Orodha ya wabunge wa CCM waliowahi kujiuzulu ubunge

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Ninaowakumbuka,

1. Augustine Lyatonga Mrema, alikuwa mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), 1995 alijiengua na kujiunga na NCCR-MAGEUZI.

2. Rostam Azizi, alikuwa mbunge wa Igunga (CCM), June 2011, huyu aliachana kabisa na siasa uchwara.

3. Lazaro Nyalandu, alikuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Oct. 2017 alijiengua na kujiunga na CHADEMA.

4. Fred Mpendazoe, alikuwa mbunge wa Kishapu (CCM), March 2010 alijiengua CCM akiwa mbunge ili kuanzisha chama kipya cha CCJ.

5.

Kama unamkumbuka mbunge yeyote please ila ni yule 'aliyejiuzulu' ubunge tu.
 
Ndugu zangu,

Nimekumbushia hilo mara nyingi, kwamba historia ni Mwalimu Mzuri. Hata kama wengine mlikuwa hamjazaliwa, lakini, hakuna marufuku ya kusoma historia.

Tunapochambua haya yanayotokea sasa wengine wetu tunaitazama historia.

Ni ukweli wa kihistoria, kuwa CCM ni zaidi ya Chama, ni taasisi kubwa yenye kugusa maisha ya kila mmoja wetu, hata akiwa nje ya CCM.

Sio tu kwa kusoma historia, nina bahati ya kushuhudia miongo minne ya matukio makubwa ya kisiasa katika nchi hii nikiwa na ufahamu na kiu ya kujifunza.

Nimesoma matukio ya TANU kutikiswa kisiasa, zama za Mwalimu. Nimeshuhudia matukio ya CCM kutikiswa kisiasa, zama za Mzee Mwinyi. Vivyo hivyo kwenye zama za Mkapa na juzi tu Jakaya Kikwete.

Katika wote waliohama CCM na waliotarajiwa wangeitikisa CCM ikayumba sana ni Profesa Kighoma Ali Malima. Huyu alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Hazina. Alikuwa msomi na mwenye ushawishi ndani ya Chama chake. Haya ya sasa, ingelikuwa enzi zile, Lazaro Nyalandu ingelikuwa ni jina maarufu kwenye vijiwe vya mtaani tu, wala si jina la kutisha ndani ya CCM.

Kwenye Daily News, Julai 17, 1995, iliripotiwa kama ifuatavyo:
" Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Viwanda, Kighoma Ali Malima, ameondoka CCM na kujiunga na Chama chake kipya cha National Reconstruction Alliance ( NRA).

Malima alitangaza hayo kwenye mkutano mjini Tabora, na anatarajiwa kuwa mgombea Urais kupitia NRA." - Daily News, Julai 17, 1995.

Siku ya pili yake, Julai 18, 1995, Kwenye Daily News, Katibu Mwenezi wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alilipotiwa akitoa kauli juu ya hatua hiyo ya Malima, kwa kutamka.

" Alichofanya Malima hakina maana yeyote kwa CCM!"

Ni nani anayejiuliza leo mchango wa Mzee Kingunge kwenye kutufikisha hapa?

Naam, historia ni Mwalimu Mzuri.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
 
Ninaowakumbuka,

1. Augustine Lyatonga Mrema, alikuwa mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), 1995 alijiengua na kujiunga na NCCR-MAGEUZI.

2. Rostam Azizi, alikuwa mbunge wa Igunga (CCM), June 2011, huyu aliachana kabisa na siasa uchwara.

3. Lazaro Nyalandu, alikuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Oct. 2017 alijiengua na kujiunga na CHADEMA.

4. Fred Mpendazoe, alikuwa mbunge wa Kishapu (CCM), March 2010 alijiengua CCM akiwa mbunge ili kuanzisha chama kipya cha CCJ.

5.

Kama unamkumbuka mbunge yeyote please ila ni yule 'aliyejiuzulu' ubunge tu.
Hawa waliojiuzulu walijiuzulu kwa maslahi ya nani?
 
5. Edward Lowassa alikuwa mbunge wa Monduli, mwaka 2015 alijiuzuru ubunge huo na kuhania chadema ambako aliteuliwa kwa njia isiyokuwa ya kidemokrasia kuwa mgombea wa kiti cha urais. Hadi leo ni mwanachama wa ccm kwani hajawahi kujiuzuru wala kufukuzwa uanachama huo wala kurudisha kadi ya uanachama wake wa ccm na havai uniform ya chama alichoko kwa sasa!

7. Fredrick Sumaye alikuwa mbunge wa Hanang'i. Mwaka 2010 baada ya kumaliza uwaziri mkuu kwenye kura za maoni kuwania jimbo hilo aliangushwa na Mary Nagu. Akajaribu kuwania urais mara tatu ikashindikana. Akahamia chadema ili kuwa kampeni meneja wa Lowasa kwa kiti cha urais. Kama mwenzake Lowassa hajawahi kirudisha kadi za uanachama wao wa ccm wala kujiuzuru au kufukuzwa cccm -- labda kwa sababu waliwahi kuwa mawaziri wakuu na wana ulinzi wa serikali.

