mwinyi - Rais msataafu
 2. Benjamin Mkapa - Rais mstaafu
 3. Jakaya Kikwete - Rais mstaafu
 4. Abeid Karume - Rais mstaafu Zanzibar
 5. Jaji Sinde Warioba - Waziri Mkuu mstaafu
 6. Salim Ahmed Salim - Waziri Mkuu mstaafu
 7. John Malechela - Waziri Mkuu mstaafu
 8. Frederick Sumaye - Waziri Mkuu mstaafu
 9. Mzee Mtei - Gavana Mkuu wa benki mstaafu
 10. Peter Pinda - Waziri Mkuu mstaafu
 11. Mama Maria Nyerere - Mke wa Baba wa Taifa ( sababu maalum)
 12. Mzee Mboma - Mkuu wa Majeshi mstaafu
 13. Jaji Boman - Mwanasheria mzoefu
 14. Jaji Lubuva - Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
 15. Alfred Tibaigana - Kamishna wa Polisi mstaafu
 16. Samweli Sitta - spika wa Bunge mstaafu
 17. Professa Mwesiga Baregu
 18. Anna Makinda - Spika wa Bunge mstaafu
 19. Pius msekwa - Spika wa Bunge mstaafu
 20. Getrudi Mongella
 21. Prof Issa Shivji
 22. Anna abdalla
  23. Cleopa msuya
  24.Profesa sarungi
  25. Mzee Joseph butiku
  26. Mzee Paul Boman

Hiyo timu ingekuwa inakutana kila baada ya muda kujadili masuala muhim, pia kikao kiwe kinaudhuliwa na rais, waziri mkuu na makamu wa rais,

Kuna watu ambao labda hawastahili kuwa kwenye orodha hii kulingana na mtazamo wako.Pia unahisi ni yupi tumemsahau anastahili kuwepo katika orodha hiyo tuambie na aliyoyafanyia nchi na sifa zake.
 

Kevin Isaya

JF-Expert Member
May 5, 2012
947
2,000
Sababu hiyo maalum ipi?
Huyu mama anajua mambo mengi hata ambayo kina warioba SAA nyingine hawajuhi, pia anajua kila kitu au asilimia kubwa ya mission za Mme wake Mzee nyerere, SAA nyingine watu wanaweza wakawa wanapotoshana alafu ye anajua ukweli juu ya jambo ilo, kutokana na cases mbali mbali ambazo mwalimu alikuwa aki handle nyumbani kwake
 

Kevin Isaya

JF-Expert Member
May 5, 2012
947
2,000
Napendekeza ktk hyo orodha pawepo pia vijana wenye maono, mm naamin wazee peke yake kwasasa ushauri wao peke yao hautoshi kutikana na mwenendo wa dunia inavyobadilika, vijana km Yerriko Nyerere, Malisa na mtatiro wawemo
Vijana hapana wanapelekwa na hisia zaidi kuliko uhalisia Leo hii ukimjumuisha , polepole au makonda au mtatiro utavuruga mambo , ni wachanga sana hawa wanapelekwa na mapenzi binafsi

Note that : naposema makonda simaanishi namtamka kama rc, hapana hapa namtamka kama kaka yangu kwenye siasa, isinukuliwe vibaya eti namsema rc , hata kwa polepole ni hivyo si msemi mheshimiwa mkuu wa wilaya namsema polepole Humphrey
 

kwemanga1

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
836
1,000
Anna Abdallah, Pancras Ndejembi, Mufti wa TZ kwa nafasi yake, mwenyekiti wa TEC na CCT kwa nafasi zao, majaji wakuu wastaafu, IGP wastaafu, wakuu wa majeshi wastaafu makamishina wa tume ya maadili wastaafu, wanasheria wakuu wastaafu ni mapendekezo tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom