Orodha ya wastaafu na stahiki zao ambao huendelea kutunzwa na serikali mpaka umauti

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wanabodi,
Kwa mujibu wa Katiba yetu ya mwaka 1977, kuna ngazi ama level ya Uongozi ukishaifikia basi wewe utaendelea kuishi kwa gharama za serikali maisha yako yote hapa duniani (mpaka ufe).

1. Rais Mstaafu

2. Makamu wa Rais Mstaafu

3. Waziri Mkuu Mstaafu

4. Spika wa Bunge Mtaafu

5. Jaji Mkuu Mstaafu

6. Mkuu wa Jeshi la Wananchi Mstaafu (CDF)

7. Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP)

8. Mwanasheria Mkuu Mstaafu (AG)

Kuna sijui Majaji , Mabalozi, Makamishina , Mabrigedia etc etc nao wana stahiki fulani fulani maisha yao yote wanapostaafu.

Kuna stahiki katika maeneo makuu yafuatayo:-

1. Mshahara

2. Samani (Furniture)

3. Mawasiliano

5. Nyumba, umeme, maji

6. Ulinzi (24 hrs) na watumishi wa kumsaidia kazi zake kama mpishi , Katibu , Dereva , Secretary n.k

7. Safari za kwenda nje mara kadhaa hivi nchi uitakayo

8. Mavazi

9. Usafiri

10. Ofisi

Na mengineyo mengi yaliyojificha.
Ni kwa kiwango gani wanapewa hapo sijui. Kuna tetesi kuwa Waziri Mkuu Mstaafu anapata 80% ya mshahara wa Waziri Mkuu wa sasa.

Lets share.
 
Kumbukumbu zangu zimenikumbusha siku moja miaka kama minne sasa huenda imepita kwenye sherehe ya "Sheria au haki au sijui kitu gani vile" alikuepo Jk na alikuepo Judge Ramadhan, akasema kuwa "kama yeye ambaye alikua Jaji Mkuu anaondolewa ulinzi nyumbani kwake, je inakuaje kwa MTU wa chini??" ....
 
Ungemuuliza ile kadi ya CCM aliificha kwa miaka mingapi? Hadi akatoa uamuzi ule wa mgombea binafsi?
 
Kuliko kuumizana vichwa kuwa kuna baadhi ya watu wanafaidi sana keki ya taifa, bora tuendelee kuwaza namna maisha yatakavyokuwa baada ya kuwa ya chama kimoja.

Inatosha heshima waliyonayo wazee wetu, tuendelee kuwaheshimu na kuwaenzi.

Yajayo yanafurahisha.
 
Sumaye analalamika kua stahiki/malupulupu yake yamepunguzwa sana kama ninguo basi alikua na suruali lkn sasaiv amebaki na kipensi chakulalia
 
Wanabodi,
Kwa mujibu wa Katiba yetu ya mwaka 1977, kuna ngazi ama level ya Uongozi ukishaifikia basi wewe utaendelea kuishi kwa gharama za serikali maisha yako yote hapa duniani (mpaka ufe).

1. Rais Mstaafu

2. Makamu wa Rais Mstaafu

3. Waziri Mkuu Mstaafu

4. Spika wa Bunge Mtaafu

5. Jaji Mkuu Mstaafu

6. Mkuu wa Jeshi la Wananchi Mstaafu (CDF)

7. Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP)

8. Mwanasheria Mkuu Mstaafu (AG)

Kuna sijui Majaji , Mabalozi, Makamishina , Mabrigedia etc etc nao wana stahiki fulani fulani maisha yao yote wanapostaafu.

Kuna stahiki katika maeneo makuu yafuatayo:-

1. Mshahara

2. Samani (Furniture)

3. Mawasiliano

5. Nyumba, umeme, maji

6. Ulinzi (24 hrs) na watumishi wa kumsaidia kazi zake kama mpishi , Katibu , Dereva , Secretary n.k

7. Safari za kwenda nje mara kadhaa hivi nchi uitakayo

8. Mavazi

9. Usafiri

10. Ofisi

Na mengineyo mengi yaliyojificha.
Ni kwa kiwango gani wanapewa hapo sijui. Kuna tetesi kuwa Waziri Mkuu Mstaafu anapata 80% ya mshahara wa Waziri Mkuu wa sasa.

Lets share.