7. Lembeli alikuwa mbunge wa Kahama, alihamia chadema 2015 baada ya jina lake kukatwa.

8. Esther Bulaya aliyekuwa mbunge wa viti maalum. Mwaka 2015 alionyesha nia ya kugombea ubunge wa jimbo la kwao huko Bunda kwa tiketi ya ccm lakini jina lake likakatwa na kubaki la Wassira. Akahamia chadema ambako faster faster akateuliwa kugombea jimbo hilo na kuchuana na Wassira na kufanikiwa kulotwaa jimbo hilo.

NB: Ukiacha Nyarandu, hao wabunge wengine walihamia vyama vingine karibu na mwisho wa ubunge wao baada ya kuona kuwa hawatafanikiwa kupata fursa ya kuendelea na ubunge au kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Yaani kwenye hiyo orodha Nyarandu is the odd man out. Ndiyo maana watu wanajiuliza kitu gani kiko nyuma ya Nyarandu? Jee, ni azima yake tu ya kumpeleka mwana Singida mwenzake Tundu Lissu marekani kwa matibabu zaidi kama ambavyo aliwapeleka wale watoto wa shule wa ile ajali mbaya iliyotokea huko Arusha? What does he benefit from it hadi aachie ubunge? Jee ni hasira tu ya kutoteuliwa uwaziri na badala yake wizara hiyo akapewa Kigwangala? Jee kujiuzuru kwake kuna uhusiano na fukua fukua inayofanywa sasa kwa wizara yake ya zamani kuhusiana na mikataba ya kifisadi kwenye mbuga zetu za wanyama?
 
Kujiuzulu kwa Nyalandu hakuwezi kutenganishwa na maslahi binafsi. Kihesabu kujiuzulu kwake ni nafuu zaidi kimaslahi kuliko kutojiuzulu. Undani unajua yeye lakini kitendo hicho kwake kinafaida kweke zaidi kuliko kubaki alipokuwa.
 
5. Edward Lowassa alikuwa mbunge wa Monduli, mwaka 2015 alijiuzuru ubunge huo na kuhania chadema ambako aliteuliwa kwa njia isiyokuwa ya kidemokrasia kuwa mgombea wa kiti cha urais. Hadi leo ni mwanachama wa ccm kwani hajawahi kujiuzuru wala kufukuzwa uanachama huo wala kurudisha kadi ya uanachama wake wa ccm na havai uniform ya chama alichoko kwa sasa!

7. Fredrick Sumaye alikuwa mbunge wa Hanang'i. Mwaka 2010 baada ya kumaliza uwaziri mkuu kwenye kura za maoni kuwania jimbo hilo aliangushwa na Mary Nagu. Akajaribu kuwania urais mara tatu ikashindikana. Akahamia chadema ili kuwa kampeni meneja wa Lowasa kwa kiti cha urais. Kama mwenzake Lowassa hajawahi kirudisha kadi za uanachama wao wa ccm wala kujiuzuru au kufukuzwa cccm -- labda kwa sababu waliwahi kuwa mawaziri wakuu na wana ulinzi wa serikali.

7. Lembeli alikuwa mbunge wa Kahama, alihamia chadema 2015 baada ya jina lake kukatwa.

8. Esther Bulaya aliyekuwa mbunge wa viti maalum. Mwaka 2015 alionyesha nia ya kugombea ubunge wa jimbo la kwao huko Bunda kwa tiketi ya ccm lakini jina lake likakatwa na kubaki la Wassira. Akahamia chadema ambako faster faster akateuliwa kugombea jimbo hilo na kuchuana na Wassira na kufanikiwa kulotwaa jimbo hilo.

NB: Ukiacha Nyarandu, hao wabunge wengine walihamia vyama vingine karibu na mwisho wa ubunge wao baada ya kuona kuwa hawatafanikiwa kupata fursa ya kuendelea na ubunge au kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Yaani kwenye hiyo orodha Nyarandu is the odd man out. Ndiyo maana watu wanajiuliza kitu gani kiko nyuma ya Nyarandu? Jee, ni azima yake tu ya kumpeleka mwana Singida mwenzake Tundu Lissu marekani kwa matibabu zaidi kama ambavyo aliwapeleka wale watoto wa shule wa ile ajali mbaya iliyotokea huko Arusha? What does he benefit from it hadi aachie ubunge? Jee ni hasira tu ya kutoteuliwa uwaziri na badala yake wizara hiyo akapewa Kigwangala? Jee kujiuzuru kwake kuna uhusiano na fukua fukua inayofanywa sasa kwa wizara yake ya zamani kuhusiana na mikataba ya kifisadi kwenye mbuga zetu za wanyama?
Rostam alijiuzuru kipindi kipi? Alikuwa amebakisha muda gani kwenye ubunge wake kukoma kwa mujibu wa sheria?
 
Back
Top Bottom