Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

Wahehe hujawaona? Kimsingi kati ya Wakurugenzi 9; Mkoa wa Iringa ulitoa theluthi. Mzena, Kitine na Mahiga. Iringa(3), Kilimanjaro (2), Ruvuma(1), Songwe(1), Morogoro(1) na Tanga(1).
Wahehe wengi ni watu wanyenyekevu na watiifu kwa top leadership. Chukua kesi ya wafuasi wa Mkwawa jinsi walivyomficha mpaka later on akaamua jiua. 'Mhehe hashindwi vita' ndivyo wanasema.

Ukienda kwenye makumbusho yao pale Iringa wanasema kuanzia watoto,wanawake na jamii nzima walimlinda kiongozi wao Mkwawa kwa uri na dhim dhidi ya mkoloni Mjerumani.

Utii kwa uongozi ni sifa muhimu katika Intelijensia.

Lakini pia Mkwawa ni miongoni mwa Machifu wachache wa Tanganyika aliekuwa na kikosi cha Intelijensia kilicho relay information kutoka garrisons za Wajerumani Pwani ya Bahari ya Hindi hasa Bagamoyo juu ya ujio wa askaris wa Kijerumani kuingia bara kupambana na vikosi tiifu mwishoni mwa miaka ya 1800s.

Kumbuka target ya Mkwawa ilikuwa kutanua himaya yake hadi afike "kululenga" yaani Bahari ya Hindi which means himaya ya uhehe ianzie Njombe, Iringa, Dodoma,Morogoro, Lindi na Dar es salaam etc ila wakati anaendelea kujitanua njiani aka akakutana na kikwazo cha askari wa Kijerumani ambao tayari walikuwa washafika Pwani na wanaingia bara. Hapo ndo mnyukano ukaanza.

Wahehe ni miongoni mwa makabila yasiyo na unafikinafiki na ndio maana tatizo la tribalism miongoni mwa Hehe people ni dogo. Kwa Mhehe 'A' ya kiongozi ni 'A' kwake pia ila kwa baadhi ya DNA 'A' ya kiongozi ni 'B' kwake. How do you trust the latter kwenye nafasi nyeti kama za usalama wa nchi yetu.

Experience ni mwalimu mzuri. Once a leader always a leader. Once a betrayal always a betrayal

Mifano ya wasaliti pia ipo
 
KUNA WATU WAMEPATA CONNECTION KWA UTELEZI NA MTEREMKO HADI RAHA.

KIPINDI CHA NYUMA WAMUJIBU JKT WALIKUWA WANACHAGULIWA NA KUCHUKULIWA JAPO SASA NI
WA KUJITOLEA,BASI KUNA INTAKE WALIKUWA NA MTOTO WA TISS.

AKAWATONYA HANGA ZIMA KWAMBA WATAKAOKUJA KESHO KUFANYISHA INTERVIEW NI TISS.
JAMAA KAMA 30 WAKAENDANA TS WALITAKA WATU WANAOTAKA KUFANYA USAFI MBANDARINI.
KWANI JAWATANGAZAGI MOJA KWA MOJA NA SASA NI TS WAKUBWA TUUU
Story za vijiwe vya kahawa mbichi
 
Hahaaa, kuna bibi mmoja Mmarekani alikuwa jirani yangu, yeye anasema hana matatizo na gay people, tatizo lake wamelichukua neno gay, lililokuwa na maana ya kuwa na furaha, wakaliteka na kulibadilisha na kulipa maana mpya kabisa.

That word, in that meaning, is so quaint.

It's like reading Fitzgerald, Steinbeck or Hemingway today!
Semantic broaderning ata neno madam ilikuwa ni la head of prostitute lakini saivi ni neno la any employed women
 
ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.

Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.

Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyepo kwa sasa

Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.

Wa pili ni Dr. Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Wa tatu ni Dr. Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr. Agustine Mahiga (PhD) - (Marehemu) ambaye alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Waziri wa Sheria chini ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.

Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha Kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.

June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".

Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.

Baada ya Kombe kuuawa alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza Idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Cornel Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Cornel Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.

Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza Idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.

August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr. Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).

Mchungaji Dr. Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.
Huyu mzee Mzema tunatoka kijiji kimoja
 
Ww toa TAARIFA na sio maelekezo
Taarifa gani zaidi ya nilivyokwisha andika?

Unayoita maelekezo ni kwa sababu wewe ulitaka nirudie niliyokiwsha andika ndiopo maana nikakuambia soma huko nyuma upate storyline kamili. Hatujadili kwa kurudia mambo yale yale ndiyo maana kuna rekodi za kudumu
 
Hivi unajua huu uzi unakuzidi sana kimo, si ukae usome tu. Yani unaulizauliza vitu vya wazi, chuo gani kwanza umesoma wanatoa graduates kama wewe?
Ww unamatatizo ya mapmb kabisa Amna mtu anaitwa jina Hilo alikuwa mkuu wa TISS
 
Hivi unajua huu uzi unakuzidi sana kimo, si ukae usome tu. Yani unaulizauliza vitu vya wazi, chuo gani kwanza umesoma wanatoa graduates kama wewe?
Kuna Nzena na mzena na Mnzwema wewe unamjua nani na makalio yako????
 
Wahehe wengi ni watu wanyenyekevu na watiifu kwa top leadership. Chukua kesi ya wafuasi wa Mkwawa jinsi walivyomficha mpaka later on akaamua jiua. 'Mhehe hashindwi vita' ndivyo wanasema.

Ukienda kwenye makumbusho yao pale Iringa wanasema kuanzia watoto,wanawake na jamii nzima walimlinda kiongozi wao Mkwawa kwa uri na dhim dhidi ya mkoloni Mjerumani.

Utii kwa uongozi ni sifa muhimu katika Intelijensia.

Lakini pia Mkwawa ni miongoni mwa Machifu wachache wa Tanganyika aliekuwa na kikosi cha Intelijensia kilicho relay information kutoka garrisons za Wajerumani Pwani ya Bahari ya Hindi hasa Bagamoyo juu ya ujio wa askaris wa Kijerumani kuingia bara kupambana na vikosi tiifu mwishoni mwa miaka ya 1800s.

Kumbuka target ya Mkwawa ilikuwa kutanua himaya yake hadi afike "kululenga" yaani Bahari ya Hindi which means himaya ya uhehe ianzie Njombe, Iringa, Dodoma,Morogoro, Lindi na Dar es salaam etc ila wakati anaendelea kujitanua njiani aka akakutana na kikwazo cha askari wa Kijerumani ambao tayari walikuwa washafika Pwani na wanaingia bara. Hapo ndo mnyukano ukaanza.

Wahehe ni miongoni mwa makabila yasiyo na unafikinafiki na ndio maana tatizo la tribalism miongoni mwa Hehe people ni dogo. Kwa Mhehe 'A' ya kiongozi ni 'A' kwake pia ila kwa baadhi ya DNA 'A' ya kiongozi ni 'B' kwake. How do you trust the latter kwenye nafasi nyeti kama za usalama wa nchi yetu.

Experience ni mwalimu mzuri. Once a leader always a leader. Once a betrayal always a betrayal

Mifano ya wasaliti pia ipo
Kwa unafiki sina uhakika...
 
Back
Top Bottom