Kwa mujibu wa Sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma (The PSSSF Act) almaarufu Sheria ya Kikokotoo iliyotungwa wakati wa awamu hii ya tano na kuanza kutumika rasmi tarehe 09 Februari 2018, Mbali na kupewa mafao ya kustaafu kulingana na ngazi ya mshahara waliokuwa wanapata kabla ya kustaafu ambayo kikokotoo chake ni kwa kanuni ifuatayo: mshahara ghafi (basic salary) x miaka ya kazi x 144/540x15.5/2 (mfano Tshs. 4,000,0000 mshahara x miaka 30 x 144/540 x 15.5/2 = pensheni Tshs. 248,000,000/=) imeboresha kwa kuongeza marupurupu / mafao yanayotokana na kustaafu kwa baadhi ya watumishi kama Jaji Mkuu (Chief Justice), Majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Kamishna Jenerali wa jeshi la Zimamoto na Kamishna Mkuu wa Magereza kama ifuatavyo:

JAJI MKUU
  1. Hati ya kusafiria ya kibalozi (Diplomatic Passport) ya kwake na mwenza wake
  2. Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu yake ndani ya Tanzania
  3. Gari moja la kutembelea lisilozidi thamani atakayoamua Rais wa JMT kwa wakati huo; hili atapewa mara moja wakati wa kustaafu kwake
  4. Lita 70 kwa wiki za mafuta ya gari
  5. Dereva
  6. Ruhusa ya Kutumia ukumbi wa watu maalum (VIP Lounge)
  7. Posho ya mshahara kwa asilimia 50 ya jumla ya mshahara wote aliopokea wakati akiwa Jaji Mkuu
MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA NA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MKUU WA JESHI LA POLISI, MKUU WA MAGEREZA NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO
  1. Hati ya kusafiria ya kibalozi (Diplomatic Passport) ya kwake na mwenza wake
  2. Gari moja la kutembelea lisilozidi thamani atakayoamua Rais wa JMT kwa wakati huo; hili atapewa mara moja wakati wa kustaafu kwake
  3. Jumla ya Fedha za kutosha kulipa mishahara ya dereva kwa kipindi cha miaka 4, hii atapewa kwa mkupuo mmoja (lumpsome)
  4. Jumla ya Fedha za kutosha kununua Lita 50 kwa wiki za mafuta ya gari kwa kipindi cha miaka 4, hii atapewa kwa mkupuo moja (lumpsome)
  5. Jumla ya Fedha za matengenezo ya gari atazopewa kwa mkupuo moja (lumpsome) kiasi cha asilimia 40 ya fedha ya mafuta ya gari
  6. Ruhusa ya Kutumia ukumbi wa watu maalum (VIP Lounge)
MKUU WA KAYA (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
Kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) na (2) cha Sheria ya Mafao kwa Nafasi za Kisiasa Sura ya 225 (The Political Service Retirement Benefits Act CAP 225 R.E 2010) yeye akistaafu anapewa mafao yafuatayo:
  1. Mshahara kwa kiwango cha asilimia themanini ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani,
  2. Mafao ya kiinua mgongo kwa kiwango cha asilimia hamsini ya jumla ya mishahara yote aliyopokea kwa kipindi chote alichokuwa akishika ofisi ya Rais,
  3. Mafao ya kifuta jasho kwa kiwango cha jumla ya fedha ambazo angepokea Rais aliyepo madarakani kwa kipindi cha miezi ishirini na nne (miaka 2)
  4. Hati ya kusafiria ya kibalozi (Diplomatic Passport) ya kwake na mwenza au wenza wake (kama wapo wengi),
  5. Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu yake ndani ya Tanzania,
  6. Matengenezo kwa magari mawili kufanywa na serikali,
  7. Nyumba yenye samani zote isiyopungua vyumba vinne vya kulala na viwili vikiwa ni vya kujitegemea (self container) ikiwa pamoja na ofisi moja yenye samani zote na nyumba ya pembeni ya wafanyakazi (servant quarter),
  8. Atapewa na serikali ulinzi na huduma zote zihusianazo na usalama kwake na kwa familia yake,
  9. Katibu Muhtasi binafsi mmoja,
  10. Msaidizi binafsi mmoja,
  11. Mhudumu wa ofisi mmoja,
  12. Mpishi mmoja,
  13. Dobi mmoja,
  14. Mtumishi wa ndani mmoja,
  15. Mhudumu wa bustani mmoja,
  16. Madereva wawili,
  17. Ruhusa ya Kutumia ukumbi wa watu maalum (VIP Lounge).

Screen Shot 2019-12-06 at 7.40.08 AM.png

Screen Shot 2019-12-06 at 7.39.29 AM.png

Screen Shot 2019-12-06 at 7.37.53 AM.png

Screen Shot 2019-12-06 at 11.08.24 PM.png
 
Back
Top Bottom